Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,842
- 46,603
Dr. Anthony Fauci alikuwa ni Mkurugenzi wa taasisi ya kitaifa ya Marekani ya magonjwa ya mzio na kuambukiza(NIAID) kwa takribani miaka 20 na jina kubwa katika masuala ya Afya Marekani kama alivyo Janabi hapa Tanzania.
Wakati wa mlipuko wa COVID anakumbukwa zaidi kwa jinsi alivyokuwa akitoa elimu dhidi ya conspiracies na myths nyingi zilizohusiana na COVID-19 na chanjo zake baadaye.
Fauci alichukiwa sana na kudhihakiwa na wapinga chanjo(anti-vaxxers) pamoja na wapenda story za nadharia za njama(conspiracists) kwa sababu kila mara alikuwa akienda kinyume nao na matamanio yao. Ilifikia hadi mahali usalama wake ukatishiwa ikabidi apewe ulinzi wa ziada.
Mashambulizi na dhihaka dhidi ya nguli Profesa Janabi kwa elimu anayoitoa kwa umma ni kama vinafuata mkondo wa Dr. Fauci.