CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,059
- 4,225
CCM YAPONGEZA JITIHADA ZA RAIS SAMIA KUIWEZESHA DIT
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Chama Cha Mapinduzi kimeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiwezesha Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kutekeleza mradi wa ujenzi wa vituo vya umahiri ambapo zaidi ya Sh. bilioni 100 zimewekwa na Serikali.
Akizungumza baada ya kufanya ziara fupi DIT, Shaka amesema wamekuwa wakienda maeneo mbalimbali kukagua na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 katika mashirika na taasisi ambazo zimepewa dhamana na Serikali.
“Kumekuwa na jitihada kubwa zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi kupitia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kwenye uwekezaji wa fedha nyingi za maendeleo maeneo mbalimbali. Moja ya eneo ambalo pengine hatujafika kuona namna ambavyo fedha zimewekwa na utekelezaji unaendelea ni eneo hili lililobeba teknolojia.
“Nikisema teknolojia tunamanisha mfumo mzima wa mabadiliko haya ya kidunia na hapa nazungmzia TEHAMA, leo tumepata fursa hii kuona namna ambavyo wenzetu wa DIT wanatumia utaalamu huu kubadilisha miundombinu hii ya magari kutoka kwenye mafuta kwenda kwenye gesi.
== ==
Soma pia...
DIT INATEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM KWA VITENDO IUNGWE MKONO -SHAKA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema kazi nzuri inayofanywa na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kubadilisha mfumo wa magari kutoka kutumia mafuta kwenda katika matumizi ya gesi, ni kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo.
Amesema hatua hiyo itachichea matumizi ya teknolojia na kwenda sawa ma mkakati wa kutumia rasilimalinzilizopo nchini kujikwamua kiuchumi.
Shaka amesema hayo ndiyo maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi, hivyo amepongeza Rais Samia Suluhu Hassan a ambaye ametoa zaidi ya sh. Bilioni 100 kwa ajili kuendeleza vituo vya umahiri ambavyo ni muhimu kwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi.