DMmasi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 437
- 670
Naam kilicho bora na imara hujengwa katika misingi iliyo bora na imara
Tanzania tunayoitaka iko mikononi kwa wazee ambapo yapaswa kukabidhiwa kwa vijana na watoto, maarifa na ujuzi ni vitu muhimu vya kutuvusha kuifikia Tanzania tunayoitaka.
Elimu itolewayo mashuleni izidi kuboreshwa isiishie tuu kwenye kutafuta ufaulu kwa kukariri bali iwajenge watoto katika hali ya kuwa jasiri, kujiamini,kutii, kuheshimu na upendo.
Yapo ya muhimu ya kuyafundisha mashuleni watoto serikali iwe na utaratibu ambao mtoto atakaye maliza elimu ya msingi ajue walau sheria mama ya nchi inasomekaje, huduma za dharura zinatolewaje.
Nasiyo kupima uwezo kwa maswali ya kuowanisha (safu A,mwaka 1807 unaenda kuangalia safu B, ninini kilitokea miaka iyo) elimu ya kukariri.
Serikali itengeneze mifumo wezeshi na mazingira yatakayo wafanya wanafunzi wafurahi kuwepo shuleni kwanzia rasilimali watu,fedha na viwezeshi vingine shule isiwe ni madarasa, vyoo,maabara na madawati bali ibebe na jukumu la kumfundisha wanafunzi uwajibikaji walai kuwepo na mashamba darasa.
Serikali inaundwa na watu na watu ndiyo sisi turudi kwa upande wa jamii
wanasema kijiji bila wazee ni mateso
Naamu nitoe rahi kwa wazazi hasa wazazi wa siku hizi waleeni watoto kama mlivyolelewa ninyi tuache kuyatafakari maisha tuliyolelewa kama maisha magumu na mateso na tuifute ile kauli ya "sitaki mtoto wangu ateseke".
Wazee wanasema "Nyakati ngumu zinamtengeneza mtu imara na mtu imara anazitengeneza nyakati rahisi, alafu nyakati rahisi zinamtengeneza mtu dhaifu na mtu dhaifu anatengeneza nyakati ngumu"
wazazi waleeni watoto kwa kuwatoa kwenye icho kiota kama ninyi mmekwisha fanikiwa basi watengenezeni kwenye mfumo wa wao kufanikiwa mara mbili yenu.
Wafungulieni watoto wakutane na watoto wengine siyo wasinde na televisheni na kuingia mitandaoni wanakitana na vitu vizito vinavyotulemea hadi sisi
Nidhamu, heshima, adabu, usafi na kujituma na kujitumikia iwe dhima ya malezi kwa watoto wetu. Jamii hii tunayoiyogopa yenye madhila na maasi mengi ndiyo jamii tunayozidi kuitengeneza
Nimalize kwa kusema jamii iliyo bora Ina Mila na tamaduni zetu. Naamu tumetengenezewa fikra ya kwamba elimu za jando na unyago ni Mila Potofu tumekumbatia "my name is doctor living stone" matokeo yake ndo haya ya familia zisizokuwa na msingi hata wanyama na ndege porini wanazaa nakulea watoto wao pamoja.
Tuzikumbuke na kuzienzi Mila na tamaduni zetu wazee walifunzwa kuheshimu na jamii iliweza kulea mtoto,
kwa nyakati hizi tunaogopa jamii kumlea mtoto sababu siyo sehemu salama watoto wanafichwa ndani hatutaki kurekebisha jamii ila tumekimbilia ndani vipi kesho shida ikiwa ni familia tutakimbilia wapi.
Wapeni muda watoto, waleeni katika misingi ya familia (baba na mama)
niliwahi kumsikia Dr Chris Mauki akisema maleza ya mama ni yakubembeleza na ya baba ni yakuelekeza na watoto wanayahitaji yote.
Tusiwalee watoto kwa kuwakandamiza bali tuwemarafika wakuzungumza wawe huru siyo kujikunyata na kushindwa kuzungumza.
ASANTENI
mwana jamii
Mmasi Dismas