Profesa Janabi: Ogopa sana vitu vitamu vitamu

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,697
12,438
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema utumiaji wa sukari kupita kiasi haufai kwa afya ya mwanadamu.

“Ukinywa glass moja asubuhi machungwa matano, mchana matano na jioni matano maana yake kwa mwezi ni machungwa 450, unaharibu afya yako, ogopa zaidi vitu vitamu tamu, unavyozungumzia sukari sio sukari tu bali ni vitu vitamutamu. Pale Muhimbili tunao watoto wa miaka tisa wana kisukari.” amesema Profesa Janabi

Amasema hayo mkoani Mwanza wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa Mafunzo wa 108 wa watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Washiriki wa mkutano huo ni watumishi kutoka taasisi mbalimbali za serikali.
 
Kufa ni constant, haijalishi unakula nini.

Kikubwa, baada ya kula chochote, mwili unaushughulisha kikamilifu kimazoezi, kazi za mikono n.k?.

Yaani mtu ashinde shambani kwenye jua kali kutwa nzima kisha "propesa" wa kisiasa aje aseme usile chochote kitamu?.

Anataka ufe njaa mwanakijiji mwenzangu baada kutoka shambani.

Hiyo kauli inawahusu nyie mnaoshinda kwenye viyoyozi kutwa nzima mlio na minofu ya kizembe huko kwenu mijini.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema utumiaji wa sukari kupita kiasi haufai kwa afya ya mwanadamu.

“Ukinywa glass moja asubuhi machungwa matano, mchana matano na jioni matano maana yake kwa mwezi ni machungwa 450, unaharibu afya yako, ogopa zaidi vitu vitamu tamu, unavyozungumzia sukari sio sukari tu bali ni vitu vitamutamu. Pale Muhimbili tunao watoto wa miaka tisa wana kisukari.” amesema Profesa Janabi

Amasema hayo mkoani Mwanza wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa Mafunzo wa 108 wa watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Washiriki wa mkutano huo ni watumishi kutoka taasisi mbalimbali za serikali.
Huyu jamaa anataka tule nini sasa?....hao watoto wa miaka 9 wenye kisukari na wao walikuwa wanakula sana vitu vitamu au wamezaliwa na huo ugonjwa?
 
Back
Top Bottom