Tahadhari: Sarafu ya pesa ya nchi yoyote inapatikana kwa kubadilishana na bidhaa tujikite kuzalisha bidhaa na kuuza nje

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,907
9,328
Ndugu na marafiki, habari za Jumamosi ya leo, Tarehe 02/09/2023.

Ndugu zangu, leo napenda kutoa elimu moja juu ya sarafu za mataifa mengine, bila kusahau sarafu yetu ya shilling.

Zipo sarafu nyingi hapa duniani, kama vile Yuan ya China, Yen ya Japan, ruble ya Urusi, dola ya Marekani, euro, pauni, n.k.

Sarafu zote hizi mtu yeyote anaweza kuzimiliki zikawa zake. Njia kuu ya kuzimiliki hizi sarafu ni kwa njia ya kufanya biashara, yaani kuuza bidhaa au huduma fulani ndio upate hizo sarafu.

Hakuna njia ya mkato ya kuzipata hizo sarafu. Sarafu zote, ikiwa ni pamoja na sarafu ya Kenya, ili uzipate inatakiwa ufanye biashara fulani.

Hivyo ndugu zangu, tukijihusisha na uzalishaji wa bidhaa na kuziuza nje ya nchi, tutaweza kupata hizo sarafu kirahisi, na mwisho wa siku, tutakuwa na hifadhi ya kutosha ya hizo sarafu.

Tunayo bidhaa nyingi hapa nchini ambazo tunaweza kuzipeleka nje ili kubadilishana na hizo sarafu. Mfano, madini ni mojawapo ya bidhaa ya haraka haraka ambayo tukiuza hata leo, itatuletea hizo sarafu.

Sitoweza kuzitaja njia zingine za kupata hizo sarafu. Mimi binafsi ni mwamini wa uzalishaji, naamini kuzalisha bidhaa ndio uchumi halisi usio feki. Na ndiyo unaweza kutupeleka mbele.
 
Kama una ufahamu wa masoko ya nje namna yanavyopatikana weka hiyo elimu pia...

Kuandika tu kwamba mwananchi anaweza akauza nje pasipo kumpa ufahamu wa namna gani, itakuwa haisaidii bado...
 
Hata tukuomba msaada zinakuja hizi pesa na ndio tumejikita huko kwa sasa mambo ya kuzalisha bidhaa ni magumu sana kwa nchi kama yetu
 
Hata tukuomba msaada zinakuja hizi pesa na ndio tumejikita huko kwa sasa mambo ya kuzalisha bidhaa ni magumu sana kwa nchi kama yetu
Hata tukuomba msaada zinakuja hizi pesa na ndio tumejikita huko kwa sasa mambo ya kuzalisha bidhaa ni magumu sana kwa nchi kama yetu
 
bila shaka unazungumzia namna ya kupandisha thamani hela yetu.
 
Back
Top Bottom