Ndoa ya DUBE na Azam FC sheikh ni TFF, Hana mkataba?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,331
12,647
Mkataba halali kati ya Dube na Azam FC ni ule unaoishia msimu wa mwaka 2024 ambao umeidhinishwa na TFF (sheikh) kuwa ni mkataba (ndoa) halali.

Maana hata kama Binti mmekubaliana wenyewe kuoana, makubaliano hayo hayatatambulika kama mke na mume mpaka ndoa ifungwe kwa idhoni ya wazazi na mfungishaji ndoa (sheikh, Mchungaji, serikali) hiyo.

Kwenye mpira mamlaka ya ufungishaji ndoa kati ya mchezaji na club ni TFF kuidhimisha makubaliano ya mchezaji na timu kuwa ndoa halali.

Je, mikataba wa Dube na Azam FC unaoishia 2026 umeidhinishwa na TFF kuwa mkataba halali? Uko TFF?

Kama haukuidhinishwa na TFF ni fake na TFF hatakiwi kuwa shahidi Wala hakimu wa kesi hiyo.
 
Chupli chupli za Azam, halafu utashangaa kuambiwa timu zina wanasheria, sijui huwa wanafanyakazi gani?

Hili si la Azam tu, inaonekana huu NI upuuzi unaoendelea Kwa timu zote za Tanzania, ubabaishaji.
 
Chupli chupli za Azam, halafu utashangaa kuambiwa timu zina wanasheria, sijui huwa wanafanyakazi gani?

Hili si la Azam tu, inaonekana huu NI upuuzi unaongelea Kwa timu zote za Tanzania, ubabaishaji.
Kosa kubwa lilitendeka huko nyuma kwa kufanikisha uhamisho wa Morrison na Faisal Salim kwenda "Simba na Azam ".

Ukiaangalia kwa ndaaaaani utaona malengo yalikuwa kuidhoofisha Yanga bila kujua kuwa wanaweka standard mpya kwa timu na wachezaji.

Sasa hivi wanamjadili Dube bila kumuambatisha na Fei toto na Morrison.
 
Hii tabia walitengeneza TFF
Mchezaji anasaliti team eti hana furaha anataka kuondoka katikat ya msimu hakuna dirisha la usajili

Walimtetea feisal, sasa dube, atakuja mwingine na mwingine
 
Hii tabia walitengeneza TFF
Mchezaji anasaliti team eti hana furaha anataka kuondoka katikat ya msimu hakuna dirisha la usajili

Walimtetea feisal, sasa dube, atakuja mwingine na mwingine
Sheria inawalazimisha kumtendea Dube kama alivyotendewa wengine waliofanya kosa kama hili ili kuepusha double standard.

Wachambuzi wetu ambao wako against na Yanga wanataka Dube apewe adhabu kubwa sana kuonyesha mfano, shame on them.
 
Hii tabia walitengeneza TFF
Mchezaji anasaliti team eti hana furaha anataka kuondoka katikat ya msimu hakuna dirisha la usajili

Walimtetea feisal, sasa dube, atakuja mwingine na mwingine

Lakini mbona suala la feisal TFF walikuwa upande wa Yanga? Maana FEI baada ya kuvunja mkataba Yanga walikimbilia TFF ambapo Feisal alifeli mara 3 zote aliambiwa ni mali halalai ya yanga. Kama anataka kuvunja mkataba akubaliane na Yanga kwanza? Ila sasa kuna wacha-mbuzi na wacha-kuku ndio walizingua
 
Mkataba wa Yanga na Fei ulikuwa upo TFF, haukuwa na shida, shida ilikuwa namna ya kuuvunja. Mkataba wa Dube unaobishaniwa hajulikani kule TFF.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom