Ni kwanini Introverts wana asilimia kubwa kwenye kutoboa?

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
259
742
Muhimu: Elewa neno asilimia kubwa haimanishi ni wote, hata wazaramo wakimya wapo lakini asilimia kubwa ni waongeaji.

Introverts ni watu ambao wanapenda kuwa peke yao muda mwingi, mkikutana mnasalimiana, anaweza kukusaidia, n.k. wepo waongeaji wazuri tu lakini bado wanapenda muda mwingi kukaa wenyewe, ni tofauti na mtu ambae hajibu salamu, hataki kusaidia wengine, n.k.

Introverts ni wachache sana lakini wana asilimia kubwa kwenye kufanikiwa kupitia masomo, ubunifu, teknolojia, n.k.

Kwenye uwanja wa teknolojia wengi ni introverts kina Elon Musk, Bill Gates, Mark Zuckbereg, Jeff Bezos, Steve Jobs (rip), n.k. pia ni mabilionea.

Wanasayansi wengi walioleta magueuzi kama Isaac Newton, Albert Einsten, n.k. ni introverts.

Wale kina John Kisomo wa shuleni ilikuwa kawaida kukuta ni introverts, mtu kapata 98% anaenda kulalamika kwa mwalimu kapunjwa, huko vyuoni waliendelea kugonga gpa za juu kiasi cha kubakizwa kuwa lecturers.

Messi ni Introvert ni mchezaji bora kuwahi kutokea kwenye mpira, Wachezaji wanakiri wenyewe kwamba wanalazimika kukusanyika hata sita kumkaba yeye tu.
 
Wapo ambao hawajafanikiwa kabisa, wapo wapo tu mitaani wala hawatengenezi networking. Nadhani haya mambo ya mafanikio siri ni bahati, kutumia fursa na kuwa na bidii bila kujali sana mambo mengine. Halafu most of time unavyopata mafanikio ndivyo unavyopunguza circle ya marafiki na unaonekana introvert.
 
Unajua alafu huna mtaji alafu hapo hapo huna wa kukushika Mkono alafu kuna mshenzi anakuona kabisa wewe unajua Ila kwa sababu unajua kumzidi yeye anasema ngoja afe kivyake siku ukipasua mawingu namjua namjua zinakuaga nyingi sana hata wakikuona kwenye Shideo utasikia "nilisoma nae yule"
 
Mkuu uwe unasoma na kuelewa post kabla ya kucomment,

hakuna sehemu nimeandika wote
 
Unajua alafu huna mtaji alafu hapo hapo huna wa kukushika Mkono alafu kuna mshenzi anakuona kabisa wewe unajua Ila kwa sababu unajua kumzidi yeye anasema ngoja afe kivyake siku ukipasua mawingu namjua namjua zinakuaga nyingi sana hata wakikuona kwenye Shideo utasikia "nilisoma nae yule"
Kabisa. Umelenga mle mle.
 
Mkuu uwe unaelewa post kwanza kabla ya kucomment, hakuna sehemu nimeandika wote
Na mimi sijasema umesema wote ndo maana nikatumia neno wapo, Au kuna tatizo nikisema wapo masikini ili kutoa maoni yangu kuwa inawezekana mafanikio yanatokana na mambo mengine zaidi ya personality?
 
Na mimi sijasema umesema wote ndo maana nikatumia neno wapo, Au kuna tatizo nikisema wapo masikini ili kutoa maoni yangu kuwa inawezekana mafanikio yanatokana na mambo mengine zaidi ya personality?
Ok sawa, ndivyo ilivyo huwezi kukuta wote wanafanana, hata wazaramo wakimya wapo
 
Screenshot_20240501_085054_WhatsApp.jpg
 
Sababu ni kwamba wanga, wachawi, wafitini, wanoko ,wenye wivu na wapuuzi wengine hawajui unakwenda kufanya nini katika mambo yako.
Wanakuja kushangaa matokeo tu!
Usichokijua Wachawi ni wengi kuliko unavyofikiri, wengine hawabebi hata Matunguli hawapai na Ungo Ila wanawanga kinoma tena wanakuwangia Mchana kweupe pee hivi unawaona nimeshuhudia mara nyingi sana wakiwa wanawanga, mtu yeyote anaekuwekea kauzibe katika Jambo lako huyo ni Mchawi
 
Muhimu: Elewa neno asilimia kubwa haimanishi ni wote, hata wazaramo wakimya wapo lakini asilimia kubwa ni waongeaji

Introverts ni wachache sana lakini wana asilimia kubwa kwenye kufanikiwa kupitia masomo, ubunifu, teknolojia, n.k.

Huku kwenye mambo ya teknolojia kuanzia kina bill gates, mark, steven jobs, n.k. ni ma introverts.

Wale kina John Kisomo wa shuleni ilikuwa kawaida kukuta ni introverts, huko vyuoni waliendelea kugonga gpa za juu kiasi cha kubakizwa kuwa lecturers.

Messi ni Introvert ni mchezaji bora kuwahi kutokea kwenye soccer, Wachezaji wanatoa siri kwamba wanalazimika kukusanyika hata sita kumkaba yeye tu
Nikupongeze kwani nami nikiwa kama Extroverts ni kweli nimeshaanza Kufanikiwa na namiini nitafanikiwa zaidi kabisa.
 
Back
Top Bottom