Kumbukumbu ya miaka 30 tangu kutokea mauaji ya Kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda

Jul 8, 2013
48
65
Nchi ya Rwanda inaadhimisha miaka 30 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994.

kumbukumbu inayofanyika Jijini Kigali na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Ulaya, Amerika na Asia wakiongozwa na Rais Paul Kagame.

Ishara ya kuanza kwa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ni pamoja na kuwashwa kwa mishumaa katika eneo la Gisozi mahala ambapo mabaki ya miili ya watu zaidi ya 250,000 imezikwa katika kaburi la pamoja.

Mauaji hayo ya kimbati yalianza April 7, 1994 siku Moja baada ya Ndege iliyombeba Rais wa wakati huo Juvenali Habyarimana na aliyekuwa Rais wa Burundi Cyprian Ntaryamira kudunguliwa wakati ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kigali.

Baada ya tukio hilo majeshi ya serikali ya wakati huo na makundi yenye silaha ya Impunzamugambi na Intarahamwe yaliyokuwa na unasaba na chama tawala MRND yalianza kuwaua watu wa Jamii ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Karibu watu milioni Moja waliuawa Hadi kufikia mwezi Julai ambapo Vikosi vya vuguvugu la Ukombozi wa Rwanda yaani Rwanda Patriotic Army, RPA vilipofanikiwa kukomesha mauaji hayo baada ya kuudhibiti mji wa Kigali.

Baadhi ya viongozi wa Afrika wanaohudhuria kumbukumbu hizo ni Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa Madagascar Andrey Rajoelina, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadera, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali, Naibu Rais wa Kenya Rigath Gachagua na Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo.

Ujumbe wa serikali ya Marekani unahudhuria kumbukumbu hizo unaongozwa na Rais wa zamani Bill Clinton.

Wakati wa Mauaji hayo mataifa kadhaa jirani na Rwanda yalibeba jukumu kubwa la kuwahudia wakimbizi wa Rwanda waliokuwa wakiiimbia nchi hiyo.

Katika kitabu Cha safari ya maisha yangu kilichoandikwa na Rais wa awamu ya pili Hayati Alhaji Ali Hassan Mwinyi ameeleza namna serikali yake ilivyokuwa ikoshughulikia wakimbizi kutoka Rwanda waliokuwa wakimiminika Kila siku nchi hususani katika wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Nayo Jumuiya ya Kimataifa hasa mataifa ya Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na Uingereza yamelaumiwa kwa kutochukua hatua za haraka kuiepusha Rwanda dhidi ya tukio hilo baya licha ya kuwepo kwa viashiria vya kutokea kwa mauaji hayo.

Umoja wa mataifa uliunda mahakama maalumu ya kushughulikia kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ambayo ilikuwa na makao Yale jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.

Katika uhai wa mahakama hiyo zaidi ya watu 60 wakiwemo waliokuwa maafisa wa serikali ya Rwanda, waandishi wa habari akiwemo Hassan Ngeze walihukumiwa vifungo vya muda mrefu kutokana na kuhusika kwao katika mauaji hayo.

Aidha katika kushughulikia kesi za washukiwa na wahusika wa mauaji hayo serikali ya Rwanda iliunda mahakama maalumu ya kijamii iitwayo Gacaca ambayo watuhimiwa walikiri makosa na kuomba msamaha kwa watu waliopoteza mapendwa wao.

Ni wazi mauji ya kimbari ya Rwanda yatasalia kuwa miongoni mwa matukio mabaya katika historia ya ulimwengu.

Miaka 30 Sasa wanyarwanda kupitia kauli mbiu Yao iitwayo Kwibuka wameendelea kuinuka na chini ya uongozi shupavu wa Rais Paul Kagame, Rwanda imeibuka kutoka kuwa Taifa lililofeli na kuwa sehemu ya matumaini kwa maisha ya binadamu.

Imeandaliwa na Fredrick Nwaka
Mwanahabari, Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC
 
Nilipata mualiko lakini niliamua kupiga kimya kwasababu kumbukumbu zenye zimejaa ulaghai kupitiliza.Mfano mzuri wanatudanganya eti mauaji ya kimbari ya watutsi wakati hata wahutu walikufa.

Siwezi kushiriki katika masuala yaliyojaa ulaghai.
🙂🙂🙂acha hasira mkuu
 
waachane nayo hayo maadhimisho yalishapita. kuendelea kuadhimisha ni kufufua kumbukumbu.
 
Nayo Jumuiya ya Kimataifa hasa mataifa ya Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na Uingereza yamelaumiwa kwa kutochukua hatua za haraka kuiepusha Rwanda dhidi ya tukio hilo baya licha ya kuwepo kwa viashiria vya kutokea kwa mauaji hayo.
Wapigane wao halafu walaumiwe wengine ambao hawakuwepo
 
Wapigane wao halafu walaumiwe wengine ambao hawakuwepo
hahaha muafirika kila siku anatafuta wa kumtupia lawama kwa makosa yake ya uchache wa akili
wazungu waliona wafirika kwa wafiirika wanataka kuchinjana wakaona wawaache. nami naona walifanya uamuzi mzuri wazungu.
 
hahaha muafirika kila siku anatafuta wa kumtupia lawama kwa makosa yake ya uchache wa akili
wazungu waliona wafirika kwa wafiirika wanataka kuchinjana wakaona wawaache. nami naona walifanya uamuzi mzuri wazungu.
🤣
 
Back
Top Bottom