True story: Mzazi ukiogopa kumlipia mtoto ajifunze kuogelea chini ya uangalizi jiandae kwa lolote mtoto akienda mtoni / beach kuogelea bila uangalizi

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,116
maji yana hatari lakini ni vema kuipunguza hatari hii kwa kujifuunza kuogelea, kuna watu wanakufa maji kwenye mafuriko kwa kushindwa kuogelea, meli zinpinduka ufukweni kuna abiria wanakufa maji kwa kushindwa kuogelea, watu wanaozama wanashindwa kuokolewa saabu anaeshuhudia hawezi kuogelea, n.k.

Kuna baadhi ya shule huwa zina swimming classes ama kuna shule maalum za kuogelea zinawajuza wazazi wapeleke watoto kujifunza kuogelea kwenye swimming pools chini ya uangalizi makini.

Nakumbuka shule flani miaka ya 2006 kulikuwa na swimming classes lakini kuna wazazi wengi walisita kwa hofu ya kuyaogopa maji na hata wao hawajui kuogelea.

miaka ilienda na kama mnavyojua watoto hasa wa kiume wakifikia miaka ya teenagers huwa wanapenda kutamanani kujaribu vitu na michezo mingi hatari.

basi ikatokea siku moja wanafunzi watatu wakapanga waende beach, moja wao alikuwa ambae wazazi wake walimkatalia kujifunza kuogelea ile shule, mbaya zaidi beach haina ulinzi wala uangalizi, nae nahisi kwa aibu hakuweza kusema hajui kuogelea labda ili asionekane mshamba kama mnavyojua mambo ya peer pressure kwa teenagers.

kufika huko beach huyo ambae ni mgeni akasogea mbali kidogo ni kama kulikuwa na korongo akaanza kuzama bila ya kuwa na sehemu ya kushika wala kujua kuyapiga maji,

wenzake walikuwa sio wazoefu hivyo hawakuwa na la kufanya, ili uweze kuokoa mtu anaezama inabidi uwe mzoefu maana mtu anaezama akipata pa kushika hakuachii hata ufanye nini, kama sio mzoefu mnaweza kuzama wote.

wakatafuta msaada lakini walishachelewa, mwenzao alikuwa tayari kanywa vikombe vya kutosha, rest in peace.
 
Umeandika kitu usichokijuwa, bahari anayeiweza ni diver peke yake.

Shauri wanaokwenda beach watumie maboya kuongelea tena kwenye maji madogo.
 
Umeandika kitu usichokijuwa, bahari anayeiweza ni diver peke yake.

Shauri wanaokwenda beach watumie maboya kuongelea tena kwenye maji madogo.
hata wanaojua kuendesha magari wanapata ajali !!

wapo wanaozama beach wakiwa wanajua kuogelea ila ni asilimia ndogo sana, ni 1 anaezama kati ya 100 pengine mawimbi, kanasa kwenye kitu, kapata kifafa akiwa anaogelea, n.k

lakini kwa wale wasiojua kuogelea wakifika vina virefu ni wengi sana karibu wote wanazama
 
Kuna baadhi ya shule huwa zina swimming classes ama kuna shule maalum za kuogelea zinawajuza wazazi wapeleke watoto kujifunza kuogelea kwenye swimming pools chini ya uangalizi makini.

Nakumbuka shule flani miaka ya 2006 kulikuwa na swimming classes lakini kuna wazazi wengi walisita kwa hofu ya kuyaogopa maji na hata wao hawajui kuogelea.

miaka ilienda na kama mnavyojua watoto hasa wa kiume wakifikia miaka ya teenagers huwa wanapenda kutamanani kujaribu vitu na michezo mingi hatari.

basi ikatokea siku moja wanafunzi watatu wakapanga waende beach, moja wao alikuwa ambae wazazi wake walimkatalia kujifunza kuogelea ile shule, mbaya zaidi beach haina ulinzi wala uangalizi, nae nahisi kwa aibu hakuweza kusema hajui kuogelea labda ili asionekane mshamba kama mnavyojua mambo ya peer pressure kwa teenagers.

kufika huko beach wale waliozoea kumbe nao hawajui vizuri kuogelea wapo sehemu zenye maji yanayowafikia kwenye usawa wa tumbo.

yule mwengine kwa ugeni akasogea mbali kidogo ni kama kulikuwa na korongo akaanza kuzama bila ya kuwa na sehemu ya kushika wala kujua kuyapiga maji,

ili uweze kuokoa mtu anaezama inabidi uwe mzoefu maana mtu anaezama akipata pa kushika hakuachii hata ufanye nini, kama sio mzoefu mnaweza kuzama wote.

wenzake walikuwa sio wazoefu hivyo hawakuwa na la kufanya, wakatafuta msaada lakini walishachelewa, mwenzao alikuwa tayari kanywa vikombe vya kutosha, rest in peace.
Kwani hilo linaumuhimu gani katika taifa........acheni malimbukeni ya vitu.
 
Back
Top Bottom