Serikali Kuwasaidia Wajasiriamali Kuzalisha Bidhaa Bora Ili Kupata Soko la Uhakika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,037
974
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amesema kuwa mpango wa Serikali katika kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora ili kupata masoko ya uhakika.

Mhe. Kigahe amabainisha hayo Aprili 16,2024 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Ester Malleko ambaye alitaka kujua mpango wa Serikali wa kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na kupata masoko ya uhakika.

Mhe. Kigahe amesema Serikali imeweka mipango kadhaa ya kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora ili kupata masoko ya uhakika ikiwa ni pamoja na kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwasaidia wajasiriamali wadogo kupata maeneo/majengo ya kuzalishia bidhaa zao, kuwapatia mitaji kupita Mfuko wa NEDF na nembo ya ubora wa bidhaa zao kwa miaka mitatu bila gharama.

pia amesema kupitia SIDO, TBS na Wakala wa Vipimo (WMA) kuendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu kanuni za uzalishaji wenye tija, elimu ya utambuzi wa vifungashio na ufungashaji bora.

Aidha amesema kuwa SIDO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuendelea kuandaa na kuratibu maonesho mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa ni sehemu ya kuchagiza ukuaji wa soko la bidhaa zinazozalishwa na Wajasiriamali.

Katika swali la nyongeza, Mhe. Malleko alitaka kujua mpango wa serikali wa kufanya mapitia ya sera ya biashara na sera ya wajasilimali adogo ambazo zimepitwa na wakati na kutaka kujua mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wajasiriamali wanazalisha bidhaa zenye ubora.

Akijibu maswali hayo, Mhe. Kigahe amesema ni kweli sera hizo zimepitwa na wakati na kuwa Serikali imeshaanza taratibu za mapitio ili ziweze kuendena na hali ya soko la ndani na nje na mahitaji ya sasa ya wajasiliamali na pia Serikali imepanga kuweka mazingira mazuri kwa wajasiriamali ili kuweza kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango bora.

WhatsApp Image 2024-04-17 at 11.58.37 (1).jpeg
IMG-20231005-WA0023.jpg
 
Back
Top Bottom