UZUSHI Unywaji wa Bia kwa wingi kwa mwanaume hupelekea kuongezeka kwa homoni za kike, na mwisho husababisha ugumba

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Je, Kuna ukweli kuwa unywaji wa Bia kwa wingi kwa mwanaume hupelekea kuongezeka kwa homoni za kike, na mwisho kupelekea mwanaume kupata ugumba?


Video inayozungumziwa (Chanzo: Times FM)

360_F_294065866_b5ICb79vwYER5mwvk9wMLbcfMxnV3GWU.jpg

Picha ya Mwanaume aliyelewa pombe (Picha: Adobe Stock)
 
Tunachokijua
Januari 16, 2024, Kituo cha Times FM kupitia Channel yao ya YouTube walirusha mojawapo ya vipindi vyao kikizungumzia masuala anuai ya Afya. Kwenye video hii, wapo watangazaji wawili na Mtu mmoja waliyemtambulisha kwa jina la Dkt. Greyson.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Greyson alinukuliwa akisema "Bia imetengenezwa kwa shayiri, shayiri ile huwa na homoni za kike kwahiyo wanaume wanaokunywa sana bia huwa na homoni za kike. Wanaume wanaokunywa sana bia wapo kwenye hatari ya kupata ugumba kutokana na kuwa na wingi wa homoni za kike"

Kauli hii ilileta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Mathalani, Januari 23, 2024, Mtumiaji wa Mtandao wa Instagram (Bongomixed_habari) alichapisha video hiyo ikiambatana na ujumbe unaosema "Fani ya udaktari imeingiliwa"

Ukweli upoje?
JamiiCheck imezungumza na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dkt. Godfrey Chale anayepatikana Jijini Dar es Salaam anafafanua:

"Hakuna ukweli juu ya suala hilo, bia ina Carbohydrates nyingi na wengi wanaokunywa huwa wanaishia kunenepa kama wanakula vizuri pia, japokuwa wapo watu ambao wanakunywa na kula vizuri lakini hawanenepi.

Inawezekana labda kuna aina za bia mpya ambazo anazizungumza huyo mtoa hoja, kwa kuwa bia ni nyingi, lakini bila standard zinazojulikana hazina madhara hayo ya mabadiliko ya homoni, kwamba Mwanaume mnyaji anapata homoni za kike."


Dkt. Chale amemalizia kwa kusema kuwa Kitaalamu unapozungumza vitu vya aina hiyo unatakiwa kuzungumza ukiwa na mifano ya tafiti na uwe na uthibitisho kuwa kilifanyika hiki na hiki hadi matokeo ya aina hiyo yaonekane.

Ugumba ni ni hali ya kushindwa kuzalisha kwa mwanaume na kwa mwanamke ni kushidwa kushika ujauzito baada ya majaribio kwa muda wa mwaka mzima. Kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 35, ina maanisha umeshindwa kupata ujauzito baada ya miezi 6 ya majaribio.
Zambians, Zimbabweans, south africans, wanakunywa mno beers 🍻 na wanazaana kama simbilisi
 
Mtu anaamka zake huko kala makande yaliyochacha anaanza kutema pumba tupu na baadhi ya watu wanampa attention... Wataalam wamekaa tu huko wanamchora

BEER IHESHIMIWE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom