Odinga ataka kifo cha General Ogolla kichunguzwe haraka kwani Wananchi Wana hofu ameuawa!

Kheri kufa kwenye helicopter kuliko kwenye kiroba kilicho fungwa jiwe ..teh teh
Kweli kabisa. Ukifa kwenye kiroba ukatupwa baharini uliwe na samaki inauma sana. Bora kwenye helikopta ndugu wataokota mabaki ya mwili wazike.
 
Mwanasiasa mkongwe na maarufu nchini Kenya, Oburu Odinga, amesema bila kumumunya maneno kuwa mkuu wa majeshi wa Kenya, Jenerali Francis Ogolla ameuawa na serikali ya William Ruto. Mwanasiasa huyo ametamka maneno hayo hadharani bila kuficha wakati wa mazishi ya Ogolla yaliyofanyika nyumbani kwake katika kaunti ya Siaya, huku akishangiliwa na mamia ya waombolezaji waliohudhuria mazishi hayo.

Mbali na kuuliwa Ogolla, amedai wanasiasa wengi kwenye jamii ya waluo akina Tom Mboya na Robert Ouko waliuawa kwa namna hiyo hiyo. Amesema wakati sasa umefika uchunguzi ufanyike bila kificho ili kujua ukweli kwani hii sasa imegeuka kuwa staili ya serikali kuwaua watu katika nchi hiyo. Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, hebu msikilize wewe mwenyewe kwenye video hii hapo chini.

View attachment 2970428
MOANI YANGU
Tungekuwa na watu angalau watano tu wenye ujasiri kama Odinga hapa Tanzania, mauaji ya kipuuzi yanaoendelea hapa nchini yangekoma mara moja. Kama ingekuwa inawezekana tungemuazima Odinga hata kwa siku moja tu aje atusaidie kupaza sauti kuhusu ndugu zetu wanaouliwa kama panya huku watu wamekaa kimya. Inauma sana.

Wapi amesema serikali ndiyo imemuua?
 
Oburu Odinga si Raila Odinga ni kaka ww Raila!
 
Back
Top Bottom