Je, Familia inaweza kushtaki ama kushtakiwa? Sheria inasemaje juu ya swala hili?

Jan 28, 2024
96
133
Labda nianze kwakusema wazi kwamba kwa mujibu wa sheria zetu Tanzania, Familia haiwezi kushitaki wala kushitakiwa. Kuelewa zaidi juu ya swala hili, nikukaribishe kuisoma Thread hii.​
ANGALIZO:
Thread hii inalenga kujibu swali la kisheria kuhusu uwezo wa familia kushitaki ama kushitakiwa, ikizingatia sheria za Tanzania. Maelezo yaliyotolewa ni kwa ajili ya kuhamasisha uelewa wa kisheria na sio ushauri wa kisheria rasmi. Ni vyema kushauriana na wataalamu wa sheria kwa masuala ya kisheria yanayohusiana na familia, haki ya kusimama mahakamani (locus standi), na masuala mengine ya kisheria. Maudhui haya hayapaswi kutumiwa kama msingi wa kesi au maamuzi ya kisheria bila ushauri wa kisheria kutoka kwa mwanasheria mwenye leseni. Tumia maelezo haya kama mwongozo tu na kwa ajili ya kujifunza.

Basankusu_-_typical_fired_brick_house.jpg

HAKI YA FAMILIA TANZANIA, KUFUNGUA AMA KUFUNGULIWA KESI
Sentensi "nataka kuishtaki familia yakena Z " au maneno mengine yeyote yanayoweza kuashiria mtu ama familia flani kutaka kuishtaki familia nyingine, ni moja ya sentence zilizozoeleka sana katika jamii yetu ya kitanzania haswa pale kunapokua na migogoro ya kifamilia. Lakini je, sheria inaruhusu familia kushitaki ama kushitakiwa?. Thread hii inalenga kujibu swali hilo kutokana na sheria zetu za Tanzania.

But, before going so far. What's Family? Familia ni kundi la watu ambao mara nyingi wana uhusiano wa damu, ndoa, au kupitishwa (adoption), na wanashirikiana katika masuala ya kijamii, kiuchumi, na kihisia. Familia inaweza kujumuisha wazazi na watoto wao, na pia ndugu wengine kama babu, bibi, na wajomba. Sasa ili kujua kama familia inayouwezo wa kushitaki ama kushitakiwa ni muhimu kuielewa kuhusu Haki ya Kusimama Mahakamani (Locus Standi). Sasa what's this?,

Locus standi ni haki au uwezo wa mtu au chombo cha kisheria kusimama mbele ya mahakama au mamlaka nyingine za kisheria kuleta kesi au kujibu kesi. Ni muhimu katika mchakato wa kisheria kwa sababu inahakikisha tu kwamba wale wanaoshiriki katika mchakato huo wana maslahi halali au uhusiano wa moja kwa moja na kesi hiyo.

Kwa mfano, katika kesi ya ardhi, mtu au chombo cha kisheria kinahitaji kuwa na locus standi ili kuweza kuleta kesi au kujibu kesi inayohusiana na ardhi hiyo. Hii inahakikisha kwamba watu wenye maslahi halali katika ardhi hiyo tu ndio wanaoshiriki katika mchakato wa kisheria unaohusiana na ardhi hiyo.

Kwa hiyo, locus standi ni msingi wa kisheria ambao huamua ni nani anaweza kuleta au kujibu kesi mbele ya mahakama au mamlaka nyingine za kisheria. Kuwa na locus standi kunahakikisha kwamba haki za watu zinaheshimiwa na mchakato wa kisheria unafanyika kwa njia sahihi na inayofuata sheria. Sasa hapa swali la msingi ni je, familia inayo hii haki (locus standi)?

Kama familia itakua na hii haki, basi inamaanisha itakua na uwezo wa kushitaki ama kushitakiwa. But if ni vise versa, itamaanisha familia haina uwezo wa kushitaki wala kushitakiwa. Wapo majaji kadhaa waliowahi kujadili juu ya swala hili katika maamuzi ya kesi kadhaa, hapa nitajitahidi baadhi ya kesi za kweli zilizowahi kutokea katika muktadha huu na namna ilivyoamuliwa.

Mosi, Jaji Itemba alijadili juu ya swala hili katika kesi ya Julius Kuperwa dhidi ya Familia ya Kafuku Mundamushimu.​
IMG_20240420_152802.jpg
Hii kesi ipo hivi. Takribani zaidi ya miaka 20 toka mzee Kafuku alipofariki December 13, 1990, familia yake haikufungua mirathi yake na kuendelea kuishi kama kawaida, mwaka 2018 ikatokea mgogoro wa aridhi baina yao na Julius Kuperwa katika moja ya mali (aridhi) za mzee Kafuku. Kwakua familia likua aijafungua mirathi basi kama familia ikaamua kufungua kesi katika baraza la kata la aridhi dhidi ya Julius . Baraza likaamua kua aridhi hiyo ni mali ya familia ya mzee Kafuku.

Julius akaona isiwe kinyonge, akakata rufaa katika baraza la aridhi na nyumba la wilaya (DLHT). DHLT nao wao wakaamua in favour of Familia ya mzee Kafuku kwa mara nyingine tena. Sasa hapa nigusie kidogo kuhusu rufaa kwafaida ya wengi kabla sijaendelea. Ni hivi, Rufaa ni mchakato wa kisheria ambapo mtu anaweza kuomba mapitio ya uamuzi wa mahakama ama chombo chochote cha sheria kilichosikiliza kesi yake kwa mara ya kwanza katika chombo ama mahakama nyingine iliyo na mamlaka makubwa zaidi ya hicho chakwanza. Hii inamaanisha kwamba kama mtu hakuridhika na uamuzi wa chombo cha sheria / mahakama ya chini, anaweza kupeleka malalamiko yake kwenye chombo / mahakama ya juu ili kupata hukumu ama uamuzi tofauti.

Vyombo ama Mahakama za juu zina uwezo wa kubatilisha au kubadilisha maamuzi yaliyofanywa na vyombo ama mahakama za chini kama itaonekana kwamba kulikuwa na makosa katika uamuzi wa awal. Kwa mfano, katika kesi za aridhi kama hii ya familia ya mzee Kafuku chombo cha kwanza chenye mamlaka ya kusikiliza kesi za hivi ni Baraza la aridhi la kata, hili lenyewe mamlaka yake ni limited to upatanishi, ikitokea mmeshindwa kupatana ama aujaridhika kwa vyovyote na maamuzi ya baraza la kata, unatakiwa kukata rufa kwenda Baraza la aridhi na nyumba la wilaya, usipo ridhika na hapa basi unaenda Mahakama kuu Divisheni ya Aridhi. Kama usipo ridhika na hapo pia unakata rufaa ya mwisho kwenda mahaka ya rufani.

Turudi kwenye kesi yetu sasa, kwaio baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya baraza la aridhi na nyumba la wilaya, Julius alikata rufaa tena kwenda mahaka kuu divisheni ya aridhi na ni kwenye huu kesi ya rufaa ndiyo Jaji Itemba alipojadili juu ya swala la locus standi ya familia ya Kafuku katika kesi hii. Hapa nitanukuu yale aliyoyasema Mh Itemba katika page ya 6 ya kesi hii, nanukuu.​
In this matter, I find that, as the owner of the plot in dispute is one Kafuku Mundamushimu who is the deceased, the respondent had no right to sue the appellant before the ward tribunal. Since the family doesn't have legal personality, it lacks capacity to sue or be sued. It is the administrator or executor of the deceased estate who has powers to sue in all causes of action which survived the deceased
Kwa kiswahili 👇
"Katika suala hili, ninaona kwamba, kwa kuwa mmiliki wa kiwanja kinachogombaniwa ni Kafuku Mundamushimu ambaye ni marehemu, mjibu rufaa (Familia ya Kafuku Mundamushimu) hawana haki ya kumshtaki (locus standi) mlalamikaji (Julius) mbele ya baraza la aridhi la Kata. Kwa kuwa familia haina utu wa kisheria, haina uwezo wa kushtaki au kushtakiwa. Ni msimamizi wa mali za marehemu pekee ambaye ana mamlaka ya kushtaki katika kila kesi inayohusu haki za madai ambazo ziliendelea baada ya kifo cha marehemu."​
Hapa kuna jambo la kujifunza katika hiyo sentence niliyoipigia mstari, sitoiongelea leo, lakini ni ya muhimu.

Mbali na kesi hiyo, ipo pia kesi ambayo iliongelea pia juu ya swala hili. Ni kesi baina ya Haridi Ahmad Khatibu dhidi ya Familia ya Ngunguni (Land Appeal No. 18 of 2023).
IMG_20240420_185428.jpg
Kwakua jibu tulilokua tunahitaji tayari tunalo, basi kesi hii sitoielezea lakini hapa nita nukuu kipande cha maneno ya Jaji Ebrahimu katika kesi hiyo, Nanukuu.
"In the instant case, the appellant sued Familia ya Ngunguni. A family unit being neither a natural person nor a juristic entity (corporate body) is devoid of locus standi and cannot sue or be sued in its name. Thus, it was a fatal anomaly to designate the 'Family ya Ngunguni' as the respondent.

A civil action like the one which was filed by the appellant in the trial Tribunal can only be instituted against a natural person or as in this case a juristic entity created and recognized by law. A suit instituted against a non-existent respondent or defendant as the case may be, is void ab initio."
Hapa, mahakama inamaanisha kuwa Familia ya Ngunguni haiwezi kushtakiwa au kushtaki kwa sababu ni kundi la familia na sio mtu halisi au kampuni. Hivyo, ilikuwa ni kosa kuitaja 'Familia ya Ngunguni' kama mshtakiwa. Kesi kama iliyofunguliwa na mlalamikaji inaweza kufunguliwa tu dhidi ya mtu halisi au kampuni iliyoundwa na kutambuliwa na sheria. Kufungua kesi dhidi ya mshtakiwa ambaye hana uwepo halisi ni batili kabisa tangu mwanzo (void ab initio).

Mwisho kabisa, k
wa kuzingatia ukweli kwamba familia haina uwezo wa kushtaki wala kushitakiwa kutokana na kukosa utu wa kisheria (legal personality) na haki ya kusimama mahakamani (locus standi) kama ilivyokuwa kwa Familia ya Ngunguni katika kesi ya Land Appeal No. 18 of 2023, haiwezi kushtakiwa. Mahakama ilieleza kuwa familia ni kundi lisilo na utu wa kisheria, hivyo haina uwezo wa kushtakiwa katika jina lake.

Hata hivyo, mahakama imefafanua kuwa katika kesi kama ile ya Familia ya Ngunguni, ni kosa kuitaja familia kama mshtakiwa. Mahakama ilieleza kuwa kufungua kesi dhidi ya familia ambayo haina uwepo wa kisheria ni batili tangu mwanzo (void ab initio), na kufanya hivyo ni kukiuka sheria za kusimama mahakamani (locus standi) na utu wa kisheria.

Nimatumaini yangu kuna lipo ulilojifunza ama jikumbusha kotoka katika thread hii. Stay connected for more.​
 
Nisaidie kiwango cha mamlaka za mahakama kwenye kiwango cha pesa..kuanzia primary, district na resident court
 
Nisaidie kiwango cha mamlaka za mahakama kwenye kiwango cha pesa..kuanzia primary, district na resident court
PC(Section 18(1)(ii)and(iii) of MCA- Rent Recovering not exceeding Tsh 50mln -Contract not Exceeding Tsh 30mln DC& RM(Section 40(2)of MCA: A: CIVIL Movable- not exceeding Tsh 200mln Immovable-not Exceeding Tsh 300mln B:COMMERCIAL Movable-Tsh 70mln Immovable-Tsh 100mln
 
Back
Top Bottom