SoC04 Afya bora kwa Watanzania na vizazi vijavyo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Apr 20, 2024
26
11
Napendekeza yafuatayo katika sekta ya afya ili kuleta manufaa kwa Watanzania wote miaka ijayo.

1. Kuhakikisha vituo vyote vya afya vinakuwa na watoa huduma toshelevu kwa ngazi zote ili wahitaji wawe wanapata huduma ndani ya wakati.

2. Kujengwa kwa vituo vya afya vinavyokidhi mahitaji ya jamii husika kuepusha foleni zisizo na msingi wakati wa huduma.

3. Serikali iongeze nguvu ya usimamizi katika mifumo yote na sheria zinazohusu sekta ya afya ili kuweka mazingira mazuri ya utoaji na upokeaji huduma mahospitarini.

4. Kuwepo na semina mbalimbali zitakazowafanya wanajamii kupata elimu juu ya suala zima la afya kwa kuzingatia makundi yao(wajawazito, watoto, vijana, watu wazima na wazee).

5. Serikali Kushirikiana na wadau mbalimbali ktoka sekta nyinginezo ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na uwezo wakutoa changamoto zao kuhusiana na suala la afya katika eneo husika.

6. Watoa huduma za afya katika ngazi zote wasimamiwe ipasavyo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao yakikazi kwa kufuata sheria na viapo vyote vya afya.

7. Kuboresha zaidi miundombinu kama maji, umeme, majengo, na mashine za kisasa za vipimo na matibabu.

8. Serikali kuajiri wafanyakazi wenye uwezo mkubwa katika vitengo mbalimbali vya afya ili kuhakikisha wahitaji wanapata msaada stahiki nasio kubabaishwa kama inavyotokea kwa baadhi ya vituo vy afya.

9. Kuongeza vyuo bora vya afya na wataalamu wabobezi ili badala ya wanafunzi kwenda nje ya nchi kutafta elimu bora zaidi basi wapate mafunzo hapa hapa nchini maana sidhani kama inashindikana sema ni uamzi tu.

10. Mwisho ni kuondoa changamoto ya ukosefu wa dawa katika vituo vya afya. Sio mgonjwa anapimwa halafu dawa anaambiwa akachukue pharmacy.

11. Wakati wa huduma watu ambao wapewe kipaumbele cha kuhudumiwa mapema basi wawe wale wenye hari mbaya(waliozidiwa) kiafya ili kunusuru maisha yao na ndipo makundi mengine yafuate.

Screenshot_20240503-181029.png
 
4. Kuwepo na semina mbalimbali zitakazowafanya wanajamii kupata elimu juu ya suala zima la afya kwa kuzingatia makundi yao(wajawazito, watoto, vijana, watu wazima na wazee).
Profesa Janabi anajitahidi kwa hili, sema wabongo baadhi sasa mmmmh!

Na hata kama hujalizungumzia, naona umetia picha inayohusisha bima. Nikuulize mleta mada. Unadhani ni nini kitawasukuma wananzengo kumtilia maanani Profesa ikiwa hata tu wakiugua ajali(kanuni za usalama barabarani), figo na moyo wataenda kutibiwa hospitali bure?

Na wadau wengine, je mnafikiri, cost sharing VS Bima kwa wote ipi ni bora?????
 
Back
Top Bottom