Serikali yatoa Tsh. Bilioni 66 Kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,759
143,210
Serikali ya Tanzania imetoa Jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Fedha hizo zimegawanywa Kwenye mikoa Yote iliyoathirika

---
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa Bilioni 66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.

Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa TANROADS mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha kadhia zilizozikumbumba barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Akizungumza Jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mha. Mohamed Besta amesema kuwa kutokana na udharula huo tayari Rais Samia ameidhinisha fedha za matengenezo ya miundiombinu hiyo ambazo zimeshapelekwa katika Mikoa yote Nchini.

Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote nchini na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharula vilivyopo TANROADS pamoja na ofisi za mikoa.

Ameongeza kuwa kutokana na tathimini iliyofanyika mpaka sasa zaidi ya Shilingi Bilioni 250 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Barabara kuu za Mikoa yote Nchini ambazo zimeharibika vibaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo kama Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu kusini mwa Nchi mvua zimeendelea kunyesha tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na sasa unaelekea mwezi wa saba na mvua bado zinaendelea kunyesha.

“Tunamshukuru Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ametupatia shilingi bilioni 66 ambazo tumezisambaza katika Mikoa yote ambapo mameneja wote wa Mikoa wamepewa kutokana na hali ya dharura ya Mkoa husika’’ ameeleza.

Chanzo: Clouds
 
Kapesa kadogo sana hako ukilinganisha na ubovu wa barabara.

Hiyo hela hata kwa jimbo la ukonga tu haitoshi
 
Rais wa JMT Dr Samia ametoa Jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Fedha hizo zimegawanywa Kwenye mikoa Yote iliyoathirika

Source: Clouds TV
Sio katoa, sema ameidhinisha!
Watanzania lazima tuamke, hizo ni kodi za wananchi na huenda yeye hakatwi hata senti.
 
Rais wa JMT Dr Samia ametoa Jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Fedha hizo zimegawanywa Kwenye mikoa Yote iliyoathirika

Source: Clouds TV
Hivi ni mimi au lugha imekwenda upande?! Ni Samia ametoa Jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua au Serikali imetoa jumla ya shilling billion 66 Ili kurekebisha Miundombinu iliyoharibiwa na mvua? Samia ametoaje bilioni 66?!
 
Usimkatalie mkuu. Huenda ametoa hela zake mwenyewe. Labda alilima ufuta sasa ameuza na amezitoa mfukoni mwake. Lakini kama ni hizi zinazokusanywa na TRA na vyanzo vingine vya serikali inabidi watubu hii dhambi maana wamesema raisi ametoa kumbe hajatoa raisi ni serikali ndiyo iliyotoa.
Samia anatoa wapi shilling billion 66 bhana?!! Ebu tuwe na umakini bhana?!
 
Back
Top Bottom