Odinga ataka kifo cha General Ogolla kichunguzwe haraka kwani Wananchi Wana hofu ameuawa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,158
142,252
1713779906069.png
Baada ya mbunge wa Kisesa mh Luhaga Mpina kuwasha moto bungeni kwamba kifo Cha Magufuli kichunguzwe, rafiki wa Magufuli naye huko Kenya amewasha moto mbele ya Rais Ruto akitaka kifo Cha CDF Ogola kichunguzwe

Odinga amesema Wananchi wanahisi Uchaguzi mkuu uliopita ndio Sababu ya General Ogala kuuwawa.

Pia soma: TANZIA - Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (KDF) Jenerali Francis Ogolla afariki katika ajali ya Helikopta ya Jeshi
---
Opposition leader Raila Odinga has called for speedy probe into the cause of the chopper crash which killed Chief of Defence Forces Francis Ogolla.

Raila in a statement on Friday urged the government to expedite the probe into the cause of the accident.
Raila raised concerns about the state of helicopters and other equipment being used by the security officers.

"Many near death encounters have occurred with the security aircrafts. We may never know what exactly brought down the helicopter in which the general died," Raila said.

"It is our prayer that this tragedy may mark the beginning of a serious relook into our security equipment, especially the aircrafts with a view to undertaking a complete overhaul and modernisation of the equipment. That was the General's vision," he added.

According to Raila, the government owes Kenyans a thorough, professional and transparent investigations into the deaths.

He said "only such an investigation will put the family and the whole nation at peace".

This is even as Raila led a section of Azimio leaders to pay a visit family of Ogolla at his Ng'iya home in Siaya to express his condolences and support.

Raila was accompanied by several other Azimio leaders who included Martha Karua (Narc-K) Kalonzo Musyoka (Wiper), Wycliffe Oparanya, Mwangi Wa Iria, James Orengo among elected leaders.

Their visit was seen as a gesture of solidarity and respect for the life and legacy of the Ogolla.

"General Ogolla devoted his life to serving this country, from the day he graduated. through multiple tours of duty, and ultimately as the top soldier in KDF," he said in a statement.

Ogolla met his death Thursday afternoon alongside nine other military officers in a chopper crash in Marakwet East.

He is set to be laid rest on April 21.

Credit: Citizen TV

Mlale Unono 😄😄🔥
 
Nyani kumchunguza ngedere.

Kila nafsi itaonja mauti. Wauwawe kisa nini? Move on.
 
Yes, kifo cha huyu aliyekuwa Mkuu wa Majeshi (CDF) wa Kenya Bw. Ogora kina utata mkubwa Sana ukichunguza kwa umakini. Uchunguzi huru unapaswa kufanyika ili kuondokana na utata uliopo.
 
Uongo mtupu Odinga alitoa kauli hii mapema ukizingatia ndani ya mwaka 1 kumetokea ajali 5 tofauti za chopper za jeshi na pia kauli tata ya Ruto kuhusu late CDF kwenda kutaka kupindua matokeo yake kule Bomas 2022 na matukio ya nyuma hasa kifo cha Professor George Saitoti 2012 kwa ajali ya chopper pia ambaye ndio alitarajiwa kugombea urais 2013.

Hivyo hapo umedanganya umma fact checking ya JF ilienda wapi??
 
Nyani kumchunguza ngedere.

Kila nafsi itaonja mauti. Wauwawe kisa nini? Move on.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Urais na Wabunge uliopita huko Kenya, CDF Ogora alienda ktk Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi walikokuwa wakihesabu kura za Urais. Alienda huko kwa lengo la kutaka Kupindua Matokeo ya Urais yaliyompa ushindi Rais wa sasa William Ruto ili atangazwe mshindi Raila Odinga, mtu wa kabila lake la Wajaluo.
 
Uongo mtupu Odinga alitoa kauli hii mapema ukizingatia ndani ya mwaka 1 kumetokea ajali 5 tofauti za chopper za jeshi na pia kauli tata ya Ruto kuhusu late CDF kwenda kutaka kupindua matokeo yake kule Bomas 2022 na matukio ya nyuma hasa kifo cha Professor George Saitoti 2012 kwa ajali ya chopper pia ambaye ndio alitarajiwa kugombea urais 2013.

Hivyo hapo umedanganya umma fact checking ya JF ilienda wapi??
Unaweza kuona kwamba hizo ajali za helicopter za Jeshi zilizotokea hapo kabla nazo zilikuwa za kutengenezwa (the staged accidents ) zikiwa kama ni maandalizi ya awali ya kuwaandaa Wananchi kisaikolojia ili wasishituke wakati wauaji watakapotekeleza ajali ya kumuua mlengwa wao Mkuu (the main target ) ambaye ni Mkuu wa Majeshi (CDF).

Hizo ajali Zilizotokea mwanzo ilikuwa kama 'Shadowing Conspiracy/Propaganda)
 
Statement ya RAO iko clear tu chopper nyingi za KDF zilikua na mechanical faults nyingi from the word go.

Mpaka ajali iliyomuua CDF ndio yote yameibuka.

Bado naona ipo haja ya kuchunguza hayo yote haki itendeke isiwepo pande itakayoonewa.
 
Unaweza kuona kwamba hizo ajali za helicopter za Jeshi zilizotokea hapo kabla nazo zilikuwa za kutengenezwa (the staged accidents ) zikiwa kama ni maandalizi ya awali ya kuwaandaa Wananchi kisaikolojia ili wasishituke wakati wauaji watakapotekeleza ajali ya kumuua mlengwa wao Mkuu (the main target ) ambaye ni Mkuu wa Majeshi (CDF).

Hizo ajali Zilizotokea mwanzo ilikuwa kama 'Shadowing Conspiracy/Propaganda)

Kenya ajali za chopper zinatokea toka early 2000's kote walikua wanafanya maandalizi ya kumuua CDF wa mwaka huu?
 
Katika Uchaguzi Mkuu wa Urais na Wabunge uliopita huko Kenya, CDF Ogora alienda ktk Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi walikokuwa wakihesabu kura za Urais. Alienda huko kwa lengo la kutaka Kupindua Matokeo ya Urais yaliyompa ushindi Rais wa sasa William Ruto ili atangazwe mshindi Raila Odinga, mtu wa kabila lake la Wajaluo.

Far fetched.
 
Mwanasiasa mkongwe na maarufu nchini Kenya, Oburu Odinga, amesema bila kumumunya maneno kuwa mkuu wa majeshi wa Kenya, Jenerali Francis Ogolla ameuawa na serikali ya William Ruto. Mwanasiasa huyo ametamka maneno hayo hadharani bila kuficha wakati wa mazishi ya Ogolla yaliyofanyika nyumbani kwake katika kaunti ya Siaya, huku akishangiliwa na mamia ya waombolezaji waliohudhuria mazishi hayo.

Mbali na kuuliwa Ogolla, amedai wanasiasa wengi kwenye jamii ya waluo akina Tom Mboya na Robert Ouko waliuawa kwa namna hiyo hiyo. Amesema wakati sasa umefika uchunguzi ufanyike bila kificho ili kujua ukweli kwani hii sasa imegeuka kuwa staili ya serikali kuwaua watu katika nchi hiyo. Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, hebu msikilize wewe mwenyewe kwenye video hii hapo chini.

MOANI YANGU
Tungekuwa na watu angalau watano tu wenye ujasiri kama Odinga hapa Tanzania, mauaji ya kipuuzi yanaoendelea hapa nchini yangekoma mara moja. Kama ingekuwa inawezekana tungemuazima Odinga hata kwa siku moja tu aje atusaidie kupaza sauti kuhusu ndugu zetu wanaouliwa kama panya huku watu wamekaa kimya. Inauma sana.
 
Back
Top Bottom