SoC04 Tahadhari zaidi inahitajika dhidi ya Mauaji ya Kinyama nchini, na si kusubiri yatokee ndipo tushughulike nayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Language Therapist

New Member
Apr 28, 2024
3
0
Screenshot_20240503-091308_1.jpg
Screenshot_20240429-195729_1.jpg
UTANGULIZI:
Miaka ya hivi karibuni watanzania tumekuwa tukipokea taarifa au kushuhudia mauaji ya kinyama kutoka mikoa mbalimbali nchini. Bila shaka wote tunatambua kuwa kumtoa mtu uhai wake ni kinyume na haki za binadamu kwani unamuondolea haki yake ya kuishi. Swali la kujiuliza ni: Je, kwa nini ufikie hatua ya kumwua binadamu mwenzio mwenye utashi na hisia kama zako? Hakika huu ni unyama na hatuna budi kufanya jitihada zote kutokomeza hali hii nchini.

Baadhi ya matukio ya mauaji yaliyowahi kuripotiwa na kuzua taharuki kutoka sehemu mbalimbali nchini:
Kwa mujibu wa BBC NEWS SWAHILI, Januari 27, 2022 baadhi ya maeneo nchini yaliripotiwa kukumbwa na changamoto ya mauaji yaliyowahi kutokea mfululizo mwanzoni mwa mwaka 2022. Baadhi ya matukio na maeneo hayo yalibainishwa kama ifuatavyo:

Dodoma; watu wasiojulikana nyakati za usiku walivamia ndani na kuwaua mume, mke, watoto wawili na mjukuu mmoja.

Mwanza; wanawake watatu waliuawa na watu wasiojulikana na kutupwa kando ya mto eneo la Nyakato.

Mtwara; mfanyabiashara Mussa Hamisi aliuawa kikatili na mwili wake kutupwa kitongoji Cha Majengo.

Dar es Salaam; watu wawili walikamatwa kwa tuhuma za kula njama na kumwua mwanamke mmoja "Barke Rashid" eneo la Tabata Segerea baada ya kupewa kitita cha fedha cha shilingi Milioni 1.7 na aliyekuwa mpenzi wake.

Hayo ni baadhi tu ya mengi yaliyowahi kuripotiwa. Yapo mengine mengi kama vile mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinos), vikongwe, na wanaotuhumiwa kuiba mitaani.

Je, nini chanzo cha mauaji haya ya kinyama katika jamii ya kitanzania?

Wivu wa kimapenzi; suala hili limechukua nafasi kubwa sana, na tumepoteza wanajamii wengi kwa mauaji ya kikatili yanayohusisha wivu wa kimapenzi. Waathirika wakubwa ni jinsia zote mbili, kwani hata wanaume wameripotiwa kuuawa na wenza wao kutokana tu na wivu au usaliti.

Tamaa ya Mali na fedha; watu wengi hususani vijana wamekuwa wakishiriki katika mauaji haya ili kujipatia fedha au mali. Wauaji hawa hulipwa na watu wengine ili kukamilisha mauaji hayo, au huua watu ili kupora mali walizonazo.

Mila potofu na ushirikina; mara kadhaa tumepata taarifa kutoka sehemu mbalimbali nchini hususani vijijini ambako ndiko waliko waathirika wengi wa suala hili. Vikongwe wanacharangwa mapanga kwa kudhaniwa ni wachawi kwa sababu tu ya macho yao mekundu na mwonekano wao. Maalbino nao waliuawa sana na watu waliohitaji viungo vyao wakiamini vitawapa utajiri.

Hasira na visasi; baadhi ya watanzania walishawahi kupitia changamoto mbalimbali zikiwemo kudhulumiwa Mali zao, kudhalilishwa, kuuliwa ndugu au wapendwa wao na kadhalika. Hali hii huwapa msongo wa mawazo na kuwajaza hasira, hatimaye huamua kulipiza kisasi kwa kuua.

Pombe na matumizi ya madawa ya kulevya; pombe kupita kiasi na madawa ya kulevya huathiri akili ya binadamu na kumfanya awe na maamuzi maovu ikiwemo ukatili. Ukichunguza hata washiriki wengi wa mauaji utabaini kuwa kabla ya kufanya mauaji hutumia madawa ya kulevya ili kujitoa akili ya kawaida na kujivika akili ya kikatili isiyo na hofu yoyote. Baadhi ya walevi wameripotiwa kuwaua wenzi wao ama watoto na wao pia kujiua.

Kujiokoa; baadhi ya watanzania walishawahi kukutana na nyakati ngumu za kuhatarisha maisha yao aidha kwa kuvamiwa ama vipigo vikali kutoka kwa watu wao wa karibu. Hivyo, katika kujinusuru wamejikuta wakikua aidha kwa makusudi ama pasipo kukusudia.

Mauaji haya yana athari gani kwa jamii na Taifa kwa ujumla?

Kupandikiza visasi na chuki; ni dhahiri kwamba dhambi moja huzaa dhambi nyingine ikiwa tahadhari haitachukuliwa. Uchunguzi umeonesha kwamba ndugu wa waathirika wa mauaji haya hujazwa na chuki na hupania kulipiza visasi, na ndiyo maana tunashuhudia mauaji ya siri, yaani watu wasiojulikana.

Kupoteza nguvukazi ya Taifa; kupitia mauaji haya tunapoteza watendaji kazi wengi na walipaji kodi wa sekta mbalimbali, ambao kupitia wao uchumi wa nchi hukua kwa namna moja ama nyingine.

Kuishi kwa mashaka; katika hali ya kawaida watanzania wamezoea mazingira ya amani. Hivyo basi nyakati za mauaji haya wengi hukumbwa na taharuki na baadhi yao kushindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali.

Kuvunjika kwa familia na kuongezeka kwa utegemezi na watoto wa mitaani; Mauaji haya huwapoteza watu wanaotegemewa na familia zao. Hivyo basi kuondoka kwao husambaratisha familia zao pia kutokana na kukosa uwezo wa kujikimu. Athari hii huzaa athari nyingine zaidi kama vile watoto wa mitaani, wizi, ukahaba na matumizi ya madawa ya kulevya.

Nini wajibu wa serikali, taasisi, jamii na mashirika mbalimbali katika kutokomeza mauaji haya? Serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali zikiwemo za kielimu na kidini, inaweza kupanga mikakati madhubuti ya kutokomeza mauaji haya angalau kuanzia sasa na miaka ijayo.Yafuatayo yafanywe ili kujenga jamii salama dhidi ya mauaji:

Suluhu iwe ndiyo ngao yetu; serikali itoe elimu ya kutosha kwa jamii juu ya umuhimu wa suluhu katika migogoro ya kimapenzi, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Watu wakae chini na kuzungumza kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali ili kuondoa tofauti zao.

Jamii ijiepushe na visasi; suala hili linaonekana ni dogo, lakini ukweli ni kwamba jamii nyingi hususani vijijini wanahitaji kuelimishwa zaidi kuhusu madhara ya visasi.

Msisitizo juu ya mafundisho ya kidini na hofu ya Mungu; serikali ishirikiane kuwekeza katika kuandaa kizazi chenye maadili ya kibinadamu na hofu ya mwenyezi Mungu. Hii itawaepusha pia na mila potofu na ushirikina. Washiriki wengi wa mauaji ukiwachunguza utabaini kuwa hawakuwekewa misingi ya kidini au kimaadili tangu awali.

Kuimarisha ulinzi binafsi na jamii kwa ujumla; wananchi wanaomiliki mali au fedha nyingi waelekezwe kujiwekea ulinzi madhubuti, raia wa kawaida pia waepuke kutembea peke yao nyakati za usiku na kukaa maeneo hatarishi hususani katika baa za pombe na makasino.

Udhibiti wa matumizi ya pombe na vita dhidi ya madawa ya kulevya; Serikali idhibiti na kusimamia kiwango cha unywaji wa pombe hali kadhalika kuzuia kwa nguvu zote uingizwaji na utumiaji wa madawa ya kulevya nchini.

ANGALIZO:
Suala la ulinzi na usalama wako dhidi ya mauaji linaanza na wewe mwenyewe. Licha ya serikali kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia mauaji ya watu wake kupitia mapendekezo yaliyotolewa, inampasa kila mwananchi kuchukua tahadhari binafsi na kutoa taarifa mapema kwenye vyombo husika, mara tu atakapoona dalili au viashiria vya kutokea kwa mauaji ya aina yoyote.
 
Wivu wa kimapenzi; suala hili limechukua nafasi kubwa sana, na tumepoteza wanajamii wengi kwa mauaji ya kikatili yanayohusisha wivu wa kimapenzi. Waathirika wakubwa ni jinsia zote mbili, kwani hata wanaume wameripotiwa kuuawa na wenza wao kutokana tu na wivu au usaliti.
Hili janga asee tunahitaji kuhakikisha walezi na mashuleni wanawafunza watoto wao akili ya kudhibiti hisia, emotional intelligence.
Mila potofu na ushirikina; mara kadhaa tumepata taarifa kutoka sehemu mbalimbali nchini hususani vijijini ambako ndiko waliko waathirika wengi wa suala hili. Vikongwe wanacharangwa mapanga kwa kudhaniwa ni wachawi kwa sababu tu ya macho yao mekundu na mwonekano wao. Maalbino nao waliuawa sana na watu waliohitaji viungo vyao wakiamini vitawapa utajiri.
Kuna haja ya serikali kuangazia mitume, manabii, waganga, makanisa na masinagogi wanapofundishana imani potofu na shuhuda zinazochochea ongezeko la imani potofu TZ. Tunaenda wapi kama Taifa?.
Kupandikiza visasi na chuki; ni dhahiri kwamba dhambi moja huzaa dhambi nyingine ikiwa tahadhari haitachukuliwa. Uchunguzi umeonesha kwamba ndugu wa waathirika wa mauaji haya hujazwa na chuki na hupania kulipiza visasi, na ndiyo maana tunashuhudia mauaji ya siri, yaani watu wasiojulikana.
Ewaa, unasemaje mtoa mada kuhusu sheria kwa hao wanaopandikiza hizo chuki?
Msisitizo juu ya mafundisho ya kidini na hofu ya Mungu; serikali ishirikiane kuwekeza katika kuandaa kizazi chenye maadili ya kibinadamu na hofu ya mwenyezi Mungu. Hii itawaepusha pia na mila potofu na ushirikina. Washiriki wengi wa mauaji ukiwachunguza utabaini kuwa hawakuwekewa misingi ya kidini au kimaadili tangu awali.
Nakazia, je athari zinazotokana na dini tunaziepuka vipi. Mauaji ya kisa dini ya mojakwamoja yapo, na ya kupitia kwa kutiana shuhuda za chuki pia yanawezekana.
ANGALIZO:
Suala la ulinzi na usalama wako dhidi ya mauaji linaanza na wewe mwenyewe. Licha ya serikali kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia mauaji ya watu wake kupitia mapendekezo yaliyotolewa, inampasa kila mwananchi kuchukua tahadhari binafsi na kutoa taarifa mapema kwenye vyombo husika, mara tu atakapoona dalili au viashiria vya kutokea kwa mauaji ya aina yoyote
Vizuri, ulinzi na usalama ni jukumu la kila raia.
 
Hili janga asee tunahitaji kuhakikisha walezi na mashuleni wanawafunza watoto wao akili ya kudhibiti hisia, emotional intelligence.

Kuna haja ya serikali kuangazia mitume, manabii, waganga, makanisa na masinagogi wanapofundishana imani potofu na shuhuda zinazochochea ongezeko la imani potofu TZ. Tunaenda wapi kama Taifa?.

Ewaa, unasemaje mtoa mada kuhusu sheria kwa hao wanaopandikiza hizo chuki?

Nakazia, je athari zinazotokana na dini tunaziepuka vipi. Mauaji ya kisa dini ya mojakwamoja yapo, na ya kupitia kwa kutiana shuhuda za chuki pia yanawezekana.

Vizuri, uli
 
Back
Top Bottom