Abdul S Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 207
- 321
Anayedaiwa kulala na kula Serena kisha kutokomea aachiliwa huru
Habari wana jamvi, awali ya yote nimesikitishwa sana na habari tajwa hapo juu👆 kwani nimejiuliza, je kama menager wa hoteli kubwa kama serena na team yake wameshindwa kung'amua tofauti iliyopo kati ya kesi za jinai na madai, sasa itakuaje kwa raia wenzangu wakawaida kabisa🤔? Japo suala hili nimewahi kuligusia katika Thread: Uelewa wa masuala ya kisheria ni mdogo sana Tanzania.. Lakini limenisukuma kuandika tena uzi huu ili uwe faida kwa umma juu ya tofauti kati ya aina mbili izi za kesi.
ANGALIZO
Taarifa zilizotolewa hapa zinakusudiwa kwa madhumuni ya elimu pekee na siyo ushauri wa kisheria. Juhudi zimefanyika kuhakikisha usahihi, lakini yaliyomo hayapaswi kutegemewa kama mbadala wa ushauri wa kitaalamu wa kisheria. Hivyo, ushauri kutoka kwa mtaalamu wa sheria mwenye sifa unapendekezwa kwa mwongozo zaidi.
Taarifa zilizotolewa hapa zinakusudiwa kwa madhumuni ya elimu pekee na siyo ushauri wa kisheria. Juhudi zimefanyika kuhakikisha usahihi, lakini yaliyomo hayapaswi kutegemewa kama mbadala wa ushauri wa kitaalamu wa kisheria. Hivyo, ushauri kutoka kwa mtaalamu wa sheria mwenye sifa unapendekezwa kwa mwongozo zaidi.
Tukianza na Kesi za jinai, hizi ni zile zinazohusisha makosa ambayo yameainishwa kisheria kuwa ni kinyume na maslahi ya jamii au nchi kwa ujumla. Makosa haya yanaweza kuwa ni pamoja na wizi, mauaji, ubakaji, na mengineyo.
Matokeo ya kesi za jinai mara nyingi ni adhabu kama vile kifungo jela, faini, au vyote viwili kwa pamoja. Japo sio mara zote ila mara nyingi kesi hizi huendeshwa na serikali kupitia ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) ambapo mwendesha mashtaka wa serikali anasimama kama mlalamikaji dhidi ya mtuhumiwa.
Mambo ya muhimu kuyafahamu kuhusu kesi za jinai ni pamoja na;
- Asili na Madhumuni: Kesi za jinai zinahusu uvunjifu wa sheria za jinai, ambapo kitendo kinachodaiwa kufanywa ni kosa la jinai lililotajwa na sheria. Madhumuni ya kesi za jinai ni kulinda jamii dhidi ya tabia zinazovuruga amani na utulivu, na kutoa adhabu kwa wahalifu ili kuzuia makosa ya baadaye.
- Wahusika wakuu: Mara nyingi mhusika mkuu ni serikali, inayowakilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) au vyombo vingine vya serikali kama polisi. Serikali inasimamia kesi dhidi ya mshtakiwa (mtuhumiwa) na mtendewa kosa (victim) atakua shaidi tu.
- Mchakato wa Kesi: Kesi za jinai huanza na uchunguzi wa polisi, kukamatwa kwa mtuhumiwa, na mashtaka kupelekwa mahakamani. Mtuhumiwa anapopelekwa mahakamani, anashtakiwa kwa kosa maalum la jinai na kesi hufanyika kwa kuzingatia ushahidi uliokusanywa na upande wa mashtaka.
View: https://youtu.be/EG_-qZMvd-0?si=oEZbAPpZI0ruvIWT
4. Kiwango cha Ushahidi: kiwango cha ushahidi katika kesi za jinai ni juu zaidi, ambapo upande wa mashtaka lazima uthibitishe kosa "pasi kuacha shaka yoyote ya kawaida" (beyond reasonable doubt).
5. Adhabu: Adhabu katika kesi za jinai inaweza kuwa kifungo gerezani, faini, huduma za jamii, au adhabu nyingine zilizotajwa kisheria kama vile kunyongwa kwa makosa makubwa kama mauaji.
Kwa upande mwingine, kesi za madai ni zile zinazohusiana na migogoro baina ya watu binafsi au taasisi ambapo upande mmoja unadai haki kutoka kwa mwingine. Hii inaweza kujumuisha masuala kama vile migogoro ya ardhi, mikataba, fidia za ajali, na kadhalika. Lengo la kesi za madai ni kupata haki au fidia kwa yule aliyeathirika. Kesi hizi zinaendeshwa na mlalamikaji binafsi, na siyo serikali.
Kama ilivyo kwenye jinai, hata kwenye madai ni muhimu kutambua yafuatayo;
Kama ilivyo kwenye jinai, hata kwenye madai ni muhimu kutambua yafuatayo;
- Asili na Madhumuni: Kesi za madai zinahusu migogoro kati ya watu binafsi au vyombo vya kisheria kuhusu haki au wajibu wa kisheria. Madhumuni ni kutafuta haki na fidia kwa mtu aliyeathiriwa kutokana na kitendo cha mtu mwingine au chombo cha kisheria.
- Wahusika wakuu: Wahusika wakuu ni mtu binafsi au taasisi inayodai kuathiriwa (mdai) na mtu binafsi au taasisi nyingine (mdaiwa).
- Mchakato wa Kesi: Kesi za madai huanza kwa mdai kuwasilisha madai mahakamani dhidi ya mdaiwa. Mahakama husikiliza ushahidi kutoka pande zote mbili (mdai na mdaiwa) na kufanya uamuzi kulingana na ushahidi uliotolewa.
View: https://youtu.be/YHw9KWnFaPQ?si=UV-xbGER4waDJX3G
4
. Kiwango cha Ushahidi
: Kiwango vya ushahidi katika kesi za madai ni chini kuliko za jinai, ambapo mdai anatakiwa kuthibitisha madai yake "kwa mizani ya uwezekano" (balance of probabilities).
5.
Adhabu: Matokeo ya kesi za madai kwa kawaida ni fidia ya fedha kwa mdai, maagizo ya mahakama kama vile zuio (injunctions), au amri nyingine za kurejesha haki au kuzuia kitendo fulani.
Kwahiyo, tofauti kuu kati ya kesi za jinai na madai ni nani anayeendesha kesi na lengo la kesi. Katika kesi za jinai, serikali ndiyo inaendesha kesi na lengo ni kuadhibu kwa kifungo au faini, wakati katika kesi za madai, mlalamikaji binafsi ndiye anayeendesha kesi na lengo ni kupata fidia au haki.