Tuache kuhukumiana mungu ni mwingi wa kusamehe binaadamu wana nongwa wengine hawajuu kusamehe hata wakiombwa msamaha, mtu kama ametubu toba ya kweli kwa mungu wake tuna amini amrsamehewa mungu hana roho mbaya kama yako ya kutopenda kusamehe siyo lazima mtu akufuate kuna mazingira mengine hayaruhusu hayo huwezi kuwafuata wote uliyowahibkuwakosea, hakuna binadamu aliyekamilikaUtasikia
fulani alikuwa jambazi hapo zamani kwa sasa kaokoka
Fulani alikuwa tapeli sugu hapo zamani kaamua kuokoka
Fulani alivunja ndoa za wengi hapo zamani kaamua kuokoka
NONSENSE, UJINGA!!
Mnakosea sana, Mnjidanganya, Mambo hayendi hivyo !!
1. TUACHE MASIKHARA KWA MUNGU WA HAKI
Ulikuwa jambazi umeibia watu, wameshindwa kuendelea kwajili yako, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliowaibia
Ulikuwa mzinzi, umekuwa chanzo cha ndoa za watu kuvunjika, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa mme / mke uliemvunjia ndoa
Ulikuwa muuaji, umeua baba, familia zinateseka, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliewaulia baba
Ulikuwa dhulumati, umedhulumu watu, wanaishi maish ya dhiki, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliowadhulumu
2. MIFANO
Baada ya Daudi kushika madaraka nchi ikawa ina majanga, alipomuuliza Mungu nini chanzo, aliambiwa utawala uliopita wa Sauli uliua wana watu wa Gibeon hivyo waende kwao wayamalize,baada ya hapoataitakasa nchi, walipoenda huko wa Gibeon waliwambia wao hawataki dhahabu wala Silver, wanataka kulipiza kisasi, wawape wana wa Sauli wa kiume saba wawaue na walipofanya hivyo nchi ilitakaswa.
Mfano mwingine Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake kwamba kabla ya kutoa sadaka kaweke kwanza mambo sawa na uliowakosea, pia alishauri patana na mshitaki wako kwanza kabla hamjafika kwa hakimu
Mfano mwingine wa zakayo alikumbuka dhambi zake na akasema atawarejeshea mara kumi aliowadhulumu, bda ya hapo ndipo aliweza kupokea wokovu
3. AGANO LA KALE LILIRUHUSU JICHO KWA JICHO, JIPYA JE ?
Agano la kale liliruhusu kulipiza jino kwa jino kama huo mfano wa kwanza wa kulipiza kisasi kwa kuua lakini haimaanishi agano jipya limefuta kila kitu, kilichobadilika ni kwamba mtu aliekukosea akija kukuomba msamaha haupaswi kulipizajino kwa jino, ni aidha umsamehe au kama roho inasita wewe mwambie wazi tu huwezi, hakuna haja ya kulipiza kwa jinsi alivyokuumiza
4. HAIWEZEKANI KUOKOKA BILA KUPATA TIKETI YA MSAMAHA WA ULIOWAUMIZA
Ni hivi, Mungu sio dhalimu,wewe unaweza kukuta umenitendea mabaya halafu unaenda kanisani kuokoka lakin unasahau mimi kila asubuh naamka na majereaha uliyoniachia aidha umeniibia duka nimefirisika, umeua watu wangu wa karibu naumia, umeniibia mke ndoa ilivunjika, umenidhulumu kiwanja sina nyumba, n.k.
Mungu hawezi kusahau uovu ulionifanyia kisa eti umebadilika, unaenda sana kanisani, unatoa sadaka (zikiwemo pesa ulizonidhulumu ), n..k NEVER !!!! Na kuhakikishia Mungu ni wa haki hata sikia sala yako ya kuokoka kama hutotubu maovu yako kwa uliowaumiza, Mungu haongeki !!!
5. MWISHO KABISA
Mwenyezi Mungu anachukizwa mno na dhambi, hakikisha unajizuia sana kutenda dhambi kuumiza wengine na ukifanya hivyo fanya uwezavyo uwaombe msamaha, ndio tiketi pekee ya kuomba msamaha kwa Mungu