Nimemlipia binti mahari lakini bado ananizungusha

Habari wapedwa wa JF, mimi ni kijana wa miaka 33. Ninaishi kanda ya ziwa na ninaishi na mama yangu. Mama na baba waliachana nilipo maliza shule hadi form 4. Nilipomaliza, sikutaka kuendelea na masomo tena. Mwaka jana mwezi wa kwanza, mama akanambia umli umefika niende nikaoe na mwanamke yupo jirani tu na anapoishi.

Sikusita, nilienda hadi nyumbani kwa mama. Mama akasema, "Twende moja kwa moja kwao binti." Nilijiandaa na kwenda na mama hadi kwao yule binti. Tulikalibishwa vizuri na ghafla yule binti alipita, akatusalimia, akapita akaingia ndani.

Mama akanambia, "Vipi umemuona binti mwenyewe?" Nikamwambia, "Ndio mama, nimemuona, lakini sijajua kitabia yupo vizuri?" Mama akasema, "Bila shaka yupo vizuri sana." Nami nikasema, "Kama wewe umesema yupo vizuri, haina shida." Mama alimwita mama mwenye mji, akasema, "Si tumekuja kuchumbia kijana wangu huyu anataka kuoa kwenye hii familia." Mama mwenye mji akasema, "Haina shida, ngoja nimwite nimuulize." Basi mama akamuita, akaja, akaulizwa, "Huyu kijana amekuja kuchumbia hapa, vipi umekubaliana naye?" Yule binti akakubali.

Tukaachiwa muda tukapiga stori hadi muda fulani hivi, nikampa buku teni tukaaga na mama, tukasepa nyumbani. Nikamuuliza mama, "Vipi huyo yupo poa mama?" Mama akasema, "Yupo vizuri kitabia." Nami sikuwa na neno, nikamwambia, "Lini tunapeleka mahali?" Mama akasema, "Tuwasiliane na baba ndio tupange." Kweli baba alituambia ni jambo jema, si mshamchunguza? Yupo poa." Nikamwambia ndio.

Mwaka jana mwezi wa kumi na moja tulienda kutoa mahali 2.5M na kiasi kikubwa kilitolewa na baba. Walifanya sherehe kwao na binti siku hiyo ya mahali ilipita. Tulipewa muda wowote tu twaweza kwenda kumchukua binti kama hamna mambo ya sherehe. Tuliendelea kuchati na kuwasiliana na Jane na kupanga mara kwa mara.

Mwezi wa kumi na mbili nilienda kumtembelea Jane kwao. Nilienda na zawadi, hadi kwao nikakalibishwa vizuri. Nilipata muda wa kuongea na Jane. Nikamwambia, "Leo nimekuja kulala, vipi mazingira yapo poa?" Akastuka, akasema, "Acha utani basi." Nami nikamwambia, "Wala si utani, mimi na wewe tulishawahi kutaniana." Akasema, "Hapana." Akaropoka Jane, alisema, "Wewe mama, hataki kabisa kusikia hilo swala."

Nami sikuwa na pingamizi, nikamkubalia, nilikuja kuaga na kwenda zangu. Sikumuhoji sana, niondoka mida ya saa mbili usiku. Kumbuka, mimi ni Mnyamwezi na binti ni Mnyantuzu, mila za kwetu na baadhi ya makabila huwa na taratibu za kwenda kulala kwao binti, lakini sikufanikisha hivyo.

Baada ya siku mbili nilienda tena kwao na binti na zawadi, niliomba show tena, Jane alikataa, "Hivi si nilikwambia kuwa mama alikataa?" Nami nikasema, "Kweli, usijali, tulipiga stori, nikatambaa." Jane akanisindikiza, nikamuaga, nikasepa.

Mwezi wa kwanza, tarehe 2, nilimpigia simu baba yake na Jane, kuwa nataka nimuoe mwenza wangu. Baba mkwe akasema, "Ngoja niwasiliane nao, nitakupa jibu." Baadaye nilimtafuta binti, namba yake ikawa ina-busy kwa muda mrefu. Baadaye alinitumia ujumbe, mambo. Nikamwambia poa, vipi mzee kakwambia kuwa nakuijia. Jane akasema, "Hapana, ata sijawasiliana naye." Nikamwambia, "Sawa."

Akanambia, "Vipi, unanipeleka wapi?" Nikamwambia, "Ni kwa mama." Jane akasema, "Kwani nyumba haijakamilika uliyokuwa unajenga?" Nikamwambia, "Ndiyo, bado, ila soon." Nilikuwa na nyumba ambayo ipo mjini, haikuisha, ilikuwa yamebaki madirisha na milango tu, na Jane na wazazi wake walijua hilo.

Basi Jane tukaendelea kuchati. Naye akasema, "Nikija hapo mimi na wewe tutalalaje? Kama kwenu kuna vyumba viwili na sebule?" Nikamwambia, "Hayo yote sisi ndio tunapanga." Akasema, "Sawa, lakini mimi niliona nisubili tu hadi nyumba ikamilike ndio uniijie." Nikamwambia, "Haitawezekana, maana hata wazazi wako walikuwa wanataka nikuijie na tutaishi kwa muda kwa wazazi wetu tukipata baraka." Jane akasema, "Afu mi naumwa." Nikamuuliza, "Unaumwa nini?" Akasema, "Uchovu tu mwili wote." Nikamwambia, "Pole."

Visingizio vilikuwa vingi baada ya kusikia nataka nimpeleke nyumbani. Kesho yake niliaga nyumbani na kwenda job mbali na nyumbani, mkoa mwingine. Tokea jana sikupata mrejesho wowote kwa baba mkwe. Niliwasiliana na Jane mara kwa mara, akawa anasema, "Najua unanifikiria vibaya kuwa siumwi, ila kweli naumwa." Nikamwambia, "Mawazo yako tu." Akajibu, "Sawa." Kesho yake Jane akanipigia simu, nimtumie pesa ya kusuka.

Nikamwambia, "Sina kwa sasa." Akasema, "Sawa, kisa kilichotokea mama yako kutukanwa na baba, ndio maana hutaki kunidumia." Mimi nilijikuta naropoka, kwahyo sikumpa pesa za matumizi. Jane akasema, "Viela vyenyewe adi nikuombe." Nilipanda na hasira, nikamwamia, "Kuanzia leo agalamiwe na wazazi wake na siyo mimi." Jane akasema, "Sawa, na nakupenda sana. Kuna watu walikuja kunichumbia, nikawakataa, afu wewe huniheshimu, sawa tu." Nikamwambia, "Usidhani."
Nikamwambia, "Sina kwa sasa." Akasema, "Sawa, kisa kilichotokea mama yako kutukanwa na baba, ndio maana hutaki kunidumia." Mimi nilijikuta naropoka, kwahyo sikumpa pesa za matumizi. Jane akasema, "Viela vyenyewe adi nikuombe." Nilipanda na hasira, nikamwamia, "Kuanzia leo agalamiwe na wazazi wake na siyo mimi." Jane akasema, "Sawa, na nakupenda sana. Kuna watu walikuja kunichumbia, nikawakataa, afu wewe huniheshimu, sawa tu." Nikamwambia, "Usidhani
 
Kadai magari yako mapema. Inaonyesha hiyo familia Ina matatizo. Kama mmeanza kutofautisha hata KABLA ya ndoa jua kuna shida mbele.

Pole sana
 
Back
Top Bottom