SoC04 Ninaifanyia nini nchi yangu?

Tanzania Tuitakayo competition threads

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,230
2,089
"Ask not what your country can do for you,but what you can do for your country " yaani
"Usiulize nchi yako inaweza kukufanyia nini,ila jiulize wewe unaweza kuifanyia nini nchi yako"

Hiko ni kifungu cha maneno maarufu ambacho kilitamkwa katika hotuba ya John F. Kennedy, kipindi akiapishwa kuwa Rais wa 35 wa Marekani.

Aya,turudi hapa nchini kwetu Tanzania.Ambapo sehemu ya Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961,mwaka huo huo ambapo JFK alitoa hiyo hotuba yake maarufu. Nchi yetu bado ni maskini, kanakwamba utajiri wa ndugu Elon Musk ni mara tatu ya pato zima la Taifa letu. Kama mtafiti akapita mtaani na maofisini na kuuliza chanzo cha umaskini huu,majibu utakayogewa yanweza yakawa.
  • Serikali inanunua ndege badala ya matrekta .
  • Serikali inalipa wabunge mishahara na marupurupu ya kutosha inayofirisi nchi.
  • Serikali imeruhusu viwanda vife kwa kubinafsisha kila kitu
  • Serikali haijengi barabara
  • Serikali haitoi mikopo kwa wananchi na vijana
  • n.k
Katika majibu yote hayo kuna neno moja ambalo limejirudia, "serikali"
Na mtafiti huyo huyo akauliza nini kifanyike nchi ili nchi yetu iweze kujikwamua katika umaskini nina uhakika majibu yatakuwa.
  • Serikali iwekeze kwenye kilimo
  • Serikali ihakikishe umeme haukatiki
  • Serikali itoe elimu bure mpaka vyuo vikuu.
  • Serikali ihakikishe maji yanapatikana nchi nzima.
  • Serikali ijenge Viwanda vya kutosha
  • Serikali ijenge barabara.
yote yatajikita kwenye neno serikali.
Katika majibu yote atakayogewa mtafiti ,nina uhakika 95% yatakuwa ya kuitupia lawama serikali na wananchi wa kawaida kujitunuku utakatifu.
Wakati ukija katika jamii,utashuhudia yafuatayo
  • Wazazi wana waoza wenyewe mabinti zao wakiwa wadogo
  • Watu Kabla ya kupata ajira tayari wanjiapiza wizi na ubadhilifu Siku wakipata fursa ya kutumikia nchi.
  • Watu wanapenda starehe kuliko kazi.
  • Ubinafsi wa kikabila.
  • Matajiri wanalipia Mashabiki zaidi ya 20,000 kuingia uwanjani na kutazama mechi.
  • Vijana wenye elimu wanakaa mtaani na kula chakula cha Mama yake ,anayejituma kwa kuuza vitafunwa
  • Watu wanajua na kutafiti mengi kuhusu Simba na Yanga kuliko uchumi wao.
  • Ndugu zao wakibaka/lawiti hutaka kuyamaliza kimyakimya.
  • Watu mabingwa wa kutolipa kodi
  • Watu mabingwa wa kuringisha fedha zao mtandaoni.
  • Watu wameajiri watoto wa miaka 10 hadi 16 kama wafanyakazi wa ndani.
Inabidi ifike wakati wananchi wenzangu ifike kipindi tutambue kama ile Tabia tunayoiona serikalini inaakisi tabia ya wananchi wake.kwakuwa hao viongozi waliopo serikalini kabla ya hapo walikuwa ni wananchi kama sisi,hizo tabia wanazitoa kwenye jamii hizi hizi tunazoishi,hapo wa kuskia haibu ni sisi wenyewe.

Kwanini sisi ni wepesi kwenye kudai haki zetu kuliko kwenye kuwajibika...?

Namna ambazo tunaweza kuwajibika na kuleta mabadiliko katika maendeleo chanya ya nchi yetu.
(Kwa wasio na kipato/kipato kikubwa)
  • Kwa wahitimu wa vyuo,Toeni elimu ya bure
-Umesoma udaktari na bado hauja ajiliwa ,hebu ingia mtaani na elimisha watu juu magonjwa yanayosumbua mitaani.
-Mhitimu wa Uchumi, ingia mtaani na elimisha watu juu ya namna bora za kujitanua kibiashara katika Masoko ya nje.
-Mhitimu wa sheria,saidia wanamtaa wenzako kwenye kujua haki zao za msingi wa kisheria.
-Mhitimu wa Uhanidisi mekanika, ingia mtaani na usaidia wahunzi namna bora ya kuboresha bidhaa zao.
-Umesoma Matangazo,saidia watu wajue namna bora za kujitangaza kibiashara

*Kila mhitimu wa fani ana namna ya kuisadia jamii ,Amini kuna mtu ataona juhudi zako na atakufungulia njia ya mafanikio.
  • Ushiriki kwenye uchaguzi
-Jitahidi kushiriki kwenye uchaguzi .
-Usisusie ushiriki wako katika uchaguzi kwakuwa atakayechaguliwa ndiye atakayepewa dhamana ya kupitisha sheria ya kodi.
-Lakini kutoendekeza rushwa katika mapendekezo ya viongozi watakao gombea.
  • Kuhakikisha shule ya eneo la kata yako ina matundu ya vyoo na madawati
Kama sisi wananchi maskin tunaweza jenga makanisa na michango ya mia mia, tunashindwaje kujenga vyoo kwa ajili ya shule zetu.

(Kwa wenye kipato kikubwa)
-Tanzania ina Mabilionea zaidi ya 435 na mamilionea zaidi ya 1000.Na kuna wengi ambao wanazidi kutajirika
  • Fadhili masomo ya wanafunzi Maskini
-Vyuo vya Havard,Yale na MIT ni wanufaika wakubwa wa ufadhili wa matajiri wa kimarekani.
-basi nawasihi matajiri wa nchi hii, jitokezeni kusaidia wanafunzi hao.
-Kuna mamia ya wanafunzi wanashindwa endelea na elimu ya vyuo kisa kukosa ada.
-Kwa mtu mwenye billioni 50,ukachangia millioni 50 katika ufadhili, jua kuna vijana 10+ ambao watapata elimu kisa wewe,hao lazima watakuja kukukumbuka maisha yao yote.

  • Chimba Kisima
Mikoa yote ndani ya nchi hii,shida ya maji bado ni kubwa sana.
Chagua mkoa wowote nchini hata ukiwa mkoa wako wa asili, nenda na uchimbe walau Kisima kimoja na uhimize wenzako.
  • Changia vifaa Tiba
Kuna uhitaji mkubwa sana wa vifaa tiba mahospitalini katika hii nchi, jitolee.
Funga safari tembelea eneo husika na utoe msaada.
(Kwa wote)
  • Tuitangaze vyema nchi yetu
Kila inapotokea fursa ya kuitangaza Tanzania, tuitumie hiyo fursa.na tuitangaze vyema.
Sisi ndiyo tuwe mabingwa wa kununua bidha zinazotengenezwa nchini.
Sisi ndiyo tuwe wawekezaji wa kwanza ndani ya hii nchi
Sisi ndiyo tuwe wa kuweka bendera yetu katika kila kitu na kila mahala.
  • Tutunze Mazingira ya nchi yetu
Kwanini watu wanatupa taka mtaroni na mitoni, kwanini twajenga kwenye njia za maji,Kwanini twapitisha mifugo kwenye vyanzo hivyo.
  • Tuasili watoto yatima
Tujijengee utamaduni wa kuasili watoto yatima,kuna wengi hawana uwezo wa kuzaa ama anahangaika hapo, kwanini usiasili mtoto?
  • Tusaidiane kwenye fursa za kazi na biashara
Mpe mtu fursa ya kazi na biashara bila hata kuendekeza kupewa chochote kitu. Pia tusiweke ukabila ama undugu kwenye fursa hizo.

Niliyotaja hapo juu ni machache kati ya mengi ambayo kila mtu anaweza kuifanyia nchi yake.Tabia zetu za sasa ndizo zitakazoweka amua ya urithi vizazi vyetu utapata.

Kwani hata katika hizo nchi zilizoendelea,ugunduzi na vumbuzi nyingi zilizoleta maendeleo, zilifanywa na watu binafsi ndipo kisha serikali ikaingia kati baada ya kuona faida.

Tusikae na kusubiri wazungu na wahindi ndiyo waje kutusaidia kama Sisi wenyewe bado hatutaki kujisaidia kwani maendeleo ya nchi yetu yapo mikononi mwetu

Kwa kila aliyesoma hili andiko,akae na kisha kujiuliza "Ninaifanyia nini nchi yangu..." na swali hilo pia ukitoka nenda umuulize jirani yako.
 
Nchi yetu bado ni maskini, kanakwamba utajiri wa ndugu Elon Musk ni mara tatu ya pato zima la Taifa letu
😆😆😆 daaaah! Ivi ni kweli!?

Inabidi ifike wakati wananchi wenzangu ifike kipindi tutambue kama ile Tabia tunayoiona serikalini inaakisi tabia ya wananchi wake.kwakuwa hao viongozi waliopo serikalini kabla ya hapo walikuwa ni wananchi kama sisi,hizo tabia wanazitoa kwenye jamii hizi hizi tunazoishi,hapo wa kuskia haibu ni sisi wenyewe.

Kwanini sisi ni wepesi kwenye kudai haki zetu kuliko kwenye kuwajibika...?
Tunasema wewe umepiga penyewe kabisa. Nakubaliana na wewe kwamna viongozi ni wawakilishi wa wananchi. Wawakilishi. Kwa hiyo serikali ni watu na watu wenyewe ndio sisi hawa hawa. Unalikumbusha jambo la msingi sana. UWAJIBIKAJI.

Kila mhitimu wa fani ana namna ya kuisadia jamii ,Amini kuna mtu ataona juhudi zako na atakufungulia njia ya mafanikio.
Sawa sawa. Na ukifanya kitu kifanye kisomi ilo wengine waige kwa kuona.
Tujijengee utamaduni wa kuasili watoto yatima,kuna wengi hawana uwezo wa kuzaa ama anahangaika hapo, kwanini usiasili mtoto
Eti bwana. Lakini nashauri mtu anaweza kiasili kichanga wale wa wamama wasiojulikana wanapojifungua na kuwakimbia watoto au kupoteza maisha. Kanakuwa katoto kako kabisa mnaweza hadi kufanana maana tabia zinafananisha haraka kuliko hata gene. E eeh, mtu akianza kunywa pombe kali atafanana na mlevi fasta hata kama baba yake wa asili hana hulka hiyo.


Kwa kila aliyesoma hili andiko,akae na kisha kujiuliza "Ninaifanyia nini nchi yangu..." na swali hilo pia ukitoka nenda umuulize jirani yako
Na iwe hivi👏👏✔
 
😆😆😆 daaaah! Ivi ni kweli!?


Tunasema wewe umepiga penyewe kabisa. Nakubaliana na wewe kwamna viongozi ni wawakilishi wa wananchi. Wawakilishi. Kwa hiyo serikali ni watu na watu wenyewe ndio sisi hawa hawa. Unalikumbusha jambo la msingi sana. UWAJIBIKAJI.


Sawa sawa. Na ukifanya kitu kifanye kisomi ilo wengine waige kwa kuona.

Eti bwana. Lakini nashauri mtu anaweza kiasili kichanga wale wa wamama wasiojulikana wanapojifungua na kuwakimbia watoto au kupoteza maisha. Kanakuwa katoto kako kabisa mnaweza hadi kufanana maana tabia zinafananisha haraka kuliko hata gene. E eeh, mtu akianza kunywa pombe kali atafanana na mlevi fasta hata kama baba yake wa asili hana hulka hiyo.



Na iwe hivi👏👏✔
Yeah,
Kama kila akiwajibika kwa namna moja au nyingine,Hii nchi itafika mbali kimaendeleo na siyo kukesha kunyooshea kidole serikali.
 
Back
Top Bottom