Uhusiano kati ya Umasikini, Utajiri, Uvivu na Werevu

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,565
19,615
Kuna baadhi yetu tumekuwa tukihusisha watu masikini kwamba ni wavivu, huenda hii ilikuwa kweli zama za kale za kuhitaji nguvu na jitahada za kulima ili upate mkate wako wa kila siku (sababu hata uwindaji huenda ulihitaji ujuzi zaidi kuliko uchapakazi); Pia huenda kipindi hicho mtu alikuwa na watoto wengi sana na kuwafanya vijakazi wake au hata watumwa wa kumfanyia kazi (Tujiulize hapo mvivu alikuwa nani)?

Na Mfalme Je, alikuwa mwerevu, mvivu au utajiri wake ulitokana na faida ya kuzaliwa na wazazi fulani? Je angezaliwa na wazazi masikini asingekuwa mchapakazi au huenda angefanikiwa zaidi kwa kufanya mapinduzi, au angekuwa mbishi na ubishi wake ungepelekea maisha yake kuwa mafupi?

Unaweza kusema kwamba masikini wengi huenda ni wavivu wa kufikiri (tukichukulia watumwa, wengi waliofikiri huenda fikra zao ndio zilikuwa mwisho wa maisha yao); na hii leo hawa chawa wanaokula kwa kukosa principles unaweza kuwaweka katika kundi gani? Na matapeli je?

Je ni kweli leo uchapakazi unalipa? Je ni kweli matajiri wanafanya kazi kuliko masikini au wanacheza na system iliyopo (ni werevu wa kupambana na system) au wanadiriki kupitia njia za mikato ili kupata utajiri wao?

Je mimi nikiwa mwerevu/mjanja na sioni faida ya (inefficiency) kwa kutumia jembe la mkono, au kulima mwenyewe na kuwatafuta watu wanilimie ili mwisho wa siku nipate kingi ni mvivu? Sababu huenda wanaolima wanafanya kazi kuliko mimi lakini sidhani kama ni vema kuwaita hao ni wavivu (wavivu wa fikra maybe, lakini huenda wamekosa mtaji - au wamekwama kwenye poverty cycle)

Je wale ambao wapo kwenye Poverty Cycle sababu hawana ajira yenye ujira (ingawa wamepewa ujuzi), hawana kasehemu ka kulima na wakilima hakuna soko; wakiomba tenda hawapewi sababu hawana connection - ni vipi watatoka kwenye umasikini na je ni vema kuwaita hawa wavivu; huenda wamekata tamaa na sio vipofu kuona kwamba chochote wanachofanya ni Rat Race.

Ofcource kuna wazembe na Wavivu lakini sio masikini wote ni wavivu (wengi ni wachapakazi) na sio Matajiri wote ni wachapakazi..., wengi hata hawahitaji kuchapa kazi. (the system works for them)

Tujikumbushe alivyosema Confucius; In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.
 
Kuna baadhi yetu tumekuwa tukihusisha watu masikini kwamba ni wavivu, huenda hii ilikuwa kweli zama za kale za kuhitaji nguvu na jitahada za kulima ili upate mkate wako wa kila siku (sababu hata uwindaji huenda ulihitaji ujuzi zaidi kuliko uchapakazi); Pia huenda kipindi hicho mtu alikuwa na watoto wengi sana na kuwafanya vijakazi wake au hata watumwa wa kumfanyia kazi (Tujiulize hapo mvivu alikuwa nani)?

Na Mfalme Je, alikuwa mwerevu, mvivu au utajiri wake ulitokana na faida ya kuzaliwa na wazazi fulani? Je angezaliwa na wazazi masikini asingekuwa mchapakazi au huenda angefanikiwa zaidi kwa kufanya mapinduzi, au angekuwa mbishi na ubishi wake ungepelea maisha yake kuwa mafupi?

Unaweza kusema kwamba masikini wengi huenda ni wavivu wa kufikiri (tukichukulia watumwa, wengi waliofikiri huenda fikra zao ndio zilikuwa mwisho wa maisha yao); na hii leo hawa chawa wanaokula kwa kukosa principles unaweza kuwaweka katika kundi gani? Na matapeli je?

Je ni kweli leo uchapakazi unalipa? Je ni kweli matajiri wanafanya kazi kuliko masikini au wanacheza na system iliyopo (ni werevu wa kupambana na system) au wanadiriki kupitia njia za mikato ili kupata utajiri wao?

Je mimi nikiwa mwerevu/mjanja na sioni faida ya (inefficiency) kwa kutumia jembe la mkono, au kulima mwenyewe na kuwatafuta watu wanilimie ili mwisho wa siku nipate kingi ni mvivu? Sababu huenda wanaolima wanafanya kazi kuliko mimi lakini sidhani kama ni vema kuwaita hao ni wavivu (wavivu wa fikra maybe, lakini huenda wamekosa mtaji - au wamekwama kwenye poverty cycle)

Je wale ambao wapo kwenye Poverty Cycle sababu hawana ajira yenye ujira (ingawa wamepewa ujuzi), hawana kasehemu ka kulima na wakilima hakuna soko; wakiomba tenda hawapewi sababu hawana connection - ni vipi watatoka kwenye umasikini na je ni vema kuwaita hawa wavivu; huenda wamekata tamaa na sio vipofu kuona kwamba chochote wanachofanya ni Rat Race.

Ofcource kuna wazembe na Wavivu lakini sio masikini wote ni wavivu (wengi ni wachapakazi) na sio Matajiri wote ni wachapakazi..., wengi hata hawahitaji kuchapa kazi. (the system works for them)

Tujikumbushe alivyosema Confucius; In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.
Wavivu ndio matajiri maana wanatafuta njia rahisi kufanyikisha mambo magumu,ila wazembe ndio wanaangukia kwenye umasikini.
 
Wavivu ndio matajiri maana wanatafuta njia rahisi kufanyikisha mambo magumu,
Mtu kama Rockefeller au Carnegie unaweza ukasema kwamba ni mvivu / wavivu;

Mfano Bongo mtu mwenye magari yake barabarani ambapo inabidi amwage rushwa hapa na pale, ameweka rehani nyumba zake na kila gari likiondoka usiku hapati usingizi kwa kuhofia huenda likapata ajali ni mvivu..., Huyu huenda maisha yake ni stress tosha na yeye ndio wa mwisho kujilipa mshahara if at all anajilipa huenda hata asi-break even

Nadhani tunakosea kuweka self made, honest wealthy people na walamba asali wanyonyaji na makabaila kwenye kundi moja..., wale wanaocheza na system na kukata njia za mikato (hawa ndio wana-give matajiri a bad name)
ila wazembe ndio wanaangukia kwenye umasikini.
Unajua kwamba huenda hizo patents zote kubwa kubwa na Big ideas huenda aliyekuja nazo sio yule aliye-cash in..., Yaani hata tukiangalia Facebook, Google n.k. huenda kuna mtu ali-toil katumia pesa kuweka idea yake kwenye mainstream mwisho wa siku competition ika-msqueeze out na aka-run bunkrupt huyu ni mzembe ?

Ukiangalia kwa jicho hilo utagundua its not black or white. and Hard Work don't normally pays, and to make it more than one thing needs to click, Inawezekana Idea yako imekuja before its time, au sio necessarily kwa wakati huo..., kwahio atakuja baadae mtu na kucopy na kupaste na kuondoka na matunda ya brainchild yako. (Though desire and Not Giving up helps)

Vilevile Definition ya Utajiri ni ipi sababu definition ya wengi ipo distorted..., Unaoweza kudhani watu fulani ni matajiri huenda sio matajiri (Mfumo wa Debt umefanya maisha kuwa Desi)

Extract from Trump Story
One day in 1990, as Donald Trump tells it, he and model Marla Maples were strolling along New York's Fifth Avenue when they passed a beggar.

"You see that man? Right now he's worth $900 million more than me. ... Right now I'm worth minus $900 million," Trump told Maples.

After a decade of profligate borrowing, Trump lacked the cash to make his loan payments. Although he owned hotels, skyscrapers, casinos and an airline, his debts exceeded the value of his properties by hundreds of millions of dollars.
 
BILL GATE once said" I will always choose a lazy person to do a very difficult job because he will find an easy way to do it." Asilimia 90 matajiri ni wavivu wanafanya vitu vigumu kuwa rahisi Kwa kufikiri muda mrefu kuliko kuifanya muda mrefu.Kugundua kitu na idea akachukua mwingine hapo ndipo tajiri na masikini wanatofautiana .
 
Hivi hizi nukuu ni lazima sana kuchukua za Wazungu, hivi hakuna nukuu nzuri zilizosemwa na Viongozi wetu wa Africa zinazoakisi dhima za maongezi yetu?
Nitafurahi kizazi kikichukua nukuu za Viongozi wetu wa Africa waliotukuka kama viambatanisho kwenye mada zetu.
Itapendeze kukutana na maneno kama ; Mangungo wa Msovero alipata kusema...., Au Kinjekitile Ngwale aliwahi kusema....., Au hata Omukama Rumanyika aliwahi kunukuliwa akisema.....
 
BILL GATE once said" I will always choose a lazy person to do a very difficult job because he will find an easy way to do it."
Necessity is the mother of all invention.., hata usipogundua wewe mwingine atagundua jambo unalosahau ni kwamba mgunduzi sio necessarily ndiye anayenuika.., Aliyegundua Simu sio kwamba Ni Graham Bell wengine walishagundua lakini ndio hivyo..., Tesla alikufa akiwa bankrupt; Farraday angekuwa bepari huenda leo Tanesco na Kampuni zote za umeme zingekuwa zinamlipa commissions yeye au watu wake...

By the way naweza kusema huyo unayemsema wewe sio mvivu wa akili sababu kutokuwa efficient huo ni upuuzi and has got nothing to do with being a hard worker... (busy doing nothing)
Asilimia 90 matajiri ni wavivu wanafanya vitu vigumu kuwa rahisi Kwa kufikiri muda mrefu kuliko kuifanya muda mrefu.
Kufikiri sio uvivu tena huenda ni uchapakazi zaidi sababu akili inafanya kazi 24/7.... Alisema Abraham Lincoln - “Give me six hours to chop down a tree and I will spend the first four sharpening the axe.”:
Huo sio uvivu ni efficiency and being smart..., tofauti na kuwatumikisha watu (watumwa) sababu eti wewe ni of Kings Blood; Au kula Kodi za Watu (Kulamba Asali) kwa mgongo wa kuwatengenezea maisha walipa Kodi

Kugundua kitu na idea akachukua mwingine hapo ndipo tajiri na masikini wanatofautiana .
Katika kila watu 100 wenye idea moja ni mmoja tu ndio ata-come out on top..., kwahio wengine kushindwa sio uzembe wala kukosa akili ni Happenstances au huenda connection zao na uwezo wao wa kwenye udhia kupenyeza rupia ni mdogo; Mostly its the Powerful who wins (and power does not necessarily mean money; A priest without money or a soldier without a dime can make Kings Kneel Down)...

“Power resides where men believe it resides. It's a trick. A shadow on the wall. And a very small man can cast a very large shadow.” - Varys - GOT
 
Hivi hizi nukuu ni lazima sana kuchukua za Wazungu, hivi hakuna nukuu nzuri zilizosemwa na Viongozi wetu wa Africa zinazoakisi dhima za maongezi yetu?
Nitafurahi kizazi kikichukua nukuu za Viongozi wetu wa Africa waliotukuka kama viambatanisho kwenye mada zetu.
Itapendeze kukutana na maneno kama ; Mangungo wa Msovero alipata kusema...., Au Kinjekitile Ngwale aliwahi kusema....., Au hata Omukama Rumanyika aliwahi kunukuliwa akisema.....
Unaweza kuanza wewe leo, sasa hivi kwenye haya maandiko yako...... after all 'Jungu Kuu halikosi Ukoko' ; Unaweza kusema 'Mwacha Asili ni Mtumwa' lakini takujibu Dunia ni kijiji na Chimbuko la Homo Sapiens wote ni Olduvai Gorge..... vilevile 'Penye wengi pana Mengi'; kwahio sio busara kuwabana watu wafanye hiki au kile (kutakuwa hakuna varieties ya Mada) cha maana wewe fanya kile ambacho ungetaka kifanyike...

By the way sisi kama Taifa tumejikita kwenye Uchawa, Tunaongelea Watu na Events badala ya Ideas..., unadhani tunaweza tukatoa quotable qoutes ngapi...., Ofcourse binafsi ninawa-qoute kina Shida, Okwonkwo, Mine Boy n.k. ila ukiona qoutes zako hazipo mainstream sio sababu ya wanao-qoute bali ni popularity ya unachokisema By the Way nukuu nyingi mpaka zifike huku fahamu kwamba zimeshakuwa za dunia nzima na sio sehemu moja.... Na nyingi ya hizo zilitokea age of enlightenment - Ingawa methali na misemo ya ki-africa ni mingi na tunaitumia kila siku
 
Hivi hizi nukuu ni lazima sana kuchukua za Wazungu, hivi hakuna nukuu nzuri zilizosemwa na Viongozi wetu wa Africa zinazoakisi dhima za maongezi yetu?
Nitafurahi kizazi kikichukua nukuu za Viongozi wetu wa Africa waliotukuka kama viambatanisho kwenye mada zetu.
Itapendeze kukutana na maneno kama ; Mangungo wa Msovero alipata kusema...., Au Kinjekitile Ngwale aliwahi kusema....., Au hata Omukama Rumanyika aliwahi kunukuliwa akisema.....
Ahahah.
 
Kuna mdau nimeona anahusisha Utajiri / Umasikini na furaha....

Nikajiuliza kwenye hii equation furaha inakuja vipi au inakosekana vipi ?

Nadhani kabla ya yote lazima kwanza tupate tafsiri ya neno utajiri, na sio mbaya tuki-assume kwamba mafanikio ni sawa na furaha (yaani ukifanikiwa utakuwa na furaha na usipofanikiwa kuna kitu kitakuwa kinakosekana hence kukosa furaha)

Formula:
Utajiri ni iwapo Mapato = Matumizi + Savings
(Yaani iwapo mapato unayopata yatatosheleza Matumizi yako na bado ukabakiwa na Chenji basi wewe sio Masikini) - Unaweza ukawa na kipato mara 10 zaidi ya mwenzako lakini kama matumizi yako ni mara 20 ya mapato yako wewe ni masikini.

Mafanikio = ni kumaliza / kukamilisha chochote ambacho umekianza au unataka kukifanikisha kwahio kama wewe target yako ni kuvuna gunia ishirini ukipata kumi hauwezi kuwa na furaha kama mtu mwenye target ya sufuria moja na akapata debe moja....

Hence furaha inatokana na (satisfaction; fulfillment; - kukidhi haja zako / Kuridhika) - kwa ufupi expectation ndio zinapelekea dissapointments au lack of....

'Blessed is he who expects nothing, for he shall never be disappointed.'

Msemo huu ninauchukulia kwamba ukijua kila kitu kinaweza kikawa na matokeo mawili (hasi na chanya) hata likitokea ambalo hulipendelei halitakuathiri kama yule ambaye anategemea asilimia 100; (Hii iwe kwenye Mapenzi; Kipato; au Chochote unachofanya) ukiwa hivyo wewe na furaha itakuwa chanda na pete (Nothing to do na umasikini au utajiri) - By the way naongelea umasikini (sio ufukara yaani atleast unapata chakula - sababu huwezi kuwa na furaha au kuwaza mengine ukiwa na tumbo tupu) - Yaani haujafanikiwa hata kutia mkono kinywani
 
Hivi hizi nukuu ni lazima sana kuchukua za Wazungu, hivi hakuna nukuu nzuri zilizosemwa na Viongozi wetu wa Africa zinazoakisi dhima za maongezi yetu?
Nitafurahi kizazi kikichukua nukuu za Viongozi wetu wa Africa waliotukuka kama viambatanisho kwenye mada zetu.
Itapendeze kukutana na maneno kama ; Mangungo wa Msovero alipata kusema...., Au Kinjekitile Ngwale aliwahi kusema....., Au hata Omukama Rumanyika aliwahi kunukuliwa akisema.....
Linyamkong'onho we Likang'ambwa wa huko idodomhya alipata kusema Welikome some time na mzee Kikwanyulo Diukizula wa Uziguani huko Kwamsisi aliwahi sema Akumsungila mnyawe kwe digwaha na adye Chitapwa
 
Aisee! Ukisikia nje ya boksi ndiyo hii sasa.

Hata mm huwa naona Mwijaku ana kipato kuliko mm. Sasa huwa najiuliza: hivi kweli Mwijaku (chawa) anachapa kazi kuliko mm?
 
Hivi hizi nukuu ni lazima sana kuchukua za Wazungu, hivi hakuna nukuu nzuri zilizosemwa na Viongozi wetu wa Africa zinazoakisi dhima za maongezi yetu?
Nitafurahi kizazi kikichukua nukuu za Viongozi wetu wa Africa waliotukuka kama viambatanisho kwenye mada zetu.
Itapendeze kukutana na maneno kama ; Mangungo wa Msovero alipata kusema...., Au Kinjekitile Ngwale aliwahi kusema....., Au hata Omukama Rumanyika aliwahi kunukuliwa akisema.....
Hapohapo unatakiwa kujua Viongozi wetu waliwahi na ndio wanaongoza kwa Ufisadi na Wizi na kama hawafit kwenye hiyo category basi bila shaka ni Masikini. Sasa wewe jiulize hizo quotes za kikwetu zinazouhusu mafanikio na hustles zitatoka wapi.
 
Back
Top Bottom