Rais Samia wape meno TFS, anzisha kampeni ya upandaji na utunzaji Miti Tanzania nzima. Iongozwe na vijana wa kujitolea JKT

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,247
26,149
Nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mama!

Kwanza nikupongeze kwa Mafanikio makubwa yanayoonekana kwenye suala la kuwahamisha Machinga na kuwapeleka maeneo rasmi. Na furaha nchi sasa imeanza kupendeza hasa majiji yetu! Nimepita Posta mpya leo na Kweli nimeiona Posta niliyoijua miaka ya 90 mwanzoni. Hongera Kwa hili! Majiji Yanaanza kupendeza bila ya kutumia ubabe wala bunduki!

Nirudi kwenye mada yangu!

Leo napenda tena kutumia fursa hii kukushauri Mhe Rais wa JMT Mama yetu Samia Suluhu Hassan baada ya kufanya utafiti kidogo juu ya hali ya mazingira hapa Tanzania.

Kwenye utafiti wangu huu, nimegundua mambo yafuatayo ambayo yamenifanya Leo niandikie humu kukushauri!

1. Nyanda za Juu kusini hasa mikoa ya Iringa, Mbeya na Songwe kuna hatari kubwa sana ya mikoa hii kukubwa na ukame miaka michache ijayo. Hii ni kutokana na shughuli za ukataji miti zinazoendelea kwa kasi kwenye mikoa hii na kasi ndogo ya kupanda Miti kwenye mikoa hii. Mikoa hii ni moja ya mikoa tegemezi kwa uzalishaji chakula. Ukataji wa Miti na kuongezeka kwa ukame kwenye mikoa hii kunaleta hatari ya mikoa hii kutozalisha chakula cha kutosha huko miaka ya mbele na kuifanya nchi kuanza kuwa tegemezi kwenye chakula! Mikoa hii pia ndo inatoa maji Kwa ajiri ya mto ruaha mkuu ambao unaenda kuungana na mto kilombero na baadae rufiji. Kukosekana kwa maji kwenye mto huu kutaleta shida Hadi kwenye upatikanaji wa maji kwenye bwawa linalojengwa la Umeme la Mwl Nyerere

2. Kanda ya Kati hasa Dodoma , Singida na Tabora hali ni mbaya sana. Kuna ukame mkubwa sana kwenye haya maeneo na hali ikiendelea kuwa hivi Kuna hatari kubwa hii mikoa kushindwa kabisa kuzalisha chakula. Hakuna Miti na wala Hakuna jitihada zozote kuongeza Miti na uoto kwenye maeneo haya.

Kwa Tabora ambako kulikuwa na Miti mingi, kwa sasa Kuna ukataji mkubwa sana wa miti unaofanywa na wahamiaji kutoka mikoa ya kanda ya Magharibi na kanda ya Ziwa. Wahamiaji hawa wanaharibu kweli mazingira na kusema kweli tusipoangalia hii mikoa itakuja kukosa kabisa mvua na uoto mzuri kutokana na ukataji Miti wa kutisha unaoendelea kwenye mikoa hii! Kwa sasa haizalishi chakula cha kutosha na kwa uharibifu huu wa mazingira huko mbeleni inaonekana hali itakuwa mbaya zaidi

3. Kanda ya Magharibi hasa Mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi huku Pia yanayoendelea sio mazuri, wahamiaji kutoka kanda ya ziwa na nchi za jirani wanaingia kwa kasi kwenye mikoa hii na kukata Miti kwa Kiwango cha kutisha. Mikoa ya Rukwa na Katavi imeanza kupata mvua kwa Kiwango kisichoridhisha na hii ni kutokana na ukataji mkubwa wa Miti unaofanyika kwenye mikoa hii.

Kwa sasa Tanzania inategemea mikoa hii pamoja na RUVUMA, Mbeya, Iringa na Njombe bila kusahau morogoro ila kwa hali inavyokwenda, huko mbele inaonekana ukataji huu wa kutisha wa miti kwenye mikoa yote hii, utapelekea nchi kupata mvua kwa Kiwango cha chini hivyo kupungua kwa uzalishaji wa chakula na kuanza kutegemea chakula kutoka nje!

4. Kanda ya Ziwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu bila kusahau Geita, huku ndo hakufai pia! Watu wa mikoa hii wameharibu sana mikoa yao kwa kukata Miti hivyo kupelekea kutokupata kwa mvua ya kutosha na kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha!

Watu wa mikoa hii sasa wanahamia mikoa ya Tabora, Rukwa , Katavi na Singida na wanachokifanya kule ndo walichofanya kwenye mikoa yao jambo lililopelekea kukubwa na ukame na kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha. Ukienda katavi leo wanaingia katikati ya misitu ikiwemo hifadhi na wanakata Miti na kuanzisha mashamba! Wanafanya hivi huku wakitegemea serikali mtarasimisha hayo maeneo na kuwapa kuendelea na makazi! Wanaiweka nchi kuwa na hatari ya kuwa jangwa katika siku chache zijazo

5. Kanda ya Mashariki- Hasa Mkoa wa Morogoro na Pwani ambako wamasai baada ya kusababisha ukame maeneo ya ARUSHA sasa wamehamia kwa kasi kwenye mikoa hii ambako wanachofanya ni kukata Miti , kuharibu uoto wa asili kutokana na wingi wa MIFUGO yao. Hili linapelekea ukame kukua na kuinyemelea kwa kasi Kubwa mikoa hii ya PWANI na Morogoro.
Mikoa hii ndo inanywesha maji wakazi wa Mkoa wa Dar kutokana na kuwa vyanzo vikubwa kwa maji ya mto wami na Ruvu. Kuna hatari Jiji la Dar kukosa kabisa maji siku chache zijazo kutokana na hali ya mazingira hasa ukataji wa miti kwenye mikoa hii utakaopelekea ukosefu wa mvua na ukame

Ushauri wangu
1. Naomba Serikali yako iache kurasimisha maeneo yanayovamiwa na watu hasa mapori na hifadhi. Tanzania haijaisha maeneo. Watu warudishwe kwenye maeneo yao ya asili na waelekezwe namna ya kuishi huko kwa kupanda Miti na kutunza mazingira na kufanya uzalishaji huko. Tabia hii ya kuacha watu wanavamia maeneo alafu badae wanapewa uhalali wa kuishi huko ndo inazidi kuifanya nchi yetu kuzidi kuwa jangwa na badae tutashindwa hata kuzalisha chakula cha kutosha Kwa kukosa mvua!

Kwenye hili kama Jamii ni ya wafugaji, wapewe teknolojia na wafundishwe kufuga wanyama wachache kibiashara. Suala la mtu kumiliki ng’ombe 5000 wakati hana teknolojia ya kuwalisha bila kuharibu mazingira limepitwa na wakati! Watu wafuge kwa teknolojia Bora ya kisasa tena kibiashara.

Ni vizuri serikali ikaanza kuweka Sheria ya kudhibiti idadi ya mifugo ya aina ya teknolojia ya ufugaji ili kuokoa mazingira yetu na uhai wetu

2. Wape meno Wakala wa Misitu wasimamiw Kweli Sheria zetu. Kwa hili napenda kukiri kuwa TFS wako vizuri ila wanarudishwa nyuma na wanasiasa. Kwenye hili Naomba wape meno TFS wasimamie misitu yote iliyovamiwa na wawaondoe watu wote waliovamia maeneo hayo!

TFS pia wapewe mandate ya kuhakikisha mapori ya misitu iliyoharibiwa vinarudishwa katika hali yake ya ubora! Hili litaokoa maeneo yetu ya kufanya nchi iendelee kupata mvua Nzuri na kuendeleza kilimo.

3. Kupitia vijana wa JKT na TFS pia , naomba uanzishe kampeni kabambe ya upandaji Miti. Ethiopia waliofanya hivi miaka ya 90-2000 na sasa wamefanikiwa sana na upandaji ule wa Miti uliwawezesha kupata mvua za kutosha na sasa wameweza zalisha chakula kingi.

Naomba uanzishe hili Tanzania na kipaumbele iwe mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, kanda ya Ziwa bila kusahau Songwe na Morogoro, huku ipandwe Miti mingi ikiwezekana hata Miti Bil 1 nchi nzima na ifanyiwe kampeni ya kuitunza na kuilinda. Hapa nafikiri tutafanikiwa sana!

Naomba kuishia hapa!
 
Jf kama itakuwa hivi litakuwa jambo la kupendeza sana......mtu anatoa tatizo na kupendekeza njia za kulitatua. Sana sana!

Mtoa mada umeongea kitu cha umuhimu kwelikweli. Hali ya kimazingira sasa ni mbaya mno. Nasali hapa kiongozi uliyemtaja umfikie ujumbe huu.......ubarikiwe sana!!!
 
Ushauri mzuri ni mno tatzo thread km hizi wasomaji huwa wachache .

Mimi ninapotembea au kusafiri hakuna kitu kinanivutia km kuona mistu na uoto mzuri wa asili. Pia huwa nakerwa sana ninopoona jangwa na uharibifu wa mazingira.
Kabisa, siku hizi watu wamekuwa ni wa kujadili mambo mepesi mepesi tu. Inasikitisha sana
 
Ushauri mzuri ni mno tatzo thread km hizi wasomaji huwa wachache .

Mimi ninapotembea au kusafiri hakuna kitu kinanivutia km kuona mistu na uoto mzuri wa asili. Pia huwa nakerwa sana ninopoona jangwa na uharibifu wa mazingira.
Ukiweza siku pita Dar- Mwanza! Hali ya Singida, Dodoma, Tabora na Shinyanga ni ya kukutoa machozi
 
Jf kama itakuwa hivi litakuwa jambo la kupendeza sana......mtu anatoa tatizo na kupendekeza njia za kulitatua. Sana sana!

Mtoa mada umeongea kitu cha umuhimu kwelikweli. Hali ya kimazingira sasa ni mbaya mno. Nasali hapa kiongozi uliyemtaja umfikie ujumbe huu.......ubarikiwe sana!!!
JF kiasili ni Home of Great Thinkers. Dhana hii ikizingatiwa Viongozi wanaweza itumia Kama chungu cha fikra endelevu kweli
 
Hili jambo linawezekana kama serikali ikiweka mkakati wa uhamasisha kuanzia ngazi ya jamii. Mfano iweke utataratibu wa Kila mwanafunzi kuanzia primary, secondary, vyuo vya kati hadi vyuo vikuuu.

Pia Kila raia, wafanyakazi wote kuanzia sekta binafisi na serikali wahakikishe kupanda at least mti 10 Kila mwaka. Maana suara la mazingira ni suara mtambuka
 
Kwa kweli mleta mada hili ni sio Ombi tu naona liwe rasmi tu
Kuhusu Mkoa wa Tabora daa miti imekatwa sana
Nakumbuka Aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri huyo jamaa alikuwa smart sana alilazimisha miti ipandwe sana katika mkoa huo

Ila tatizo kila anaekuja anakuja na lake ingekuwa kwenye moja ya kazi zao Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuhakikisha wanasimamia upandaji wa miti na kuhakikisha wanaochoma moto wakamatwe na kufikishwa mahakamani, na pia hao wahamiaji wa kisukuma na mifugo yao ambao wana vita na Miti
 
Kwa kweli mleta mada hili ni sio Ombi tu naona liwe rasmi tu
Kuhusu Mkoa wa Tabora daa miti imekatwa sana....
Tabora inasikitisha ndugu! Ukipita barabara ya itigi ndo hapafai, njia ya kigoma hapafai, njia ya Katavi hapafai, kuelekea Uyui na Nzega napo hapafai!

Hii nchi tusipoamka sasa tunaweza jikuta tunaanza kuagiza chakula nje kwa sisi kushindwa kuzalisha chakula kutokan ana ukosefu wa mvua
 
Hili jambo linawezekana kama serikali ikiweka mkakati wa uhamasisha kuanzia ngazi ya jamii. Mfano iweke utataratibu wa Kila mwanafunzi kuanzia primary, secondary, vyuo vya kati hadi vyuo vikuuu. Pia Kila raia, wafanyakazi wote kuanzia sekta binafisi na serikali wahakikishe kupanda at least mti 10 Kila mwaka. Maana suara la mazingira ni suara mtambuka
Kweli kabisa! Uzuri wa jambo hili halihitaji gharama! Ni uhamasishaji tu
 
Thread kama hizi huwa hazisomwi. Watu wanataka thread za kutupia picha za warembo, vituko mitandaoni, kubeti au siasa. Bahati mbaya waandishi wa thread kama hizi hapa Jamiiforums hawawezi wekwa kwenye lile kapu la story for change (Stories of change???)
 
Tabora inasikitisha ndugu! Ukipita barabara ya itigi ndo hapafai, njia ya kigoma hapafai, njia ya Katavi hapafai, kuelekea Uyui na Nzega napo hapafai! Hii nchi tusipoamka sasa tunaweza jikuta tunaanza kuagiza chakula nje kwa sisi kushindwa kuzalisha chakula kutokan ana ukosefu wa mvua

Mkuu unaweza kulia kama unapenda nature

Watu hawana elimu kabisa na serikali haiwekezi katika elimu hii ya kutunza ardhi yetu

Hapa naangalia Earthshot Price 2021
Ambapo five inspiring projects wanapewa £1m each

Ukipata hii programme angalia hata kenya wamo kwenye mchakato

Tupiganie sana na mijadala iwe mingi ili tusikike mpaka kwa Rais na ajue global warming ipo
Mkoa wa Tabora najua huwa lina joto ila joto la mwaka huu limezidi sana
 
Back
Top Bottom