SoC04 Suluhisho la msongamano wa magari barabarani na faida zake

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mkoba wa Mama

Senior Member
May 5, 2021
119
49
Utangulizi
Kutokana na ongezeko kubwa la magari hasa katika maeneo ya mjini ni wakati sasa wa serikali kuchukua hatua madhubuti ili kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini na kulinda miundombinu ya barabara.

Moja ya hatua zinazoweza kuchukuliwa ni pamoja na ujenzi wa barabara maalum kwa ajili ya magari ya mizigo pembezoni mwa miji ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya miji na kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini.

Kwa mfano katika jiji la Dar es salaam, magari ya mizigo yanayotoka na kuingia bandarini na yale yanayopita kutoka mikoa mingine kwenda nje ya nchi au mikoani yote yaelekezwe katika barabara hizo maalum.
Barabara hizo zitumike kwa magari ya mizigo tu bila kuingiliana na magari mengine au watembea kwa miguu.

Faida na manufaa yake

Kupunguza Msongamano wa Magari Katikati ya Miji:

Kutapunguza idadi ya magari makubwa yanayopita katikati ya miji. Hii itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kufanya safari za mijini kuwa za haraka na zenye ufanisi zaidi. Hii ni kwa sababu magari mengi ya mizigo huenda kwa kasi ya taratibu zaidi lakini pia huchukua nafasi kubwa barabarani kutoka na ukubwa wa magari hayo.
Lakini pia barabara hizo zinaweza kutumika kwa misafara ya viongozi na misafara mingine kutoka mkoa mmoja hadi mwingine kwa njia ya barabara ili kupunguza adha wanayokutana nayo watumiaji wengine wa barabara pale kunapokuwa na misafara ya viongozi.

Kuboresha Ufanisi wa Usafirishaji wa Mizigo:
Barabara hizi zitatoa njia mbadala na za moja kwa moja kwa magari ya mizigo, kupunguza muda wa safari na gharama za usafirishaji. Kwa njia hizi, mizigo itafika kwa wakati na kuongeza ufanisi wa shughuli za usafirishaji.

Kupunguza Uharibifu wa Barabara za Mijini:
Magari makubwa ya mizigo yanasababisha uharibifu wa barabara kutokana na uzito wake lakini pia kutokana na kusimama sehemu moja kwa mda mrefu sababu ya msongamano mkubwa wa magari.

Kwa kuelekeza magari haya kwenye barabara maalum zitakazo jengwa kulingana na uzito wa magari hayo, barabara za katikati ya miji zitadumu kwa muda mrefu na kupunguza gharama za matengenezo na ukarabati wa mara kwa mara.

Kuboresha Ubora wa Hewa na Kupunguza Uchafuzi wa Mazingira:
Kupunguza msongamano wa magari katikati ya miji kutapunguza utoaji wa gesi chafu zinazotokana na magari yaliyopo kwenye foleni yanayo simama kwa mda mrefu. Hii itachangia kuboresha ubora wa hewa, Kupunguza uchafuzi wa mazingira na kupunguza magonjwa yanayotokana na uchafuzi wa hewa.

Kuimarisha Usalama Barabarani na Kupunguza Ajali za barabarani:
Tumekuwa tukishuhudia mara nyingi ajali zinazotokana na magari ya mizigo kugongana na magari madogo au magari ya abiria na kupelekea vifo vya watu wengi na kuwaacha wengine na ulemavu wa kudumu, lakini pia mara kadhaa tumeshuhudia malori ya mafuta yakilipuka barabarani tena karibu kabisa na makazi ya watu na maeneo ya biashara na kusababisha athari kubwa ikiwemo vifo na uharibifu wa mali za watu.

Barabara mpya pembezoni mwa miji zitasaidia kuimarisha usalama wa watumiaji wote wa barabara kwa sababu barabara hizo zitakuwa maalum kwa ajili ya magari ya mizigo tu bila kuingiliana na magari mengine na watembea kwa miguu.

Kuongeza Ufanisi wa Huduma za Dharura:
Kupunguza msongamano wa magari katikati ya miji kutasaidia magari ya huduma za dharura kama vile magari ya kubeba wagonjwa na magari ya zimamoto kufika haraka kwenye maeneo ya dharura au sehemu husika, hivyo kuokoa maisha ya wagonjwa wanaowahishwa hospitali, kuokoa maisha ya wahanga wa ajali za moto na nyinginezo na kupunguza uharibifu wa mali kutokana na majanga mbalimbali.

Kuboresha na Kuchochea Maendeleo ya Kiuchumi:
Barabara mpya pembezoni mwa miji zitasaidia kukuza biashara na viwanda vilivyo nje ya miji. Hii itachangia katika ukuaji wa uchumi wa maeneo haya na kupanua fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo ya pembezoni.

Kusaidia Mipango Miji na Maendeleo Endelevu:
Kujenga barabara maalum kwa maroli na magari ya mizigo ni sehemu ya mipango bora ya miji. Itasaidia kupanga miji kwa namna endelevu, kupunguza msongamano na kuwezesha usafiri wa haraka na salama kwa wananchi, hivyo kufika kwa wakati sehemu husika.

Kupunguza Gharama za Usafiri:
Wakati msongamano unapopungua, matumizi ya mafuta yanaweza kupungua kwani magari hayakai muda mrefu kwenye foleni. Hii itapunguza gharama za usafiri kwa wakazi wa miji na kwa wale wanaotumia magari binafsi kutumia gharama ndogo katika ununuzi wa mafuta na kufanya maisha kuwa nafuu zaidi.

Kuongeza Ufanisi wa Usafiri wa Umma:
Wakati ambapo maroli na magari yote ya mizigo yatakapokuwa yakipita nje ya miji hii itaunguza msongamano wa magari na kutasaidia kuboresha huduma za usafiri wa umma kama vile mabasi na daladala. Hii itawafanya watu wengi zaidi kutumia usafiri wa umma, na hivyo inaweza hata kupunguza matumizi ya magari binafsi. Kwa sababu watu watakua wakifika safari zao kwa wakati pasipo kukaa barabarani kwa mda mrefu.

Kupunguza Kelele Mijini:
Msongamano wa magari unachangia kelele za mjini ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya akili na uzalishaji wa watu. Kuondoa magari makubwa kutapunguza kelele hizo, na kufanya mazingira ya mijini kuwa tulivu zaidi na kuruhusu watu kufanya kazi zao katika hali ya utulivi, usikivu na kwa amani zaidi.

Kuimarisha Usafirishaji wa Bidhaa na Huduma:
Kwa nyakati tofauti kumekuwepo na changamoto ya bidhaa kuchelewa kufika katika masoko kutokana na magari ya mizigo kushindwa kufikisha bidhaa ndani ya mda unaotakiwa Barabara hizi zitasaidia kuunganisha maeneo ya bandari kavu, viwanda, maghala na masoko, hivyo kurahisisha usafirishaji wa haraka na salama zaidi wa bidhaa na huduma.

Kukuza Matumizi ya Njia Mbadala za Usafiri:
Kupunguza magari makubwa barabarani kutachochea watu kutumia njia mbadala za usafiri kwa safari fupi kama vile baiskeli na kutembea kwa miguu. Hii itachangia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuboresha afya ya umma kwa sababu itakua ni njia mojawapo ya kufanya mazoezi.

Kuboresha Uwezo wa Kukabiliana na Majanga:
Barabara mpya pembezoni mwa miji zitakuwa muhimu sana wakati wa majanga ya asili kama mafuriko au tetemeko la ardhi. Zitatumika kama njia mbadala za kuhamisha watu na kusafirisha msaada wa dharura haraka zaidi.

Kupunguza Msongo wa Mawazo kwa Watumiaji Wengine wa Barabara.
Watu wamekuwa wakijikuta na msongo wa mawazo unaosababishwa na foleni yo barabarani, hasa wanapofikiria kuanza safari mda wa kwenda kazini, shuleni au katika biashara na shughuli nyingine wakiwa na hofu ya kuchelewa kufika, lakini pia mda wa kurejea nyumbani wanatumia mda mwingi barabarani hivyo kushindwa kupata mda wa kutosha wa kupumzika na familia zao na pia kupumzisha miili na akili.
 
Moja ya hatua zinazoweza kuchukuliwa ni pamoja na ujenzi wa barabara maalum kwa ajili ya magari yote ya mizigo nje au pembezoni mwa miji ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya miji na kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini.
Nnaona ni wazo zuri tu, panapowezekana kutenganisha matumizi ya barabara.

Kupunguza msongamano wa magari katikati ya miji kutapunguza utoaji wa gesi chafu zinazotokana na magari yaliyopo kwenye foleni yanayo simama kwa mda mrefu. Hii itachangia kuboresha ubora wa hewa, Kupunguza uchafuzi wa mazingira na kupunguza magonjwa yanayotokana na uchafuzi wa hewa.
Kwenye kuboresha hali ya hewa kuna haja pia ya kuweka miundombinu ya miti pembezoni au kutenganisha barabara. Maana kupunguza gesi mbaya lazima kuendane na kutengeneza oksijeni nzuri.

Kujenga barabara maalum kwa ajili ya magari ya mizigo pembezoni mwa miji ni hatua muhimu kwa kuboresha mfumo wa usafiri na maisha mijini. Faida zake ni nyingi na zinajumuisha kupunguza msongamano, kuboresha usafirishaji wa mizigo, kuimarisha usalama barabarani, na kuchangia katika maendeleo endelevu ya miji. Ni muhimu kwa serikali na wadau wa maendeleo kuwekeza katika miradi hii ili kuboresha hali ya maisha na ufanisi wa kiuchumi katika miji yetu
YAs mojawapo wa hatua nzuri tunazoweza kuchukua.

Lakini pia mleta mada nikuulize, je hauhisi kuwa kwa hali hii tutaingia hasara ya kugeuza taifa zima kuwa ni mabarabara tu? Je umewaza kuhusu mbinu nyingine kama bandari na reli?
 
Tulishindwa kupanga mapema matokeo yake ndiyo hayo, mfano kwanini hadi leo hatujengi barabara nne kwenye miji yetu hasa inayokua,tunasubiri muujiza hupi?
 
Back
Top Bottom