SoC01 Serikali iwekeze katika Muziki, Michezo na Kilimo ili kukuza Uchumi kwa Vijana wa kitanzania na Taifa kwa ujumla

Stories of Change - 2021 Competition

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
779
Nipende kuwasalimu ninyi nyote, habari za muda huu! Niende kwenye mada moja kwa moja. Tanzania ni kati ya nchi maskini duniani japo ina rasilimali muhimu na nyingi karibia kila mkoa.

Je tatizo linatokea wapi mpaka ongezeko la vijana wasio na ajira kuendelea kuwa kubwa?

Katika uchumi kuna kitu kinajulikana kama "Demand and Supply" kwamba kwa kila uitaji wa kununua kuwe sawa na kiwango cha bidhaa zilizopo sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Hiyo principle ya uchumi ambayo ilishafanyiwa utafiti na kutiki, kimoja kikiwa kikubwa zaidi ya kingine kutakuwa na madhara katika uchumi.

Mfano endapo uitaji wa kununua bidhaa umekuwa mkubwa kuliko bidhaa zilizopo sokoni kwa ajili ya kuuzwa, tegemea kuona bei ya bidhaa hiyo kupanda kwa sababu kila mtu ataitaji bidhaa hiyo ili aipate.

Kwa nini kwenye uzi wangu nimesema sekta mbili muhimu? Ni katika kutaka kuzingatia uhalisia wa nadhalia hiyo ya uchumi kinyume na watu wengi ambao wakitoa mapendekezo ya mafanikio ya uchumi hawazingatii nadhalia hiyo na mwisho wa siku ukija kupima maoni yao kiuchumi unakuta yamepwaya kwa sababu wameongelea upande mmoja na kusahau upande mwingine wa hoja yake endepo utapindua meza na kwenda kichume na mawazo yake nini kitatokea!
Kama point ni demand iwe sawa na supply, mwingine anaweza kusema "production should be equal to consumption" kwamba kiwango cha uzalishaji kiwe sawa na kiwango manunuzi. Kinyume cha hapo kama ni kwenye biashara kama unazalisha kingi lakini unauza vichache elewa hiyo biashara sio rahisi kuendelea kwa sababu utajikuta gharama za uzalishaji zinakuwa kubwa kuliko kiwango cha mauzo unayokusanya.

Kwa kusema hivyo napendekeza sekta hizi mbili muhimu serikali iongeze uwekazaji wa kutosha kwenye sekta hizo;
1. Kilimo,
2. michezo na muziki

Hizo ndo sekta muhimu kuinua uchumi wa taifa na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wengi chini Tanzania. Mfano kwa mwaka 2014, Tanzania ilikadiriwa kuzalisha vijana zaidi ya laki sita tayari kuingia katika soko la ajira wakati soko lenyewe lilikuwa na uwezo wa kuchukua vijana chini ya 100,000.

Kumbe kwa kuangalia maelezo hayo hapo juu tunaona namna tatizo la ajira lilivyokuwa kubwa Tanzania mpaka hivi sasa.

Unaweza kuniuliza kwa nini nimechagua sekta hizo mbili tu na kuacha sekta nyingine kama sekta ya Madini, utalii n.k, jibu ni jepesi tu nimefanya utafiti kwa sekta zote na ndio nikabakiwa na sekta hizo mbili kwamba ni mukombozi kwa vijana endapo serikali kwayo itaongeza uwekezaji.

Unapochagua sekta ya uwekezaji lazima uzingatie kitu inajulika kama " Cost Benefit Analysis" ili mwisho wa siku upate sekta ya kuiendeleza ambayo inaleta matokeo makubwa hasa kwa wananchi wako. Ukisema uendeleze sana sekta ya madini au ya utalii au ya kwa mfano, hizo ni sekta Nzuri kuendelezwa ila zisiwe na kipaumbele cha kwanza katika kuendelezwa kwa sababu ni "sekta baguzi" kwamba zinaitaji watu wachache tena wengi wao wawe wasomi.

Lakini tunajua namna mfumo wetu wa elimu usivyo rafiki kwamba idadi ya vijana wengi wanafeli na kushindwa kuendelea naasomo ya juu wanabaki mtaani huku idadi ndogo inayopanda kwenda vyuo vikuu wanashindwa kupambana kwa soko la ajira kutoka na elimu duni itolewayo kwenye vyuo vyetu. kibaya zaidi tumeingia kwenye muungano wa Africa mashariki tukaruhusu sera ya "free mobility of labor force" wakati wenzetu wameboresha mfumo wa elimu yao unawaruhusu vijana wao wengi kuongoza kuajiriwa katika umoja huu.

Na kwa kuzingatia hayo ndo maana nikaja na huu utafiti. Tuanze na sekta ya Michezo na Muziki. dah! Napenda sana sekta hii, kwa sababu imeinua sana maisha ya vijana wenzetu wengi. hivi ni nani kwake haoni miziki, tamthilia, movie au michezo? Nani asiyependa vitu hivyo?

Vijana wanapata utajiri mkubwa kwenye muziki na michezo. Hivi mnaweza kuniambia Diamond Platinum, Alikiba, Rayvany, Harmonize, Mbana Ali Samatta, Idris Sultan, Vicent Kigosi, Saimon Msuva, Marioo, Darasa, Zuchu, Stive Nyerere, John Boco na wengine wengi wana Academic Masters za masomo gani?!! Utashangaa hawana hiyo elimu tukimaanisha kwamba wengi wao wameishia elimu ya kidato cha nne ila kwa ukwasi wao ni mara hata tano ya wasomi wengi wenye degree na masters tuliopo Tanzania.

Shida sio kusoma hadi masters, shida ni gharama mtu anazotumia kusoma hadi level ya degree au masters halafu unakuja kuwa jobless.

kumbe kama akina harmonize wasio na elimu ya vyeti wametoboa hadi kuwa wasanii wakubwa wanaoeleweka Afrika na duniani, kumbe serikali kama ingekuwa serious katika kuitendea haki sekta ili ikue zaidi ya hapa ilipo na kuacha tabia ya kuwatumia tu wasanii kipindi cha kampeni ya uchaguzi hakika tungeona mapinduzi makubwa sana na maendeo makubwa kwenye uchumi wetu kwa sababu kadiri mtu mmoja anavyotoka kwenye ukosefu wa ajira na kuingia kwenye ajira hasa Muziki au michezo au filamu reflection yake inaenda kuonekana kwenye ukuzi wa uchumi kwa sababu msanii huyo ataajiri na yeye wataalam wake, atanunua magari, atajenga nyumba n.k

Mfano kutoka kwenye ukurusa wa THE AFRICA REPORT.com uliochapisha andiko tarehe 1/8/2014. Kwamba katika mwaka 2011, serikali ya Nigeria chini ya uongozi wa Bwana Goodluck Jonathan waliweza kutoa kiasi cha shs za kitanzania zaidi ya billion 400 kwa ajili ya kusapoti kazi za wasanii hasa waigizaji wa filamu.

Baada ya miaka 3 ya uwekezaji huu, taasisi ya filamu Nigeria ijulikanayo kama Nollywood iliweza kuongeza volume ya uzalishaji huku ikiwa ya pili duniani, wakati huo huo ikaongeza mapato kwenye tasnia hadi nafasi ya tatu nyuma ya Bollywood ya India na Hollywood ya Marekani.


Kwa mfano huo nasema pia sekta michezo, muziki na filamu vinaweza kuleta mapinduzi makubwa, narudia tena hili litafanikiwa tu endapo serikali itaunga mkono kwa vitendo ukuaji wa sekta hiyo.

kipi kifanywe na serikali ili kukuza sekta hizo;
1. Tuanze na sekta ya muziki na filamu;
√ Serikali ihakikishe kila wilaya kuna chuo cha Veta, ndani ya chuo hicho ihakikishe kuna kozi ya kujifunza muziki na filamu hapo pia ihakikishe vyombo vya mziki vya kisasa vinakuwepo ndani ya vyuo hivyo.​
✓ pia ndani ya vyuo hivyo, serikali ihakikishe kuna MUSIC/ FILM RECORDING STUDIO yenye hadhi ya kutengeneza muziki au filamu nzuri kutokea huko huko mikoani walipo sio mpaka wasafiri kuja Dar ili waweze kurekodi, hii itasaidia kuongea vipaji vya wasanii wengi visifie mikoani.​
Twende kwenye michezo serikali ifanye haya kuleta mapinduzi ya Michezo yenye kuleta mafanikio na ajira kwa vijana.
✓ Umitashumita na Umiseta viendelee na mwisho wa siku watoto wenye vipaji wapelekwe kwenye chuo cha michezo.​
✓ serikali isimamie na ihakikishe kila timu hasa za ligi kuu na za ligi daraja la kwanza zinakuwa na timu za watoto na vijana wawe wamesajiriwa kwenye hizo team ( hiyo iwe lazima takwa la kisheria)​
✓ Viwanja vinavyotumika kuchezewa mpira kwa ligi kuu , hasa pitches lazima viwe vya kiwango cha kimataifa. Pitches zitazoruhusiwa ni kama ile ya Azam complex, uwanja wa Mkapa na uhuru. Ni bora timu zote 18 za ligi kuu kucheza kwenye viwanja 5 vyenye hadhi ya kimataifa kuliko kuonesha mechi za ligi kuu kwenye viwanya vibovu kama vya Namungo, Mwadui, karume musoma N.k viwanja hivyo vinashusha sana hadhi ya ligi kuu yetu Tanzania na mwisho wa siku tunakosa uwekazaji mkubwa kutoka nje ya nchi. Kumbuka viwanja hivyo vibovu vinashusha hadhi ya ligi yetu kimataifa japo tuna dabi kubwa barani Afrika ( mechi ya Simba na Yanga)​
Sasa turudi kwenye mwanzo wetu kule kwamba ili uchumi ukue huku ukiwa balanced lazima Demand iwe sawa na supply ili kuepusha uchumi usitetereke.

Sekta ya Michezo, muziki na filamu watu wake kutokana na kulipwa pesa nyingi Hawa wanakuwa sana ni wanunuzi wa bidhaa na huduma hivyo wanakuwa kwenye upande wa Demand. Sasa endapo serikali haitasimamia hilo ongezeko la demand, mfuko wa bei utatokea na hivyo bei za bidhaa zitaenda juu. Kwa sababu maitaji makubwa ya binadamu yapo katika kupata chakula cha kila siku kwa hiyo kuasaidia sekta zingine bila kuboresha sekta ya Kilimo ni kuchochea mkaa kwenye uchumi wako.

2. Sekta ya Kilimo.
Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya Kilimo ndo maana nikaunganisha sekta hii kwenye huu uzi wangu ili kuonesha uhusiano uliopo kati ya demand side na supply side, sekta ya kilimo ndo inakuja kuweka usawa wa vipato vikubwa walivyo navyo watu katika taifa husika kwa sababu sasa watu watakuwa na uhakika wa kupata chakula kwa sababu sekta ya kilimo itakuwa imeboreshwa.

Njia ambazo serikali inaweza kutumia kuleta matokeo makubwa kwenye sekta ya kilimo ni pamoja na;
✓sekta ya kilimo nimeichagua kwa sababu sio sekta baguzi kwa maana inatoa nafasi ya ajira kwa watu wote kwa waliosoma na wasiosoma. Hivyo kwa kuwa serikali inataka kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana sekta hii inaajiri watu wengi.​
Kinachotakiwa kifanyike ni Serikali kujua idadi ya mapori na mashamba yasiyoendelezwa nchi nzima. Baada ya kumaliza kutambua ukubwa wa hekali za mapori na aina ya kilimo kinachofaa hapo serikali iamue kuyagawa bure kwa vijana wake umri kati ya miaka 18 hadi 35. Kinachotakiwa kifanyike ni vijana hao wanaungana kuanzia wa 5 hadi 10 wanaomba shamba hekali 1 nakupewa bure. Hii itasaidia watanzania kuweza kutumia rasilimali ardhi kubwa iliyoachwa idle bila matumizi yoyote karibia kila mkoa. Vijana kwa kuwa watakuwa na hakika ya kupata ardhi ya mashamba bure mikoani itakuwa rahisi kwao kutoka mijini na kurudi mashambani kuzalisha bidhaa za kilimo.​
✓kitu kingine serikali huko mashambani ihakikishe inaweka mifumo ya maji ili kuruhusu kilimo cha umwagiliziaji ili vijana watakaenda kujiajiri huko vijijini wasikose maji ya uhakika katika mashamba yao.​
✓ Na mwisho kabisa serikali itapaswa kutumia bajeti yake kuagiza matrekta ambayo yatatumika katika kilimo cha vijana hao huko mashambani.​
Kwa kusema hayo na kuzingatia sekta hizo mbili muhimu tutakuwa na uhakika wa kujenga uchumi imara wa vijana na wa taifa kwa ujumla huku tukiwezesha ukuaji wa uchumi unaoenda sambamba kati ya upande wa manunuzi na uzalishaji.​
Thanks​
Tchao​
 
Back
Top Bottom