Nimemlipia binti mahari lakini bado ananizungusha

Habari wapedwa wa JF, mimi ni kijana wa miaka 33. Ninaishi kanda ya ziwa na ninaishi na mama yangu. Mama na baba waliachana nilipo maliza shule hadi form 4. Nilipomaliza, sikutaka kuendelea na masomo tena. Mwaka jana mwezi wa kwanza, mama akanambia umli umefika niende nikaoe na mwanamke yupo jirani tu na anapoishi.

Sikusita, nilienda hadi nyumbani kwa mama. Mama akasema, "Twende moja kwa moja kwao binti." Nilijiandaa na kwenda na mama hadi kwao yule binti. Tulikalibishwa vizuri na ghafla yule binti alipita, akatusalimia, akapita akaingia ndani.

Mama akanambia, "Vipi umemuona binti mwenyewe?" Nikamwambia, "Ndio mama, nimemuona, lakini sijajua kitabia yupo vizuri?" Mama akasema, "Bila shaka yupo vizuri sana." Nami nikasema, "Kama wewe umesema yupo vizuri, haina shida." Mama alimwita mama mwenye mji, akasema, "Si tumekuja kuchumbia kijana wangu huyu anataka kuoa kwenye hii familia." Mama mwenye mji akasema, "Haina shida, ngoja nimwite nimuulize." Basi mama akamuita, akaja, akaulizwa, "Huyu kijana amekuja kuchumbia hapa, vipi umekubaliana naye?" Yule binti akakubali.

Tukaachiwa muda tukapiga stori hadi muda fulani hivi, nikampa buku teni tukaaga na mama, tukasepa nyumbani. Nikamuuliza mama, "Vipi huyo yupo poa mama?" Mama akasema, "Yupo vizuri kitabia." Nami sikuwa na neno, nikamwambia, "Lini tunapeleka mahali?" Mama akasema, "Tuwasiliane na baba ndio tupange." Kweli baba alituambia ni jambo jema, si mshamchunguza? Yupo poa." Nikamwambia ndio.

Mwaka jana mwezi wa kumi na moja tulienda kutoa mahali 2.5M na kiasi kikubwa kilitolewa na baba. Walifanya sherehe kwao na binti siku hiyo ya mahali ilipita. Tulipewa muda wowote tu twaweza kwenda kumchukua binti kama hamna mambo ya sherehe. Tuliendelea kuchati na kuwasiliana na Jane na kupanga mara kwa mara.

Mwezi wa kumi na mbili nilienda kumtembelea Jane kwao. Nilienda na zawadi, hadi kwao nikakalibishwa vizuri. Nilipata muda wa kuongea na Jane. Nikamwambia, "Leo nimekuja kulala, vipi mazingira yapo poa?" Akastuka, akasema, "Acha utani basi." Nami nikamwambia, "Wala si utani, mimi na wewe tulishawahi kutaniana." Akasema, "Hapana." Akaropoka Jane, alisema, "Wewe mama, hataki kabisa kusikia hilo swala."

Nami sikuwa na pingamizi, nikamkubalia, nilikuja kuaga na kwenda zangu. Sikumuhoji sana, niondoka mida ya saa mbili usiku. Kumbuka, mimi ni Mnyamwezi na binti ni Mnyantuzu, mila za kwetu na baadhi ya makabila huwa na taratibu za kwenda kulala kwao binti, lakini sikufanikisha hivyo.

Baada ya siku mbili nilienda tena kwao na binti na zawadi, niliomba show tena, Jane alikataa, "Hivi si nilikwambia kuwa mama alikataa?" Nami nikasema, "Kweli, usijali, tulipiga stori, nikatambaa." Jane akanisindikiza, nikamuaga, nikasepa.

Mwezi wa kwanza, tarehe 2, nilimpigia simu baba yake na Jane, kuwa nataka nimuoe mwenza wangu. Baba mkwe akasema, "Ngoja niwasiliane nao, nitakupa jibu." Baadaye nilimtafuta binti, namba yake ikawa ina-busy kwa muda mrefu. Baadaye alinitumia ujumbe, mambo. Nikamwambia poa, vipi mzee kakwambia kuwa nakuijia. Jane akasema, "Hapana, ata sijawasiliana naye." Nikamwambia, "Sawa."

Akanambia, "Vipi, unanipeleka wapi?" Nikamwambia, "Ni kwa mama." Jane akasema, "Kwani nyumba haijakamilika uliyokuwa unajenga?" Nikamwambia, "Ndiyo, bado, ila soon." Nilikuwa na nyumba ambayo ipo mjini, haikuisha, ilikuwa yamebaki madirisha na milango tu, na Jane na wazazi wake walijua hilo.

Basi Jane tukaendelea kuchati. Naye akasema, "Nikija hapo mimi na wewe tutalalaje? Kama kwenu kuna vyumba viwili na sebule?" Nikamwambia, "Hayo yote sisi ndio tunapanga." Akasema, "Sawa, lakini mimi niliona nisubili tu hadi nyumba ikamilike ndio uniijie." Nikamwambia, "Haitawezekana, maana hata wazazi wako walikuwa wanataka nikuijie na tutaishi kwa muda kwa wazazi wetu tukipata baraka." Jane akasema, "Afu mi naumwa." Nikamuuliza, "Unaumwa nini?" Akasema, "Uchovu tu mwili wote." Nikamwambia, "Pole."

Visingizio vilikuwa vingi baada ya kusikia nataka nimpeleke nyumbani. Kesho yake niliaga nyumbani na kwenda job mbali na nyumbani, mkoa mwingine. Tokea jana sikupata mrejesho wowote kwa baba mkwe. Niliwasiliana na Jane mara kwa mara, akawa anasema, "Najua unanifikiria vibaya kuwa siumwi, ila kweli naumwa." Nikamwambia, "Mawazo yako tu." Akajibu, "Sawa." Kesho yake Jane akanipigia simu, nimtumie pesa ya kusuka.

Nikamwambia, "Sina kwa sasa." Akasema, "Sawa, kisa kilichotokea mama yako kutukanwa na baba, ndio maana hutaki kunidumia." Mimi nilijikuta naropoka, kwahyo sikumpa pesa za matumizi. Jane akasema, "Viela vyenyewe adi nikuombe." Nilipanda na hasira, nikamwamia, "Kuanzia leo agalamiwe na wazazi wake na siyo mimi." Jane akasema, "Sawa, na nakupenda sana. Kuna watu walikuja kunichumbia, nikawakataa, afu wewe huniheshimu, sawa tu." Nikamwambia, "Usidhani."
Huyu dada hakupendi, hata mm nisingekubali, ulitakiwa umtongoze muwe kwenye lavidavi kabla ya mambo ya ndoa, amekuitikia tu ndio kwasababu wazaz walikuwepo. Na anaona niolewe nae bas hta nitambe mtaani mwanaume Ana nyumba ila kuoa na kumlaza kwenu na hakupendi usitegemee ndoa hapo. Ila kwel unaenda na mama kutongoza binti akiwa na mama yake.
 
Mi nikishaona mtu mzima kwenye masimulizi yake hakuishi maneno yafuatayo

Mama yangu..
Baba yangu
Dada yangu
Kaka yangu
Baba Mkwe
Shemeji
My dad sijui my mum.

Napoteza kabisa Nguvu ya kumsikiliza au kumsoma.

Sijui vile ni yatimaaa!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Habari wapedwa wa JF, mimi ni kijana wa miaka 33. Ninaishi kanda ya ziwa na ninaishi na mama yangu. Mama na baba waliachana nilipo maliza shule hadi form 4. Nilipomaliza, sikutaka kuendelea na masomo tena. Mwaka jana mwezi wa kwanza, mama akanambia umli umefika niende nikaoe na mwanamke yupo jirani tu na anapoishi.

Sikusita, nilienda hadi nyumbani kwa mama. Mama akasema, "Twende moja kwa moja kwao binti." Nilijiandaa na kwenda na mama hadi kwao yule binti. Tulikalibishwa vizuri na ghafla yule binti alipita, akatusalimia, akapita akaingia ndani.

Mama akanambia, "Vipi umemuona binti mwenyewe?" Nikamwambia, "Ndio mama, nimemuona, lakini sijajua kitabia yupo vizuri?" Mama akasema, "Bila shaka yupo vizuri sana." Nami nikasema, "Kama wewe umesema yupo vizuri, haina shida." Mama alimwita mama mwenye mji, akasema, "Si tumekuja kuchumbia kijana wangu huyu anataka kuoa kwenye hii familia." Mama mwenye mji akasema, "Haina shida, ngoja nimwite nimuulize." Basi mama akamuita, akaja, akaulizwa, "Huyu kijana amekuja kuchumbia hapa, vipi umekubaliana naye?" Yule binti akakubali.

Tukaachiwa muda tukapiga stori hadi muda fulani hivi, nikampa buku teni tukaaga na mama, tukasepa nyumbani. Nikamuuliza mama, "Vipi huyo yupo poa mama?" Mama akasema, "Yupo vizuri kitabia." Nami sikuwa na neno, nikamwambia, "Lini tunapeleka mahali?" Mama akasema, "Tuwasiliane na baba ndio tupange." Kweli baba alituambia ni jambo jema, si mshamchunguza? Yupo poa." Nikamwambia ndio.

Mwaka jana mwezi wa kumi na moja tulienda kutoa mahali 2.5M na kiasi kikubwa kilitolewa na baba. Walifanya sherehe kwao na binti siku hiyo ya mahali ilipita. Tulipewa muda wowote tu twaweza kwenda kumchukua binti kama hamna mambo ya sherehe. Tuliendelea kuchati na kuwasiliana na Jane na kupanga mara kwa mara.

Mwezi wa kumi na mbili nilienda kumtembelea Jane kwao. Nilienda na zawadi, hadi kwao nikakalibishwa vizuri. Nilipata muda wa kuongea na Jane. Nikamwambia, "Leo nimekuja kulala, vipi mazingira yapo poa?" Akastuka, akasema, "Acha utani basi." Nami nikamwambia, "Wala si utani, mimi na wewe tulishawahi kutaniana." Akasema, "Hapana." Akaropoka Jane, alisema, "Wewe mama, hataki kabisa kusikia hilo swala."

Nami sikuwa na pingamizi, nikamkubalia, nilikuja kuaga na kwenda zangu. Sikumuhoji sana, niondoka mida ya saa mbili usiku. Kumbuka, mimi ni Mnyamwezi na binti ni Mnyantuzu, mila za kwetu na baadhi ya makabila huwa na taratibu za kwenda kulala kwao binti, lakini sikufanikisha hivyo.

Baada ya siku mbili nilienda tena kwao na binti na zawadi, niliomba show tena, Jane alikataa, "Hivi si nilikwambia kuwa mama alikataa?" Nami nikasema, "Kweli, usijali, tulipiga stori, nikatambaa." Jane akanisindikiza, nikamuaga, nikasepa.

Mwezi wa kwanza, tarehe 2, nilimpigia simu baba yake na Jane, kuwa nataka nimuoe mwenza wangu. Baba mkwe akasema, "Ngoja niwasiliane nao, nitakupa jibu." Baadaye nilimtafuta binti, namba yake ikawa ina-busy kwa muda mrefu. Baadaye alinitumia ujumbe, mambo. Nikamwambia poa, vipi mzee kakwambia kuwa nakuijia. Jane akasema, "Hapana, ata sijawasiliana naye." Nikamwambia, "Sawa."

Akanambia, "Vipi, unanipeleka wapi?" Nikamwambia, "Ni kwa mama." Jane akasema, "Kwani nyumba haijakamilika uliyokuwa unajenga?" Nikamwambia, "Ndiyo, bado, ila soon." Nilikuwa na nyumba ambayo ipo mjini, haikuisha, ilikuwa yamebaki madirisha na milango tu, na Jane na wazazi wake walijua hilo.

Basi Jane tukaendelea kuchati. Naye akasema, "Nikija hapo mimi na wewe tutalalaje? Kama kwenu kuna vyumba viwili na sebule?" Nikamwambia, "Hayo yote sisi ndio tunapanga." Akasema, "Sawa, lakini mimi niliona nisubili tu hadi nyumba ikamilike ndio uniijie." Nikamwambia, "Haitawezekana, maana hata wazazi wako walikuwa wanataka nikuijie na tutaishi kwa muda kwa wazazi wetu tukipata baraka." Jane akasema, "Afu mi naumwa." Nikamuuliza, "Unaumwa nini?" Akasema, "Uchovu tu mwili wote." Nikamwambia, "Pole."

Visingizio vilikuwa vingi baada ya kusikia nataka nimpeleke nyumbani. Kesho yake niliaga nyumbani na kwenda job mbali na nyumbani, mkoa mwingine. Tokea jana sikupata mrejesho wowote kwa baba mkwe. Niliwasiliana na Jane mara kwa mara, akawa anasema, "Najua unanifikiria vibaya kuwa siumwi, ila kweli naumwa." Nikamwambia, "Mawazo yako tu." Akajibu, "Sawa." Kesho yake Jane akanipigia simu, nimtumie pesa ya kusuka.

Nikamwambia, "Sina kwa sasa." Akasema, "Sawa, kisa kilichotokea mama yako kutukanwa na baba, ndio maana hutaki kunidumia." Mimi nilijikuta naropoka, kwahyo sikumpa pesa za matumizi. Jane akasema, "Viela vyenyewe adi nikuombe." Nilipanda na hasira, nikamwamia, "Kuanzia leo agalamiwe na wazazi wake na siyo mimi." Jane akasema, "Sawa, na nakupenda sana. Kuna watu walikuja kunichumbia, nikawakataa, afu wewe huniheshimu, sawa tu." Nikamwambia, "Usidhani."
tupe mrejesho
 
Umekosea unaendaje kuposa binti wewe binafsi hujaongea naye wala kumjua wakati unayeishi naye ni wewe?
 
Vijana wa siku hizi ndiyo maana mnaitwa kwa majina mengi!

Mnaitwa 'mwendo kasi', voda fasta, dotcom nk nk kutokana na uvunjifu wa maadili mnaozaliwa nao kutoka tumboni mwa mama zenu, mnazaliwa kwa mfano kama nyoka wanavyozaliwa na kuanza kuuma bila ya kufundishwa!

Kwa taarifa yako mila za kinyamwezi na kinyantuzu kuhusu namna ya kuchumbiana na hadi kuoana hazipishani sana kwa sababu ninazijua.

Unaenda kuchumbia mtoto wa mtu, kabla ya kufunga ndoa unataka kuzini naye kwanza, ndizo mila za kinyamwezi zinavyotaka?

Mimi ninavyofahamu, mnyamwezi akitaka kuoa, siku ya kwanza hupeleka sura yake kwa msichana anayetamani kumuoa na kumtongoza kwa kuweka wazi dhamira yake hiyo.

Msichana kama ataridhia, ataenda kutoa taarifa kwa wazazi wake na wazazi wakiridhia, basi msichana atarejesha majibu kwa kijana kuwa wazazi wamekubali, lakini wamesema asubiri kwanza na baada ya wiki moja au mbili aje achukue majibu.

Kwenye kipindi hiki cha mpito watatumwa wapelelezi kuchunguza wasifu wa familia ya mvulana na kama watajiridhisha na wasifu wa ukoo huo, basi muda uliosubirishwa utakuta majibu ya" ndiyo".

Baada ya hapo wewe na mchumba hapatakuwa na mawasiliano tena ya moja kwa moja, bali sasa wewe mvulana utatafuta mshenga(mwakilishi) kwenda kupeleka kishika uchumba na kupatanisha mahari.

Mahari iliyopangwa na kukubaliana kwa pande zote mbili, itatolewa na ndoa kuandikishwa kuanza kutangazwa kwa wiki tatu, huku pande zote zikijiandaa kwa sherehe ya harusi.

Process zote hizo hufanyika mfululizo, hakuna sijui nimalizie kujenga, sijui namalizia chuo ama tutafunga ndoa mwakani, no, likianzishwa huwa halipoi.

Kwa muktadha wa bandiko lako, wewe ulienda kutafuta hawara, siyo mke wa kuoa.

Ulisikia kijana gani wa kinyamwezi anaenda kutafuta mchumba huku kaongozana na mamake mzazi?

Kama mama alipendezwa na tabia za msichana huyo na kupenda mwanaye ukamuoe, kwanini asitumie njia ya kukuelekeza tu ili taratibu na mila za kutafuta mchumba za kinyamwezi zifuatwe?

Kiuhalisia ninamuunga mkono huyo msichana kwa kuruka kihunzi cha kufanywa sex toy kwa hadaa ya kishika uchumba!

Mahari kitu gani, watu wanatoa mamilioni ya mahari waliyopangiwa na binti akijichanganya akakubali kutoa unyumba kabla ya ndoa, muoaji ana hiyari aingie mitini siku ya ndoa bila kujali gharama alizozitoa ili kuudhalilisha umalaya wa msichana na mambo huishia hapo.

Ninayosema kama ni uongo na hauridhiki nayo, kamuulize mheshimiwa Viki Kamata.

Wachumba hawatakiwi kukutana kimwili kabla ya ndoa, huo ni uhawara ni tabia ovu tunazozipigia kelele kila kukicha kwa sababu zinaenda kinyume na maadili.

Utafiti uliokwisha kufanywa ni kwamba, uchumba mwingi huvunjika kwa wachumba wanaofanya mapenzi kabla ya ndoa na hilo lipo wazi kuliko idadi ya wachumba wanaofikia ndoa na kuoana bila ya 'kujuana' kwanza.

Halafu mara mbili nzima unataka kwenda kumlala huyo msichana nyumbani kwao, lengo likiwa ni nini, umuone dosari zake za kimwili ama ilikuwa unataka kugundua nini?

Vijana wa siku hizi ni wa hovyo sana.

Huyo baba mkwe wako alitakiwa akutukanie wazazi wako wote wawili pamoja na wewe asibague, awatukane matusi ya nguoni yenye kuumiza kama adhabu yenu ya uzembe wa kushindwa kukulea katika maadili mema ya mila zenu za kinyamwezi zilizo nyoofu.

Na una bahati sana, umeilenga nyumba ya singel mother isiyo na udhibiti!

Ukikuta nyumba zenye kufuata maadili sawasawa, pamoja na kuchumbia lakini sasa unataka kuleta uhuni wako, kaka zake na msichana wangekugawana hadi ungelishangaa na usiamani unachofanyiwa!

Ungefukuzwa hapo kwa matusi, na ikiwezekana fimbo za aibu zingetembezwa ili akili zikukae sawa.

Kuchumbia na kutoa mahari siyo leseni ya kufanya ufuska na mtoto wa mtu, dini zote na mila zote zinakataza kabisa jambo hilo kwa kuwa ni haramu.
Aiseee,baba mkwe huna binti uniozeshe?
 
Back
Top Bottom