Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

We pasco itakua unapumuliwa kisogoni,zanzibar ni nchi naitabakia kua nchi kashindwa babu yako nyerere kuigeuza znz mkoa mtaiweza nyie.
 
haws wazanzibati ambao wapo ccm na wanatetea muundo wa serikali mbili mf dr maua daftari ni wajinga sana.
na wameshawaona wanaccm wenzao wa bara wanaotetea serikali mbili ni mapimbi sana.
ukweli ni kwamba hawa wazenj akina maua daftari mtazamo wao ni Chetu chetu chakwao chetu.
watanganyika tusiwe mazoba tuipiganie serikali yetu hata ikibidi kuuvunja huu muungano.
huu muungano kiukweli na kihalisia hauna faida yeyote kwetu sisi watanganyika
 
Ukiumbuke mwanzo mke alitoka nje ndipo akaomba uhuru zaidi, ataingia chumba cha kukutania stakapo jisikia yeye!. Huke kwake akiendelea kupokea wageni!. Utaweza kuvumilia?!.
Pasco

hahahaaa !ujue hata mke anauhakikamume anatoka nje kimyakimya! sema mum hasemi!
 
Ndio....kumbe Tanganyika iliolewa?
mwanamke akiolewa hubadili jina na kua mrs. lakini mwanaume habadili jina akioa.
Na mpaka hapo leo ndo nimejua kumbe
Mme ni ZANZIBAR na mke ni TANGANYIKA ndo maana jina la mke likafa na mme likabaki
Kuna watu wanapenda kufa, kuoza. Hujaona mtu kapenda hadi kila kitu kakabidhi kwa mke?.
P
 
Wanabodi,

Mungu Ibariki Tanzania!.

Muungano Milele na utalindwa kwa gharama yoyote!.

Paskali
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

pasco nakuita hivi maana ndio jina nimelizoea tokea miaka ile..
Kwanza nikupe hongera kwa mabandiko yako mengi humu na naamini siku moja watu wengi watakuwa wakiyarejea kwa wakati husika na kisha kutambua ni nini ulikuwa ukikiona kwa wakati ule.

Hili la serikali kuwa moja mimi binafsi naliafiki na ndio maana halisi ya muungano.

kuna vitu huwa najiuliza iweje tuseme nchi moja ilihali vitu vingi viko tofauti?

Toa kitu visiwani kilete bara utaambiwa lipia kodi kama vile umekitoa nchi nyingine sasa hii haileti maana kabisa ya muungano yapo mengi sana ambayo yanashangaza na aina hii ya muungano wa sasa.
 
Toa kitu visiwani kilete bara utaambiwa lipia kodi kama vile umekitoa nchi nyingine sasa hii haileti maana kabisa ya muungano yapo mengi sana ambayo yanashangaza na aina hii ya muungano wa sasa.
Mkuu Fast Forward , ni kweli kwenye huu muungano wetu adhimu wa nchi moja, kuna vitu vingine ni vya ajabu sana!. Mfano lile sakata la sukari ya kiwanda cha Maruhubi Zanzibar, kukataliwa kuingia Bara!, huku Tanzania bara tuna uhaba wa sukari, tunaagiza nje ya nchi!.

Halafu hali ya kiajira upande wa visiwani hasa serikali ya kimapinduzi, taasisi zingine mfano jeshi la polisi au TPDF au TRA ndio utaona watu kutoka bara ila nafasi za wawakilishi hautakaa uone mtu kutoka bara japo huku bara mtu wa visiwani anaweza kuwa mbunge kwa huku.

Suala la sukari ni kituko sana yaani sijui ilikuwaje hawa jamaa wakafanya lile jambo namna ile.

Tunashida sana ya maono na uamuzi kwa viongozi wetu.
 
Tanganyika iliungana na Waafrika kutoka bara kuwapinduwa Wapemba na Waunguja—Wazanzibari.
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Pamoja na kwamba mada ni ya muda mrefu na pia Muungano wenyewe siupendi na wala sioni kama una maana yoyote zaidi ya sisi Watanganyika kujigeuza mabwege na kuruhusu kutawaliwa na Wazanzibar hadi wilayani huko kwa kuwekewa ma DC kutoka Zanzibar wakati huko Zanzibar Mtanganyika haruhusiwi hata kuwa mjumbe wa nyumba 10,yaani siwezi kuita huu ni muungano bali tumeamua kutawaliwa na Zanzibar hii ni aibu kubwa.
Ebu angalia leo hii Rais tunayemuita wa muungano ni Mzanzibar anateuwa kila kiongozi huku Tanganyika lakini hana mamlaka ya kuteua hata afisa tarafa kule Zanzibar!
Lakini nilichotaka kujua kutoka kwako mleta mada unapofananisha huu "Muungano" ni sawa na ndoa je nani mume na nani mke? Au unamaanisha Tanganyika ndiyo mke na Zanzibar ndiyo mume na ukizingatia kwa sasa Tanganyika ndiyo tunatawaliwa na raia wa Zanzibar?
 
Back
Top Bottom