SoC04 Tanzania tuitakayo ambayo itajali, kuboresha sheria za nchi na kuthamini haki za wafungwa magerezani

Tanzania Tuitakayo competition threads

kiroba kifupi

Member
Apr 10, 2020
92
162
UTANGULIZI.

👉 Watu hufungwa jela kwa sababu mbalimbali, zinazohusiana na kuvunja sheria za nchi.
images.jpeg

Picha kwa hisani ya mtandao.

👉 Adhabu ya kifungo jela inakusudia,
1. Kutoa adhabu.Kuwaadhibu wale waliovunja sheria na kuonyesha kwamba matendo yao hayakubaliki katika jamii.

2. Kuzuia Uhalifu. Kuwazuia wahalifu kufanya makosa zaidi na kutoa mfano kwa wengine ili wasivunje sheria.

3. Rehabilitation.Kuwapa wahalifu nafasi ya kujirekebisha na kujifunza kuwa raia wema kupitia programu za mafunzo na ushauri nasaha.

4. Kulinda Jamii.Kuwaweka wahalifu hatarishi mbali na jamii kwa kipindi fulani ili kulinda usalama wa raia wengine na usalama wao.

TUTAZAME DHANA TUNDUIZI.

👉
Tanzania tunayoitaka ni ile ambayo itaweka mbele umuhimu wa sheria na haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kuboresha sheria za nchi na kuthamini haki za wafungwa magerezani.

👉 Katika kuunda taifa lenye haki na usawa, mambo yafuatayo ni muhimu Sana kuyatafakari.,

1. Kuhakikisha Haki za Wafungwa. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa haki za wafungwa zinaheshimiwa, ikijumuisha haki ya kupata huduma za afya, chakula bora, na makazi mazuri. Haki hizi ni za msingi na zinapaswa kuheshimiwa bila kujali sababu za mtu kuwekwa gerezani.

2. Maboresho ya Sheria. Sheria zinapaswa kuboreshwa ili kuendana na wakati na hali halisi. Hii inajumuisha kurekebisha sheria kandamizi na zile ambazo hazizingatii haki za binadamu. Maboresho haya yanapaswa kujumuisha ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa sheria mpya au zilizoboreshwa zinaakisi mahitaji na matakwa ya jamii kwa ujumla.

3. Uwazi na Uwajibikaji. Mfumo wa haki unapaswa kuwa wazi na uwajibikaji lazima uwepo. Mahakama na vyombo vya dola vinapaswa kufanya kazi kwa uwazi, huku kukiwa na mifumo ya kukagua na kuhakiki mwenendo wa kesi na utendaji kazi wa maafisa wa serikali.

4. Elimu na Mafunzo. Elimu kwa maafisa wa sheria na askari magereza ni muhimu ili kuhakikisha wanatambua na kuheshimu haki za binadamu. Mafunzo haya yanapaswa kuwa endelevu na ya kina ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa haki na uadilifu.

5. Kupunguza Msongamano Magerezani. Njia mbadala za adhabu kwa makosa madogo madogo, kama vile huduma za jamii, zinaweza kupunguza msongamano magerezani. Hii itasaidia kuboresha hali za maisha kwa wale wanaobakia magerezani na kutoa nafasi zaidi kwa huduma bora.

6. Usawa na Utawala wa Sheria. Kila mtu anapaswa kuwa sawa mbele ya sheria, bila kujali cheo, hadhi au uwezo wa kifedha. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa hakuna anayesimama juu ya sheria na kwamba wote wanawajibishwa kwa matendo yao.

download.jpeg

NB: picha kwa hisani ya mtandao

MAPENDEKEZO BINAFSI KUHUSU HAKI ZA WAFUNGWA ZITAZOWALETEA NURU NA KUHISI WANATHAMIKA.

👉
Kutoa fursa za kazi ndani ya magereza ili wafungwa waweze kujipatia kipato, kujifunza stadi mpya, na kujihusisha katika shughuli za manufaa. Ajira hizi zinapaswa kuwa na malipo stahiki na mazingira salama ya kazi.

👉Kuwapa wafungwa angalau 10% ya mapato yanayotokana na kazi wanayoifanya wakiwa gerezani ni wazo zuri ambalo linaweza kuwa na manufaa makubwa kwao na kwa jamii kwa ujumla. Kiasi hiki cha fedha kinaweza kuwa akiba muhimu kwa wafungwa baada ya kumaliza vifungo vyao. Itawasaidia kuanza maisha mapya kwa urahisi zaidi na kupunguza uwezekano wa kurudia makosa.

👉Ushiriki wa Jamii.Wafungwa wanapolipwa kwa kazi zao, wanaweza kuchangia katika ustawi wa familia zao hata wakiwa gerezani. Hii inasaidia kudumisha uhusiano wa kifamilia na kupunguza mzigo wa kifedha kwa familia zao.

👉Kuwapa wafungwa haki ya ndoa kwa wenza wao wakati wakiwa kifungoni ni hatua muhimu inayoweza kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa magereza na haki za binadamu. Hii inaweza kutekelezwa kwa kuanzisha sheria mpya au kuboresha sheria zilizopo.

Itamsaidia mfungwa:.
1.Haki ya ndoa itasaidia kuhifadhi na kuimarisha mahusiano ya kifamilia, ambayo ni muhimu kwa ustawi wa kijamii na kihisia wa wafungwa na wenzi wao.

2. Kuwepo kwa uhusiano wa karibu na wa kudumu na mwenza wao kunaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo na matatizo ya kiakili yanayowakumba wafungwa.

3. Haki ya ndoa inaweza kusaidia wafungwa kurudi katika jamii wakiwa na mtazamo chanya na uhusiano mzuri na familia zao.

4. Kuwapa wafungwa haki ya ndoa ni sehemu ya kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa. Maana tunasema mahitaji makuu ya binadamu kamili mtu mzima ni chakula,malazi,mavazi ,na sex 😄.

👉
Kutambua na kuheshimu haki ya wafungwa kuoa au kuolewa wakiwa kifungoni ni hatua muhimu katika kuboresha haki za binadamu na kuimarisha mfumo wa magereza. Kwa kutekeleza sheria na taratibu zinazowezesha hili, nchi inaweza kujenga jamii yenye haki, usawa, na ustawi bora kwa wote.
👉Kuwapa wafungwa haki ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali za nchi ni hatua muhimu inayoweza kuimarisha demokrasia na haki za binadamu.
Kwanini tufanikishe hili???

1.
Haki ya kupiga kura ni haki ya msingi ya kiraia na kisiasa inayotambulika kimataifa. Kuwanyima wafungwa haki hii ni kinyume na misingi ya haki za binadamu na demokrasia.

2.Kuwapa wafungwa haki ya kupiga kura kunawasaidia kuhisi kuwa ni sehemu ya jamii na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii na kisiasa hata wakiwa gerezani.

3.Haki ya kupiga kura kwa wafungwa inachangia katika kujenga mfumo wa haki na usawa ambapo kila raia anapata fursa ya kushiriki katika maamuzi ya kitaifa bila ubaguzi.

4. Hatua hii inasaidia kuondoa ubaguzi na kuhakikisha kuwa wote wanajaliwe sawa na kwamba wafungwa hawabaguliwi kwa sababu ya hali yao ya kifungo.

👉Kuwapa wafungwa haki ya kupata likizo maalum kwa ajili ya kuhudhuria matukio muhimu ya kijamii, kama vile mazishi ya wapendwa wao, ni hatua inayoweza kuboresha hali zao za kiakili na kijamii, na kuchangia katika mchakato wa urekebishaji.

👉Kuwapatia wafungwa bima ya afya maalumu ambayo italipiwa kwa kazi wanazofanya wakiwa kifungoni ni Lengo linaloweza kuboresha afya na ustawi wao kwa ujumla.

KWA KUHITIMISHA TUBORESHE MAZINGIRA YA MAGEREZA YETU.

images (1).jpeg

NB: picha kwa hisani ya mtandao.

👉
Kuweka mazingira mazuri katika magereza ni muhimu sana kwa kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa na kuzuia mateso au adhabu isiyo ya haki.

👉 Mazingira ya gerezani yanapaswa kuwekwa vizuri ,Kwa sababu kila mmoja NI mfungwa mtarajiwa ,usipojiandalia mahala pazuri ,Kesho utateseka mwenyewe 😄 ukiwa kwenye mikondo ya sheria ,hasa pale utapoingia kwenye jinai Kwa kusingiziwa.

👉Mazingira mabaya yanaweza kuchochea au kuruhusu vitendo vya mateso au unyanyasaji ndani ya magereza. Kwa kuboresha mazingira, tunaweza kuzuia mateso na kuhakikisha kuwa wafungwa wanatendewa kwa haki na kwa staha.

👉Mazingira mabaya ya gereza yanaweza kuchangia katika kuvunja heshima na utu wa wafungwa, ambayo inaweza kusababisha mwenendo wa uhalifu baada ya kutoka gerezani. Kwa kuzingatia hili, kuboresha mazingira ya gereza kunaweza kusaidia kukuza tabia nzuri na uadilifu miongoni mwa wafungwa.

~ Alamsiki.
 
Rehabilitation.Kuwapa wahalifu nafasi ya kujirekebisha na kujifunza kuwa raia wema kupitia programu za mafunzo na ushauri nasaha.
Hii, hii ikipanuliwa zaidi tutapata rehabilitation sio tu ya wafungwa ni hadi ya taifa zima. Nasikiaga wachina wanaokuja kwenye miradi huku wengi wao ni wafungwa, ndo ya kuiga haya sasaa.

Kupunguza Msongamano Magerezani. Njia mbadala za adhabu kwa makosa madogo madogo, kama vile huduma za jamii, zinaweza kupunguza msongamano magerezani. Hii itasaidia kuboresha hali za maisha kwa wale wanaobakia magerezani na kutoa nafasi zaidi kwa huduma bora.
Nzuri, aliyeivuruga jamii kwa kiwango fulani.... akifanya kazi ya kuilipia hicho kiwango aende zake ameshalipa deni yake. Hasa kwa makosa yasiyohatarisha wengine.
Tumeenda sawa hadi kwenye zile haki za kufanya kazi na kulipwa ujira sawa. Haki zao za ndoa sawa japo kwa wanawake inabidi kuwe na ulazima wa njia za uzazi wa mpango. Na mazingira mazuri tu kwa ujumla.

Isipokuwa nina swali hapo kwenye kupiga kura. Huoni kama tunaweza kuwa tunajipinga wenyewe? Wafungwa wamefungiwa huko kwa sababu wamekataliwa kukaa na jamii kutokana na kutoendana na mkataba unaotufunga kuishi kijamii (written and unwritten social contracts) wamevunja visheria fulanifulani. Sasa tutamuaminije tena kupiga kura na kuwachagulia raia namna ya kuishi, seea na kuongozwa???
 
Nzuri, aliyeivuruga jamii kwa kiwango fulani.... akifanya kazi ya kuilipia hicho kiwango aende zake ameshalipa deni yake. Hasa kwa makosa yasiyohatarisha wengine.
Natamani tutoke kwenye sheria za kikoloni tuje kwenye sheria za kujengana na kuleana.
 
Tumeenda sawa hadi kwenye zile haki za kufanya kazi na kulipwa ujira sawa. Haki zao za ndoa sawa japo kwa wanawake inabidi kuwe na ulazima wa njia za uzazi wa mpango. Na mazingira mazuri tu kwa ujumla.
Mkuu unahofia watazaliana jela 😃??,kama anafanyakazi na anaujira kiasi chake maisha yanaweza kuendelea,Sera na miongozo itawalinda hawa ,mafunzo ya tabia na sheria za nchi sio lazima mitutu ya bunduki hata Kwa alieiba kuku 😸.
 
swali hapo kwenye kupiga kura. Huoni kama tunaweza kuwa tunajipinga wenyewe? Wafungwa wamefungiwa huko kwa sababu wamekataliwa kukaa na jamii kutokana na kutoendana na mkataba unaotufunga kuishi kijamii (written and unwritten social contracts) wamevunja visheria fulanifulani. Sasa tutamuaminije tena kupiga kura na kuwachagulia raia namna ya kuishi, seea na kuongozwa???
Je mwanao akivunja mlango katika kucheza kwake! ,hutamlaza ndani siku hio ?? Je utataka alale nje???(HAKI NA WAJIBU)
- NI kwamba Kunyima haki ya kupiga kura kwa kundi moja la watu, hata kama ni wafungwa, kunaweza kuonekana kama aina ya ubaguzi. Jamii inayofuata misingi ya usawa na haki inapaswa kutoruhusu aina yoyote ya ubaguzi wa haki za msingi.
-Pia mkuu Kwa matakwa ya sheria za nchi Mfumo wa haki ya jinai unalenga si tu kuadhibu BALI pia kurekebisha tabia. Kuwaruhusu wafungwa kupiga kura inaweza kusaidia katika mchakato wa kurekebisha na kuwaunganisha tena na jamii.
 
Back
Top Bottom