Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Mkuu ni vizuri umeleta hi mada, watu wengi hawajui government bonds zinafanya je faida au UTT utawasikia weka pesa UTT utapata faida kubwa hawajui masikini. Biashara ya hisa bonds fixed acc nk haziwezi kukulipa katika nchi kama Tanzania, yenye high lnflation rate, unstable exchange rate, low business transaction rate, unstable bank intrest nk ........wanao faidi hiyo finicial market ni wafanya biashara wenye idol finance au wapiga dili kubwa ndo njia peke ya kuficha pesa zao ila wewe menye kupata pension ya 100m uiweke benki upata 8% annually nu kupoteza pesa na mda
Ni ukweli usiopingika kuwa ukitaka kuifaidi hiyo mifuko lazima uwe na si chini ya million 500 kwa miaka 25 ili kila mwezi upate million 5. Million 5 zinaweza kukulisha ila siyo kukufanya uishi kipapaa. Chini ya hapo, hutaifaidi hiyo mifuko.
 
Where are the Customers' Yachts ?

"Once in the dear dead days beyond recall, an out-of-town visitor was being shown the wonders of the New York financial district. When the party arrived at the Battery, one of his guides indicated some handsome ships riding at anchor. He said, 'Look, those are the bankers' and brokers' yachts.' 'Where are the customers' yachts?' asked the naïve visitor."
 
Mpk unaingiza 5M kwa uwekezaji tu hao wajukuu lazima sio njaa kali hapo
Matumizi ya wakati huo ni pamoja na magonjwa ya uzeeni yenye gharama, kurepair etc. Bora kupata 160K ukiwa kijana kuliko hiyo na matumizi kuwa makubwa ya uzeeni. Usisahau wakati huo hata watoto wazuri unakula kwa macho na michepuko haikubali kuja kwa Bus bali ndege.
 
Government bond ni biashara ya Wahindi, anaweza kuweka B 1 BOT kila mwezi akavuta mshahara wa million kadhaa na pesa inazaa.

Kapuku na biashara ya pesa hakuna kitu kama hicho.

Mambo ya Forex na bit coin sijui ndio cryptocurrency achana nayo kabisa.

Nimemsikia Bongo zozo mara nyingi akidanganya watu kwamba Siri ya yeye kuwa na pesa ya kusafiri duniani ni bit coin, si kweli msiingizwe mkenge huo, wazungu ni fallen Angels huwezi kuujuwa undani wao.

Kwenye ujasiriamali ukiwa na roho ngumu na ukakomaa pesa unaweza kuiona, na kingine Bongo visource vya income unatakiwa uwe navyo vingivingi tu bila kusahau kujenga lodge, hii ndio biashara ya uhakika, starehe ya mafukara NI ngono.
You are correct.
 
Mijadala yote ya aina hii huwa iko based kwenye ONE WRONG ASSUMPTION!

Watu wengi sana wanaofanya biashara hua wana assume kwamba kwavile wao wameweza kufanya biashara na kufanikiwa, basi MTU YOYOTE anaweza nae kufanya biashara na kufanikiwa! Mfano mleta mada anaona kwavile yeye ameweza kukuza 10m ikafika 40m, basi mtu yoyote yule mwenye 10m akifanya biashara nae atapata 40m, kitu ambacho SIO KWELI HATA KIDOGO..

JAMANI, BIASHARA NI KIPAJII... SIO KILA MTU ANAWEZAA..! TUACHENI TUSIOWEZA TUWEKEZE HUKO UTT, fixed deposits, nyumba za kupanga nk hata kama tunapata faida ndogo ni sawa, kuliko kuchoma mitaji yetu midogo kwenye biashara tusizoziweza.
 
kwani wenzetu mnaishi wapi?
5M monthly kweli usiishi kiboss?? Kila siku maximum 160k
Mtuu mwenye pesa idol mpaka 500m kweli unaona kwa nwenzi 5m ni pesa nyingi ya kumfanya aishi kudoni kweli, mbona watu tunamaisha magumu loh,......mtu kama huyu ana watoto wa 3 wana soma Feza ada ni 15 to 11m bill za maji na umeme kwa mwezi pamoja na house mantainance mbona hiyo pesa ndogo sanaa loh.
 
INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..

Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.

BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.

Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""

Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""

SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.

Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.

PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.

Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).

Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.

Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.

Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).

CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.

Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.

Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!

ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.

Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!

Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.

Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.

2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.

Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.

Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA
 
Hapa wataalam wangeweza kusema, bora ungeweka kwenye stock/shares mfano CRDB, kwa kuwa umoja na wenyewe wanaenda ku-invest kwenye shares! Ila mimi si mjuvi sana wa sector!
Muwe mnajisomea ili mfiche ujinga sometimes. Iko wazi kabisa,wewe binafsi unaweza kwenda sokoni moja kwa moja bila kupitia UTT. Lakini faida utakayo pata ni ndogo ukilinganisha na yule aliye wekeza kupitia UTT.
 
unauhakika kozi ulisomea uchumi mkuu? compounding interest unaielewa vyema inavyo piga kaz there is no wonder ulipigwa forex inaonekana unapenda utajir wa chap kitu ambacho kimewaponza kina meek mill
Kwa mfano wangu huohuo
Kuna utofauti Kati ya Compound interest ya Mkurugenzi/boss wako na mdada wenu wa kazi.

Jikite kwenye mada, hebu tengeneza schedule ya house girl kuwa tajiri kwa hizo compound interest akiwa na miaka 25.

Usisahau LIFE SPAN yetu.

#YNWA
 
Sasa kama umesoma up to masters level I assume unayafaham haya yote, hukutakiwa hata kuanzisha hii debate au kudiscourage wanaowekeza huko hata kwa udogo wa investments zao…Kwenye issue za personal finance and investments , there is no right or wrong, decisions zinategemea na malengo ya mtu binafsi, kwa mfano mm nina 2M zangu huwezi ukaniambia nisiweke Utt niweke kwenye bussiness huwezi jua , malengo yangu ni nn au strategies zangu ni zipi…Kusema Money Market yetu bado sanaaa ni kweli ndio tunaendelea kukua huwezi kulinganisha DSE na NYSE ,LSE au HKSE…But kuna hatua tumepiga tofauti na 5-10 yrs back, kuna watu wamemake Millions through Money Markets za Tanzania, huwezi kuundermine the progress!!….
Wanao make hizo millions unadhani ni hawa bodaboda na ma-house girl.

Hebu tafuta taarifa ya Rostam (Mirambo holding) alivyouza hisa zake za Vodacom na kuzinunua tena

Halafu jilinganishe na wewe uniambie UTAFIKA LINI na hivyo vipande vya buku 10

#YNWA
 
Back
Top Bottom