Msongo wa mawazo huongeza nafasi ya kupatwa na kifo cha Ghafla kwa 43%

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
575
2,559
Mtu mwenye Msongo wa Mawazo huwa na 43% zaidi ya kupatwa na Kifo cha Ghafla kuliko mtu asiye na tatizo hili

Pia, huongeza nafasi ya kuugua Magonjwa sugu, kujiingiza kwenye tabia hatarishi kama unywaji wa Pombe uliopindukia, uvutaji wa Sigara na Matumizi ya Dawa za kulevya.

Wanawake wajawazito kupata Msongo wa Mawazo
Kwa mujibu wa tafiti, takriban 84% ya wanawake wajawazito hupatwa na Msongo wa Mawazo utokanao na Mabadiliko ya Homoni za mwili

Hali hii huharibu Usingizi pamoja na kuongeza hatari ya kupatwa na Shinikizo kubwa la Damu, kuharibika kwa Ujauzito kabla ya wiki ya 20, Kifafa cha Mimba au Kujifungua kabla ya wakati

Mahudhurio ya mara kwa mara ya kliniki husaidia kubaini hali hii na kuondoa hatari zote zinazoambata nayo.

Afya ya uzazi
Msongo wa Mawazo huathiri afya ya Uzazi kwa kupunguza ufanisi wa Kushiriki tendo la Ndoa kwa Wanaume, kuathiri uzalishwaji wa Mbegu za Kiume pamoja na kusababisha Ugumba.

Kwa wanawake, husababisha kuharibika kwa Mzunguko wa hedhi, Ukavu wakati wa kushiriki tendo la Ndoa pamoja na Mvurugiko wa homoni za mwili.

Ufuatiliaji wa mapema wa dalili hizi husaidia upatikanaji wa Matibabu ya haraka pamoja na kuboresha hali ya Maisha ya kawaida ya Mhusika.

Msongo wa mawazo kwa watoto
Kama ilivyo kwa watu Wazima, Watoto wanaweza pia Kupatwa na Msongo wa Mawazo

Changamoto za Kimasomo, Unyanyasaji, Ugomvi wa Wazazi na Mabadiliko wanayopitia wakati wa Umri wa Balehe ni miongoni mwa mambo yanayotajwa na Tafiti kuwa chanzo cha Kutokea kwa hali hiyo

Wazazi na Walezi wanapaswa kutenga Muda wa kukaa na Watoto ili Kusikiliza Changamoto zao na Kuzipatia Majibu Stahiki kabla hazijawaleta Madhara, ikiwemo kupawafanya wapatwe na Msongo wa Mawazo

Msaada wa kukufanya uondokane na changamoto hii upo karibu yako, kwenye jamii unayoishi. Vunja ukimya

Pia, unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kuikabili hali hii;
  • Tembelea ndugu, jamaa na marafiki unaowaamini
  • Toa muda wako kwenye mambo ya kijamii na kiimani
  • Andika kila siku mambo mazuri yaliyowahi kukupa furaha kwenye maisha yako
  • Pata muda wa kupumzika
  • Shiriki mazoezi
Aidha, unaweza pia kusikiliza muziki na kufumba macho huku ukivuta pumzi taratibu.

Chanzo: NIH/ Healthline
 
Duh wengine tunatumbukia kwenye ulevi lkn bado hali ni ile ile napitia kipindi kigumu cjawahi kukitarajia
Daah pole sana ndugu , jitaidi kukamjlisha mambo machine kati hayo waliyotaja wataftit apo , ukiwa na mawazo kama hivo jitaidi kusikikiza hata mziki , au fanya mazoezi hata ya kukimbia ,itakusaidia sana na kukutoa kwenye kutumia pombe na vitu vingine mama madawa
 
Back
Top Bottom