Umeumiza watu halafu unataka kuokoka bila kuwaomba msamaha uliowaumiza, hilo haliwezekani!

gearbox

Senior Member
Apr 20, 2024
151
382
Utasikia, fulani alikuwa jambazi hapo zamani kwa sasa kaokoka, fulani alikuwa tapeli sugu hapo zamani kaamua kuokoka au fulani alikuwa mbakaji hapo zamani kaamua kuokoka. NONSENSE, UJINGA! Mnakosea sana, mnjidanganya, mambo hayendi hivyo!

1. TUACHE MASIKHARA KWA MUNGU WA HAKI

Huwezi kuroga watu wakapatwa magonjwa na matatizo mengine halafu uanze kutafuta wokovu eti unasalimisha matunguli yako kanisani yachomwe, Mungu wa haki hawezi kukubali huo msamaha !! anza kwa kuwaomba msamaha uliowachawia na utegue vifungo !!

Umedhulumu shamba la mtu kisa masikini, unavuna kila mwaka huku familia yake wanalala njaa ama chakula hakiwatoshi kwajili yako, Unajidai kupeleka sadaka kanisani kwa mavuno ya shamba la wizi eti unatafuta wokovu, Mungu wa haki hawezi kukubali huo msamaha !! anza kwa kurudisha shamba na uombe msamaha


Huwezi kudhulumu mali ya masikini au yatima halafu uanze kutafuta wokovu, Mungu wa haki hawezi kukubali huo msamaha !! anza kwa kurudisha ulivyoiba na kuwaomba msamaha wahusika !!

Huwezi kufarakanisha wanandoa wakaachana halafu uanze kutafuta wokovu, Mungu wa haki hawezi kukubali huo msamaha !! anza kwa kuwaomba msamaha uliowafarakanisha !!

Huwezi kuua watu wanaacha familia zao halafu uanze kutafuta wokovu, Mungu wa haki hawezi kukubali huo msamaha !! anza kwa kuwaomba msamaha wanafamilia wake !!

shinda kanisani muda wote, sikiliza gospel siku nzima, toa sana sadaka, vaa mashati ya vitenge, n.k. Mungu wa haki hawezi kukubali msamaha wako, anzia kwanza kwenye chanzo cha watu uliowaumiza !!

2. MIFANO

Baada ya Daudi kushika madaraka nchi ikawa ina majanga, alipomuuliza Mungu nini chanzo, aliambiwa utawala uliopita wa Sauli uliua wana watu wa Gibeon hivyo waende kwao wayamalize, baada ya hapoataitakasa nchi, walipoenda huko wa Gibeon waliwambia wao hawataki dhahabu wala Silver, wanataka kulipiza kisasi, wawape wana wa Sauli wa kiume saba wawaue na walipofanya hivyo nchi ilitakaswa.

Mfano mwingine Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake kwamba kabla ya kutoa sadaka kaweke kwanza mambo sawa na uliowakosea, pia alishauri patana na mshitaki wako kwanza kabla hamjafika kwa hakimu.

Mfano mwingine wa zakayo alikumbuka dhambi zake na akasema atawarejeshea mara kumi aliowadhulumu, bda ya hapo ndipo aliweza kupokea wokovu.

Mfalme Daudi alimuua Uria ili Daudi aweze kumuoa mke Uria. Kilichotokea ili kulipa hyo dhambi mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mke wa Uria alikufa ndo Daudi akapata msamaha wa Mungu.

3. AGANO LA KALE LILIRUHUSU JICHO KWA JICHO, JIPYA JE?

Agano la kale liliruhusu kulipiza jino kwa jino lakini haimaanishi agano jipya limefuta kila kitu, agano jipya linatusihi zaidi tupendane hivyo kilichobadilika ni kwamba mtu aliekukosea akija kukuomba msamaha haupaswi kulipiza jino kwa jino, ni aidha umsamehe au kama roho inasita wewe mwambie wazi tu huwezi, hakuna haja ya kulipiza.

Na kwa mawazo yangu navyoona kwamba mwenye dhambi kama hajabatizwa anaweza kusamehewa dhambi zake moja kwa moja ikiwa yupo tayari kumpkea Yesu, lakini baada ya hapo kigezo chako cha kusamehewa kinakuwa kizito zaidi, na kumbuka kubatizwa huwa ni mara moja tu

4. HAIWEZEKANI KUOKOKA BILA KUPATA TIKETI YA MSAMAHA WA ULIOWAUMIZA

Ni hivi, Mungu sio dhalimu,wewe unaweza kukuta umenitendea mabaya halafu unaenda kanisani kuokoka lakin unasahau mimi kila asubuh naamka na majereaha uliyoniachia aidha umeniibia duka nimefirisika, umeua watu wangu wa karibu naumia, umeniibia mke ndoa ilivunjika, umenidhulumu kiwanja sina nyumba, n.k.

Mungu hawezi kusahau uovu ulionifanyia kisa eti umebadilika, unaenda sana kanisani, unatoa sadaka (zikiwemo pesa ulizonidhulumu ), n..k NEVER !!!! Na kuhakikishia Mungu ni wa haki hata sikia sala yako ya kuokoka kama hutotubu maovu yako kwa uliowaumiza, Mungu haongeki!

5. MWISHO KABISA

Huwezi kumruka mtu uliyemuumiza na kukurupuka kukimbilia kanisani kwa mchungaji akuwekee mikono kichwani kukuombea msamaha kwa Mungu huo ni upotofu, mambo hayaendi hivyo!. Toba ya kweli ni kuanza kupatana na uliyemkosea na sio huu upumbavu wa kwenda kutubu kanisani na kumhonga mchungaji sadaka huku uliowaumiza wakiendelea kuumia.
 
Hapo kwenye kuyamaliza,, kumbuka siyo kila mtu atakubali kuyamaliza na wewe kwa amani!!!

Tuchukulie wewe ni jambazi, umekuja kupora mali kwangu then ukaiumiza na familia yangu,, then end of the day baada ya kukusakua sana nikakukosa uje ujilete unahitaji mapatano na mimi ety kwa sababu umeamua kuokoka!!!!

NAKUHAKIKISHIA NITAKUTANGULIZA KWA MUUMBA WAKO KABLA YASIKU ZAKO 😒
 
Ni mwepesi wa ksamehe ukianza kuomba msamaha kwanza kwa uliowakosea kisha mkiweka mambo yenu sawa ndio uende kwake, huwezi mdhurumu mtu alafu uende kwa Mungu mwenye haki akusamehe , NEVER !!!! Huyo uliemdhulumu nae anamuomba Mungu
Mungu angekua katili kama unavyomuelezea hapo, dunia ingekuwa chungu sana kwa wakosefu. Ndo maana tunaambiwa M/Mungu ni mwingi wa Neema na Rehema. Pia M/Mungu ni baba wa wote.
 
Nautangaza huu uzi kuwa uzi bora kwa mwaka 2024. Suala la kusema UMEOKOKA huku unatumbua pesa za dhuluma na kutoa sadaka lukuki ni ushenzi mtupu. Mtoa mada UBARIKIWE SANA
AMEN mkuu, Mungu hawezi kuhongeka na visadaka, yeye anamiliki kila kitu ulimwengu mzima.
 
Hapo kwenye kuyamaliza,, kumbuka siyo kila mtu atakubali kuyamaliza na wewe kwa amani!...
Kama ulikuwa jambazi ili kusamehewa inabidi uwe tayari kupokea maumivu kuzidi uliyosababishia wengine. hakuna mbadala, ila na wewe kumbuka utakuwa umetenda dhambi ya kuua mtu anaetaka kumrudia Mungu wake
 
Na yule aliyedhulum na kuiba Kisha akamrudia mungu wake baada ya hivi vyote kuisha na afanyaje?

Je akihofia akienda kujikumbusha na kuomba msamaha kwa aliowatendea mabaya kisasi kibaya kitamkuta afanyaje?

Ushauri wangu ni kwamba yyt mwenye kutubu dhambi zake aanze kwanza kuongea na mungu wake na atubie kwake na kuahidi hakuna alichowahi kukifanya isipokuwa anakiaacha.

Baada ya hapo aombe pia ni namna Gani anaweza kuponyesha majeraha kwa wale aliowaumiza kama inawezekana.

Yaan mungu ndo amuonyeshe namna Gani sahh anaweza kuomba msamaha kwa wale aliowakosea.

Ila chakwanza iwe Toba na kubadilika kwanza mengine yafuate, na ukiwa na Toba yakweli mungu atakuonyesha njia sahh yakuomba msamaha wale uliowakosea,

Pia usisahau wakat wa sala zako kuwaombea na wale uliowakosea mungu awarudishie haki zao na kuwaponya vidonda vyao ulivyovisababisha.
 
Ndio
Mungu angekua katili kama unavyomuelezea hapo, dunia ingekuwa chungu sana kwa wakosefu. Ndo maana tunaambiwa M/Mungu ni mwingi wa Neema na Rehema. Pia M/Mungu ni baba wa wote.
Maana kuna kale kamsemo

"Mungu sio Athumani" Hakika Mungu ni wa Rehema na Neema
 
Utasikia

fulani alikuwa jambazi hapo zamani kwa sasa kaokoka
...
Sasa kama HAO uliowakosea hawapo labla wamekufa au uliwauwa mwenyewe inakuwaje? Hutasamehewa milele hakika?

Utasemehewa kabisa kwakuwa kila mtu ametenda zambi na kupungukiwa na ukukufu wa mungu so hata hao uliowakosea na wanazambi zao so mungu ameweka mlango wa kutokea ni toba na kubadila I mean kuacha zambi unazofanya
 
Utasikia

fulani alikuwa jambazi hapo zamani kwa sasa kaokoka
Fulani alikuwa tapeli sugu hapo zamani kaamua kuokoka
Fulani alivunja ndoa za wengi hapo zamani kaamua kuokoka

NONSENSE, UJINGA!!

Mnakosea sana, Mnjidanganya, Mambo hayendi hivyo !!

Ulikuwa jambazi umeibia watu, wameshindwa kuendelea kwajili yako, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliowaibia

Ulikuwa mzinzi, umekuwa chanzo cha ndoa za watu kuvunjika, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa mme / mke uliemvunjia ndoa

Ulikuwa muuaji, umeua baba, familia zinateseka, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliewaulia baba

Ulikuwa dhulumati, umedhulumu watu, wanaishi maish ya dhiki, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliowadhulumu


Baada ya Daudi kushika madaraka nchi ikawa ina majanga, alipomuuliza Mungu nini chanzo, aliambiwa utawala uliopita wa Sauli uliua wana watu wa Gibeon hivyo waende kwao wayamalize,baada ya hapoataitakasa nchi, walipoenda huko wa Gibeon waliwambia wao hawataki dhahabu wala Silver, wanataka kulipiza kisasi, wawape wana wa Sauli wa kiume saba wawaue na walipofanya hivyo nchi ilitakaswa.

Mfano mwingine Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake kwamba kabla ya kutoa sadaka kaweke kwanza mambo sawa na uliowakosea, pia alishauri patana na mshitaki wako kwanza kabla hamjafika kwa hakimu

Mfano mwingine wa zakayo alikumbuka dhambi zake na akasema atawarejeshea mara kumi aliowadhulumu, bda ya hapo ndipo aliweza kupokea wokovu

Ni hiv, Mungu sio dhalimu,wewe unaweza kukuta umenitendea mabaya halafu unaenda kanisani kuokoka lakin unasahau mimi kila asubuh naamka na majereaha uliyoniachia aidha umeniibia duka nimefirisika, umeua watu wangu wa karibu naumia, umeniibia mke ndoa ilivunjika, umenidhulumu kiwanja sina nyumba, n.k.

Mungu hawezi kusahau uovu ulionifanyia kisa eti umebadilika, unaenda sana kanisani, unatoa sadaka (zikiwemo pesa ulizonidhulumu ), n..k NEVER !!!! Na kuhakikishia Mungu ni wa haki hata sikia sala yako ya kuokoka kama hutotubu maovu yako kwa uliowaumiza, Mungu haongeki !!!


Mwenyezi Mungu anachukizwa mno na dhambi
Kumbuka tulisha toka kwenye agano la jino Kwa jino
 
Back
Top Bottom