SoC04 Nchi inahitaji uongozi shirikishi ili kuondoa malalamiko, na chuki dhidi ya Serikali

Tanzania Tuitakayo competition threads

JOHN MAXWELL

Member
Feb 26, 2024
33
67
NCHI INAHITAJI UONGOZI SHIRIKISHI ILI KUONDOA MALALAMIKO, NA CHUKI DHIDI YA SERIKALI.

Utangulizi:
"Tanzania tuitakayo"


Taifa letu TANZANIA ni Taifa ambalo linahitaji uongozi shirikishi ,kuanzia ngazi ya Taifa ,mkoa ,wilaya hadi mtaa, kijiji na kitongoji, ili kuifikia Tanzania tuitakayo.

Kama Taifa tumekuwa tukipitia nyakati ambazo kuna watu wanalaumu, kukosoa ,kulalamika kuhusu serikali iliyopo madarakani , hii inazuia uwajibikaji miongoni mwa wananchi , kwa kusababisha wananchi kushindwa kujua kipi wafanye wajiletee maendeleo na kipi serikali ifanye ili kuleta maendeleo.

Ni kweli serikali bora na kiongozi bora ni yule anayekubali kukoselewa ila wananchi bora ni wale ambao watawakosoa viongozi na serikali yao baada ya wao kutimiza wajibu wao kama wananchi.

Hivyo Kitendo cha wananchi wengi kulalamika na kubeba chuki kwa kila uongozi unaoingia madarakani, husababishwa na serikali kutowaelimisha wanachi vyakutosha kuhusu kipi serikali inabidi kufanya na kipi wananchi wanabidi kufanya wao kama wao ili kujiletea maendeleo na kuliletea Taifa letu maendeleo. Hii hupelekea wanachi wengi (ku -decline responsibility Kwa kuamini wao hawausiki katika maendeleo .

Ili kuifikia Tanzania tuitakayo lazima uongozi wa juu (serikali) uwe na mawasiliano na wananchi ili kuondoa chuki, lawama, malalamiko ambayo hayana msingi ili wanachi waweze kuwajibika katika maeneo yao.

Natoa mapendekezo matano (05) ambayo serikali inabidi kuwekeza ili kuondoa malalamiko, chuki ,hasira na kuleta uwajibikaji kwa wananchi pamoja na serikali yenyewe ili nchi kujipatia maendeleo Pamoja na Maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na kudumisha Amani.

(1) Serikali- iandae mpango kazi ambao utamuezesha kila mwanachi kuwa na taarifa sahihi za kipi serikali inabidi kufanya katika eneo lake alilopo - mfano serikali inaweza kuhakikisha inatoa taarifa kwa uwazi na kuonesha kipi kitafanyika kwa muda fulani hii inaweza kufanywa kwa kuchapisha maandiko kupitia mitandao ya kijamii , au tovuti za serikali pamoja na kuziweka hizo taarifa katika ngazi za chini za serikali.

(2) Kutoa Elimu kwa umma kuhusu dhana nzima ya maendeleo- ili tutimize lengo la kuleta maendeleo hatuwezi kujitenga na sakata la kutoa Elimu kwa umma katika nchi yetu imekuwa ikikumbwa na umasikini ambao husababishwa na wananchi kutopata elimu ya kujitambua kuhusu maana ya maendeleo na kusubiri serikali kuwafanyia kila kitu . endapo serikali itajikita kuwapa watu Elimu kuhusu uongozi na majukumu ya serikali ili kila mtu au mwananchi ajitambue na kutambua sehemu au maeneo ambayo serikali itashughulikia na maeneo ambayo mtu binafsi atayashughulikia yeye kama yeye. katika kutoa elimu kwa umma hapa serikali inaweza kutumia vyombo vya habari kama Television , radio , magazeti , pamoja na kuwatumia wajumbe maalumu wenye uwezo wa kutoa elimu kwa umma. Elimu inaweza kujikita katika (Personal growth, self-development, mentorship programmes , na n.k.

(3) Watu Kufundishwa dhana nzima ya uzalendo , Ili nchi yetu iwe na maendeleo tunahitaji uzalendo kwa wananchi na uzalendo huwa unajengwa ndani ya mioyo ya WATU kwa kuwafundisha wananchi falsafa mbalimbali ikiwemo kujua kuwa nchi huwa haipiti ila viongozi wabaya wanapita ,hivyo hata ikitokea tatizo lolote ndani ya serikali wasianze kuichukia nchi ila waendelee kuamini kuwa viongozi wabaya hupita ila nchi huwa haipiti , hivyo ili kuifikia Tanzania tuitakayo serikali inabidi kujiikita katika kutoa elimu kwa wananchi kuweka uzalendo mbele .

(4) Kuwapa wanachi Elimu ya uraia ili waweze kushiriki kikamilifu katika maswala ya siasa, nchi yetu imekuwa na kundi kubwa la WATU ambalo halijishughulishi na siasa.na mwisho kuishia kulaumu serikali kwa maamuzi ambayo serikali inachukua na baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kuwa siasa haiwaathiri moja kwa moja , jambo ambalo limepelekea kuwepo kwa kundi kubwa la watu ambalo halijui majukumu ya viongozi wao ni nini na mwisho kundi hili huishia kuwa na chuki ,kulalamika na kusema kuwa linatengwa , hivyo elimu ya uraia itaondoa malalamiko ,chuki ,hasira na kuongeza uwajibakaji kwa wananchi kwa kutambua kuwa siasa ni sehemu ya MAISHA yetu hivyo inabidi kila mtu kushiriki kikamilifu .

(5) Serikali inabidi kuwaambia wananchi umuhimu wa wao kuanza au kutangulia kisha serikali kufata nyuma- serikali inabidi kuandaa sera na mkakati utakaompa mwanga mwananchi au wananchi kuanza kufanya kazi zao za kujiletea maendeleo na serikali kuwafata nyuma, mfano wananchi wanapoona kuna uhaba wa shule katika eneo lao wanaweza kutoa taarifa kwa uongozi wao wa kijiji au mtaa na wakaanza kujenga miundombinu na kisha serikali ikafataia nyuma. Kuleta walimu, vifaa n.k serikali ambayo wanachi watatangulia itatimiza uwajibikaji kwa kila mwananchi .


Hizi ni faida tano (05) zitakazopatikana baada ya kuwa na uongozi shirikikishi katika swala zima la uwajibikaji kuanzia serikali hadi kwa wananchi.

( 1 ) Kuongezeka kwa uwajibikaji kwa wananchi na serikali maana kila mtu atakuwa anajua kipi anabidi afanye ili kujiletea maendeleo na kuliletea taifa maendeleo kwakuwa hakutakuwa na Mtu anayemsubiri mwenzake kati ya serikali na wananchi.

(2) Kuongezeka kwa uzalendo - hii itapelekea kuongezeka kwa uzalendo ,AMANI pamoja na utulivu maana mambo mengi yatakuwa wazi hivyo uzalendo. utaongezeka mara dufu miongoni mwa wananchi.

(3) Watu wengi kushiriki katika shughuli za kisiasa katika kuchagua viongozi wanaowapenda ili waweze kuwaongoza katika maeneo yao hivyo itapelekea kupata viongozi bora maana maamuzi ya wengi huleta maana ya kuwa kiongozi ni bora.

(4) Nchi kupata maendeleo pamoja na mtu mmoja mmoja kupata maendeleo - ikiwa mtu ataelewa kuwa serikali inategemea wananchi na wananchi wanategemea serikali na wote serikali na wananchi wakijitoa kwa njia chanya basi serikali itapata maendeleo pamoja na mtu mmoja mmoja atapata maendeleo.

(5) Kujitambua kwa wananchi- ili serikali ifikie lengo la kufikisha maendeleo kwa watu wake wote lazima watu wawe wanajitambua na kuelewa maana halisi ya maendeleo hivyo kupitia kutoa Elimu kwa umma kuhusu maendeleo wananchi wengi watatoka gizani na kujitambua na kuanza kujitafutia maendeleo pasipo kuisubiri serikali.

Hitimisho:
Taifa bora litajengwa na watu bora na watu bora ni wale ambao watajikita katika kujenga ,kurekebisha na sio kulaumu, kubeba chuki, na kuichukia nchi , safari hii ,ni mimi na wewe hivyo ikiwa tutawajibika kikamilifu kwa kushirikiana katika maeneo yetu ya kazi basi tutaifikia Tanzania tuitakayo yenye Maendeleo UPENDO , utu , maadili na yenye kujali mchango wa kila Mtu.

Uongozi shirikishi -ni uongozi utakaomfanya mwananchi wa kawaida kuamini na kujua kuwa na yeye ni sehemu ya uongozi Hivyo kuwajibika ni muhimu .

"Fahamu tu kuwa uongozi mbaya huwa unapita ila nchi huwa inaendelea kubaki Hivyo usiichukie nchi yako ipende na iombee Amani"
 
Ni kweli serikali bora na kiongozi bora ni yule anayekubali kukoselewa ila wananchi bora ni wale ambao watawakosoa viongozi na serikali yao baada ya wao kutimiza wajib
Umeiweka vizuri sana. Summary timiza wajibu pata haki.

(3) Watu Kufundishwa dhana nzima ya uzalendo , Ili nchi yetu iwe na maendeleo tunahitaji uzalendo kwa wananchi na uzalendo huwa unajengwa ndani ya mioyo ya WATU kwa kuwafundisha wananchi falsafa mbalimbali ikiwemo kujua kuwa nchi huwa haipiti ila viongozi wabaya wanapita ,hivyo hata ikitokea tatizo lolote ndani ya serikali wasianze kuichukia nchi ila waendelee kuamini kuwa viongozi wabaya hupita ila nchi huwa haipiti , hivyo ili kuifikia Tanzania tuitakayo serikali inabidi kujiikita katika kutoa elimu kwa wananchi kuweka uzalendo mbele
Yas tunahitaji kuwa na falsafa moja kama taifa. Na namna ya kuifikia hii sio lazima mashuleni tu. Vitu kama filamu vinaweza kutusaidia sana.
Waandishi wa script wanapewa yanayohitajiwa kuwekwa na wakitoa filamu yenye funzo wanapata ruzuku (public funds should always fund public service). Sio kila siku tunatunga sijui yule kampenda yule, yuke kamkataa huyu na mwanaume analilia mapenzi. Je hizi ndio dhima zetu kama taifa?

Hitimisho:
Taifa bora litajengwa na watu bora na watu bora ni wale ambao watajikita katika kujenga ,kurekebisha na sio kulaumu, kubeba chuki, na kuichukia nchi , safafi hii ni mimi na wewe hivyo ikiwa tutawajibika kikamilifu katika maeneo yetu ya kazi basi tutaifikia Tanzania tuitakayo yenye UPENDO , utu , maadili na yenye kujali mchango wa kila mtu.
Ahsante kwa kutujuza haya.👏
 
Andiko bora Sana , kuna kitu nimejifunza kuhusu uongozi shirikishi mfano huwa tunawalaumu watu pasipo kujua majukumu yao yanaishia wapi.
 
Mkuu umeongea mambo ya msingi Sana kuna baadhi ya wananchi huwa hawatimizi majukumu yao kisawasawa kwa kuamini serikali itafanya kila kitu.
 
Back
Top Bottom