Serikali ifanye maamuzi magumu ya kupiga marufuku bodaboda mimi zitumike vijijini tu kupungiza ajali au iweke kodi kubwa zisiingie nchini kwa wingi

Tatizo ni kuwa serkali haibuni ajira kwa vijana
Serkali ikizuia bodaboada bila kubuni ajira nyingine tarajia ujambazi wa kutisha km miaka ya 90
 
Nchi hii kuna viongozi wa ajabu sana.Walivipiga marufuku Vipanya vya abiria 20 kuingia katikati ya jiji la Dar ila wakaruhusu bodaboda na bajaj kuingia katikati ya jiji
Bajaji zilianza Route moja tu ya kariakoo Kivukoni kwa ajili ya walemavu. Sasa hiv mjini kote ni bajaji na bodaboda tupu.
Tunaenda kufanana India soon.
Yaan waliondoa Daladala na kuruhusu bajaji
 
Leo hii kuna ajali imetokoe huko. Misungwi ambapo bodaboda zinazodaiwa kuwa katika mwendo wa kasi zimegongana na waliokuwa kwenye hizo pikipi kuungua moto vibaya sana ingawa wanacnhi waliwaokoa kwa kuwamwagia mchanga. na sidhani kama wote wame-survuve (mtu anaangua kama nyama iliyowekwa kwenye wavu ikichomwa).

Nimeona clip kwakweli inaumiza sana kuona mwanadsmu mwenzako anateketea kwa moto na kuja kuokolewa dakika za mwisho na sijui kama watapona.

Nafikiri wakati umefika watanzania na serikali kwa ujumla tupige hesabu ya faida na hasara ya hizo bodaboda licha ya ukweli kuwa bodaboda hizi zimekuwa. zikitoa ajira kwa mamia kama sio maelefu ya vijana wa Kitanzania.

Binafsi nafikiri wakati umefika kwa serikali kufanya maamuzi magumu ya kupiga marufuku hizo bodaboda ingawa najua kelele zitakuwa kubwa na sasa itahusika sana.

Kama ni lazima sana, option mojawapo iwe ni hizi bodaboda kupigwa kabisa marufuku maeneo ya mijini zibaki kutumika vijijini ambako barabara haziruhusu sana kuendesha hizi pikipiki kwa kasi kama huku mijini ambapo miundombinu ni bora ila ni hatari sana kwa hizo bodaboda.

Option nyingine ni serikali kuweka kodi kubwa ili kupunguza kabisa uingizaji wa hizi bodaboda humu nchini na baadae zitoweke kabisa.

Bodaboda zikitoweka au kupigwa marufuku, ni wazi kutakuwa na madhara kwa waliojiajiri katika hiyo kazi na sisi wote tunaotumua bodaboda katika safari kama vile kwenda/kuwahi makazimi, sehemu za biashara na kufikia maeneo ambayo magari hayafiki kabisa.

Hata hivyo, ni bora watu wakateseka kwa kukosa ajira au huo usafiri, kuliko kuacha kundi kubwa la vijana wa Kitanzania wakipoteza maisha na wengine kupata ulemavu kisa tu ajira jambo ambalo linaweza kutatuliwa watu wakiamua kukaa chini na kutafuta suluhisho la ajira kwa vijana wetu.
Naunga mkono hoja. Tujiulize tu kabla ya ujio wa bodaboda kama njia ya usafiri tulikuwa tunatatua vipi changamoto za usafiri.

Kiukweli tumejiendekeza tu kupanda bodaboda. Imagine mtu anatoka TRA Longroom pale karibu na Central Police anakodi boda kwenda Askari Monument??

Bodaboda zitumike kuwatoa watu swekeni kama Mabwepande kuwaleta Bunju A. Baada ya hapo daladala ziendelee kubeba watu wa main roads
 
Kwa anayefahamu dynamics za ukuaji wa miji kiholela km inavyotokea kwa miji mingi Africa na pace ya maendeleo kwa ujumla huwezi zuia boda boda, tafuta namna ya kupambana na uvunjifu wa sheria unapotokea..si boda boda wote ni wavunjifu wa sheria.
 
Serikali yoyote duniani huwalinda huwalinda wananchi wake. Kuna kipindi serikali ya nchi moja ya Ulaya ilipiga marufuku kuendesha skuta za kukodi wakati wa usiku baada ya kuona vijana wengi wanapata ajali wakati wanatoka night club!
Wanakwambia wamepata ajira.watakuja kula kwako?
 
Issue ya bodaboda wanaichukulia poa. Ila naamini tukipata takwimu vizuri za ajali za bodaboda kwa mwezi, siziopikwa. Ni hatari
 
Kwa tulipofikia ni vigumu kuzuia hiyo biashara, watawala nao wanapenda waendelee kutawala hawana haja ya kutafuta purukushani. Cha muhimu japo wengi niliona wakilaumu aliyechukua video kwenye Lile tukio wakidai ilibidi akafanye uokozi badala ya kuchukua video. Sasa bila video kama hizo kuwafikia hao bodaboda Kona zote za nchi wakajionea ikawa Somo unafikiri wataelewa? Elimu itolewe zaidi, tusifiche matukio ya ajali ziwekwe wazi waone kinachotokea.
 
Wanakwambia wamepata ajira.watakuja kula kwako?
Kuwekewa sheria na kanuni za kuwalinda ajali kutawafanya waje kula kwangu? Bodaboda inatakiwa walindwe kwa kudhibitiwa. Serikali yoyote inayowajibika huwa inachukuwa hatua pale inapoona madhara yanatokea
 
Kuwekewa sheria na kanuni za kuwalinda ajali kutawafanya waje kula kwangu? Bodaboda inatakiwa walindwe kwa kudhibitiwa. Serikali yoyote inayowajibika huwa inachukuwa hatua pale inapoona madhara yanatokea
Kumbe hata wewe haujui mleta mada anataka nini.haya soma tena uelewe
 
Nadhani kwa busara tusingesema Serikali ipige marufuku bali iboreshe usafiri wa UMMA ili kusiwepo na ulazima wa Bodaboda in the first place...

Lakini what do I know...., Ni kama unalaumu watu kutumia vidole kula tambi wakati hakuna umma wala vijiti.....
 
Kumbe hata wewe haujui mleta mada anataka nini.haya soma tena uelewe
Nimeelewa vizuri kabisa. Tatizo ni kuwa hujui nilichojibu nini. Mimi nimejibu comment iliyosema kuwa serikali haipaswi kufanya lolote kwa sababu wao bodaboda hawajihurumii. Mimi nikatoa mfano wa nchi ya Ulaya iliyokataza watu kuendesha skuta za kukodi wakati wa usiku kwa sababu walevi wengi walikuwa wanaziendesha wakiwa wamelewa na kupata ajali. Yaani nimeonyesha maana ya serikali kujali wananchi wake i.e. serikali kuweka sheria. Upo?
 
Nimeelewa vizuri kabisa. Tatizo ni kuwa hujui nilichojibu nini. Mimi nimejibu comment iliyosema kuwa serikali haipaswi kufanya lolote kwa sababu wao bodaboda hawajihurumii. Mimi nikatoa mfano wa nchi ya Ulaya iliyokataza watu kuendesha skuta za kukodi wakati wa usiku kwa sababu walevi wengi walikuwa wanaziendesha wakiwa wamelewa na kupata ajali. Yaani nimeonyesha maana ya serikali kujali wananchi wake i.e. serikali kuweka sheria. Upo?
Ni kweli hawajihurumii.hakuna watoto pale.hata useme uwachape fimbo hawatasikia.kikubwa acha wafe.wenye akili watazingatia sheria za barabarani.dunia ya sasa si yakuoneana huruma.jihurumie kwanza wewe
 
Back
Top Bottom