SI KWELI Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inapokea Maombi ya Wafanyakazi wa Kuboresha Daftari la Wapiga Kura Mtandaoni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Habari,

Nimeona tangazo Mtandaoni linadaiwa kutolewa na NEC, kwamba wametangaza nafasi za kazi ya uandishi wa daftari la kudumu la wapiga kura Mwaka 2024. Kinachonipa wasiwasi naona kama tovuti hii si rasmi.

Ukweli wake upoje?

IMG_20240426_155251_721.jpg
 
Tunachokijua
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ni chombo kilichoanzishwa Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa chaguzi kwa mujibu wa sheria ili kulinda demokrasia kwa manufaa ya wananchi, vyama vya siasa na wagombea.

Pamoja na kazi hii, Dira yake ni kuhakikisha Uwepo wa mfumo wa uchaguzi unaoaminika na unaohakikisha chaguzi huru na za haki.

Madai ya tume kuanzisha maombi Mtandaoni
Aprili 15, 2024, Tume Huru ya Uchaguzi ilitoa tangazo kupitia halmashauri zote nchini la kukaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki kwenye vituo vya kuboresha daftari.

Baada ya kutolewa kwa tangazo hili, zimeibuka tovuti mbalimbali zinazotaka watu watume maombi ya kazi husika na mojawapo ya tovuti hizo ni hii iliyowekwa hapa na Mdau Heparin

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa tangazo hili linalosamba Mtandaoni kupitia tovuti likiwataka watu kutuma maombi kwa njia ya Mtandao halijatolewa na Tume Huru ya Uchaguzi.

JamiiCheck imebaini kuwa Tangazo hilo limetolewa na Taasisi inayojiita 'Tume ya Uchaguzi' na si 'Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi' kama inavyofahamika kwa sasa baada ya kufanyiwa Marekebisho.

Aidha, tovuti hiyo yenye kikoo cha blogspot si rasmi, wala haitumiwi na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambayo tovuti yake rasmi ni inec.go.tz.

Ishara nyingine inayoonesha kuwa tovuti hii si ya kuaminika ni uwepo wa ujumbe wa tahadhari unaotolewa wakati wa kutuma taarifa husika wakati wa kujaza maombi. Tazama hapa chini.

1000031332-jpg.2974603


Taarifa ya Kanusho
Aprili 25, 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa inayotoa tahadhari kwa watu kuhusu uwepo wa matangazo yasiyo rasmi ya nafasi za kazi za Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura.

"Tunapenda kusisitiza kwamba, barua zote za maombi ziwasilishwe kwa Maafisa Watendaji wa Kata zikiwa zimefungwa. Maafisa Watendaji wa Kata watazipokea na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika.

Mwombaji hatakiwi kutoa malipo yoyote"
ilisema sehemu ya maelezo rasmi ya barua ya tume.

Kwa kutambua uwepo wa aina hii ya utapeli kupitia matangazo ya kazi, Machi 4, 2024, JamiiCheck ilichapisha mada inayofafanua jinsi ya kutambua matangazo haya na jinsi ya kuepuka kutapeliwa.

Katika nyakati hizi zenye uhaba mkubwa wa ajira ni muhimu kuwa makini ili kujiepusha na matapeli wanaoweza kutumia mwanya huu kujipatia kipato.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom