Nani anatakiwa kusaini pleadings (nyaraka) za kwenda Mahakamani kwenye kesi ya madai?

Apr 26, 2022
64
100
Nyaraka za kufungulia na kujibu kesi Mahakamani (Pleadings) kama vile hati ya madai (plaint) na hati ya utetezi (WSD) zinatakiwa kusainiwa na mhusika (mdai au mdaiwa) pamoja na wakili wake (kama yupo) au mtu yeyote ambaye ameruhusiwa na mhusika.

Hata wakili peke yake anaweza kusaini kama tu ameruhusiwa na mteja wake.

Hii ni kwa mujibu wa kifungu au Order VI(14) ya Sheria ya Mwenendo wa kesi za madai (Civil Procedure Code au kwa kifupi tunaiita 'CPC').

Tazama pia maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye Kesi ya AGATHA MSHOTE Vs EDSON EMMANUEL, CIVIL APPEAL NO. 121 OF 2019.

Kama nyaraka isiposainiwa kabisa na mhusika ni kosa kisheria au ikisainiwa na mtu mwingine ambaye hana mamlaka au hajaruhusiwa ni kosa kisheria, na inaweza kupelekea kesi yako kufutwa kwa sababu ya kutumia nyaraka mbovu (defective plaint or WSD).
 

Attachments

  • FB_IMG_1712740044965.jpg
    FB_IMG_1712740044965.jpg
    124 KB · Views: 4
Back
Top Bottom