Unyanyasaji kwa wanafunzi (wao kwa wao) Leo tuzungumze kidogo juu ya wanafunzi mashuleni

Mar 25, 2024
20
28
Wazazi, hivi huwa mnaketi na watoto wenu na kuzungumza nao juu ya maisha Yao shuleni? J

uzi kwenye MITANDAO ya KIJAMII imesambaa video ikimuonesha Binti aliejulikana kwa Jina la "Mariamu" akimpiga mwanafunzi mwenzie Aliejulikana kwa Jina la "Namtira "sababu kubwa ikidaiwa kuwa karibu na "crush " wake.

Hili swala limezua taharuki Sana, lakini kwa upande wetu wa Tanzania tunaona hili ni suala la kawaida Sana, wazazi tukumbuke kuwa watoto wetu mashuleni wanakutana na mambo mengi ambayo yanawanyima confidence na inaweza kufanya matokeo Yao kuwa mabaya darasani.

Sasa ukiangalia huyo mwanafunzi anavopigwa vibao unahisi akienda shuleni atakuwa na amani darasani? Wakati huo hao ndo anaoshirikiana nao.

Sasa hapa naongea na wazazi wa Kitanzania, Mama, Baba, Jenga tabia ya kuzungumza na Mtoto wako, yapi yanamkuta hasa huko shuleni.
 
Back
Top Bottom