Natamani Sana Rais Samia angemteua Dkt Shukuru Kawambwa nafasi yoyote ile serikalini au Chamani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,650
10,046
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeangalia video inayomuonesha Mheshimiwa Shukuru Kawambwa waziri wa zamani na mstaafu katika serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ,nimejikuta moyo wangu unaumia sana kwa namna alivyodhalilishwa na namna alivyotumia hekima,busara ya kiwango kilichovuka ubinadamu wa kawaida. Moyo wangu umesikitika sana,kuhuzunika sana,kupatwa na hasira sana pale nilipoona Mheshimiwa Kawambwa mtu anayelingana na Baba yangu kiumri akidhalilishwa kiasi kile.

Mheshimiwa Kawambwa ameonyesha kuwa yeye siyo binadamu wa kawaida ,ameonyesha utu uzima ni dawa.hekima aliyonayo na aliyoionesha siyo ya kujifunza kutoka darasani bali ni ya kuzaliwa nayo,ni ya kutoka nayo tumboni mwa mama yake,ni hekima aliyopewa na kujaliwa na Mungu wake. Kwa mtu aliyefikia ngazi ya uwaziri tena vipindi viwili ,mwenye kujuana na kufahamiana na viongozi mbalimbali wakumbwa wakumbwa ndani ya chama na serikali ni ngumu sana kumkuta akijishusha kwa kiwango kile na kuwa mtulivu katikati ya udhalilishaji na kutwezwa utu na heshima yake.

Natamani sana Rais Samia angemvuta binadamu huyu mwenye moyo wa kipekee na hekima za aina yake na utulivu wa kiwango cha juu kumsaidia kazi mahali popote pale ndani ya chama au serikalini,iwe ni kwenye mashirika ya umma,vyuoni au hata kwenye bodi mbalimbali. Huyu mtu ni hadhina .bado anazo nguvu za akili na mwili, bado anaishi maisha yenye hofu ya Mungu na yampendezayo Mungu. Mungu amjalie maisha marefu sana Mheshimiwa shukuru Kawambwa.

Naviomba vyombo vya dola viwachukulie hatua kali sana tena sana tena sanaaa kale kakikundi kote kalikofanya udhalilishaji kwa Mheshimiwa Kawambwa na yule mzee mstaafu..hatua kali za kisheria zichukuliwe zitakazo kuwa fundisho kwa wahuni wengine. Hatua ambazo wakitoka huko wakawe walimu kwa wengine.

Pia watu wale waamrishwe kuja hadharani kuomba radhi kwa magoti huku wakibubujikwa na machozi kwa udhalilishaji walioufanya kwa wazee wetu hawa wenye watoto,wajukuu,wakwe,ndugu,jamaa na marafiki. Vijana tuache ujinga na mihemuko ya kijinga,tuache kukurupuka na kujimwambafai .mtu amepata vijisenti kidogo anaanza kudhalilisha watu wengine .ndio maana wakati mwingine inakuwa ngumu sana kwetu vijana kuaminiwa katika mambo makubwa ,kwa kuwa tunatumia moyo na hisia kufanya maamuzi badala ya akili na mantiki.

Mheshimiwa Kawambwa ni darasa tosha na mfano halisia juu na maana ya mtu kuwa na hekima na busara.serikalini na ndani ya chama chetu cha Mapinduzi tunahitaji wazee wenye hekima na busara kiasi hiki,ambao wanajuwa waongee nini na wafanye nini na wakati gani,tunahitaji wazee wa aina hii ambao watatufunda vijana ndani ya chama kimaadili,tunahitaji wazee wa aina hiyo ya Kawambwa ambao hata katika hali ngumu na ya presha na ya udhalilishaji wanabaki watulivu na wenye stamini ya moyo na hisia na kumaliza mambo kwa utulivu.

Mheshimiwa Kawambwa ni mtu na nusu,Mungu aendelee kumbariki sana.natamani ningepata hata nafasi ya dakika tano kuchota na kupata busara zake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. MAMA ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kutokana na uchapa kazi wake uliotukuka na kukata kiu ya mamilioni ya watanzania.
 
Ili iwe nini yaani?

Wakati nchi za wenzetu zinazojitambua wanaondoa wazee kwenye ajira ili kuweka damu changa kujaribu kukimbizana na umbali wa mwendo wa dunia ya kwanza uliopo, wewe unapigia debe wazee

Wakati huo huo huna ajira zaidi ya uchawa, kweli wewe ni Mwashambwa
Nchi gani hizo? Mbona Marekani walimpa Urais Joe Biden? Je hakuna vijana kule? Hivi sasa Donald Trumph anautaka tena urais ,je Republic hawana vijana?

Uongozi ni hekima na busara na siyo habari za umri wala mvi au ndevu kama beberu. Tuwape uongozi watu kwa kuangalia uwezo wao wa kumudu majukumu na siyo habari za ujana au uzee.

Sasa vijana kama wale wahuni waliomdhalilisha Mheshimiwa Kawambwa unaweza vipi wapatia uongozi?
 
Bila shaka wewe hisia zako zipo kama za wale vijana wahuni waliowadhalilisha wazee wetu? Vijana tujifunze kutumia akili kufanya maamuzi badala ya hisia na mihemuko utafikiri wagonjwa wa akili.
Kaka Lucas, prof wala sio wakupigia chepuo hapo tayari atapata mialiko ya kutosha kutoa somo la social ethics, na mama anamfahamu vizuri its matter of time
 
Back
Top Bottom