Msukusu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2022
- 216
- 409
Wakubwa habari zenu mimi ni kijana wa 30+ na hivi karibuni natarajia kupata mtoto wa pili, majaliwa ya mwenyezi mungu.
Haya tujikite kwenye mada hapo juu, kwa jamii ninayo ishi nimeshuhudia vitendo viovu na maadili mabaya hasa kwa wadogo zetu, wengine watoto ambao unao uwezo wa kumzaa.
Nilishuhudia mtoto wa miaka saba anamjibu mama mmoja vibaya, pale alipoambiwa aende nyumbani kuoga, mtoto alimjibu achana na mimi kwani wwe ni mama yangu.
Kisa cha pili kuna kibinti cha kidato cha pili mara nyingi sana naona, hasa wadada na kina mama wanavaa kanga moko na nguo ya ndani halafu wanaenda gengeni, mara nyingi hutokea nyakati za jioni au asubuhi sababu sijui.
Basi huyo binti alikuwa anakatiza kwa watu wazima wamekaa na hiyo kanga moko yake, kuna mubaba mmoja alikuwa anamuangalia sana, yule binti akamwambia mbona unaniangalia sana unataka k.
Kama unataka sema sio kunitolea mimacho. Twende mashuleni kipindi tunasoma wale waliozaliwa miaka ya 80 na 90 tulichapwa sana viboko mashuleni.
Sio shuleni tu hadi wazazi walitutandika sana viboko pale tulipokosea. Kipindi tunasoma ukikutana na mwalimu hujachomekea ni viboko sana, kwa sasa unaweza pishana na wanafunzi wa kiume hajachomekea na mwalimu ukimuadhibu kwa viboko utatengenezewa kamati.
Wasichana ukikutwa umefuga kucha au kupanga rangi ni viboko, kwa kizazi hiki hakuna mwalimu anayeshughulika na wewe ufuge kucha, upake rangi utajijua kimpango wako. Kumiliki simu shuleni ni sawa umekutwa na nyara za serikali au biashara haramu.
Na pia ilikuwa ni kosa la kumfukuza mwanafunzi shule pale utakapokutwa simu, kwa sasa mwanafunzi wa kidato cha kwanza anamiliki simu, walimu hawana muda wa kukemea na wala wazazi hawana muda huo.
Walimu naona watoto wamewashindwa wao kwa sasa wanafundisha tu ili mradi mishahara inaingia, habari ya kukipizana au kuchapa mtoto wa mtu hawana habari hizo.
Na tunajua kabisa swala la maadili ni kijamii nzima. Wazazi ndio wa kwanza kabisa wanaofuata ni walimu sababu kule mashuleni watoto wetu wanakutana na watoto wenzao walio lelewa na familia tofauti.
Jamii inapopinga viboko mashuleni je wazazi mtaweza kuwalea watoto wenu kwenye maadili mema?