Natamani sana biashara ya kudaka mitumba na kuitembeza mtaani!

navigator msomi

Senior Member
May 8, 2018
158
170
Wakuu nisaidieni kunipa mbinu,nina ka mtaji kama laki hivi nataka daka mitumba kadhaa na kupita nayo kitaa kuizungusha,

Mm ni mgeni mwanza ila nataka hii iwe starting point yangu ya kuijua mwanza, ni eneo gani zuri nitapata hii mitumba na je ni sehem zipi nzuri naweza tembea mitumba yangu ikatoka kwa haraka...nitangulize shukrani sana
 
Safi na hongera sana kwa uthubutu. Hujachelewa kabisa, fanya tathimini angalau ya siku tatu wahi mapema kabisa mida ya saa kumi pale mlango mmoja. Katika hizo siku tatu angalia vile wanafanya na utafute mwenyeji katika hizo mishe. Naimani katika hizo siku tatu utakuwa umepata kitu, hizo siku tatu usichukue mzigo we nenda kwa ajili ya kusoma namna wanavyo fanya na kupata uenyeji vizuri pia wadau kadhaa.

Baada ya hapo ingia mzigoni sasa, chukua bidhaa ambayo unaona inatoka kwa urahisi huko kitaa. Pita kitaa ukiuza viwalo vyako, usiogope unapo enda kwa mteja akagoma kununua ni sehemu ya mchezo husika. Muhimu we kaza tu, fanya kwa miezi mitano ndani ya mwaka huu naimani hiyo 100k itakuwa imezaa sana.

Sote kwa pamoja tukifika mwezi wa kumi panapo majaliwa nitafute nikupe heka tatu huko Mpanda-Katavi upige kilimo cha mahindi, utakuja kunishukuru. Maishani ni ukutane na watu sahihi tu, wengi tunafeli kwa kuwa na watu wasio sahihi.
 
Chukua mzigo ukitaka kupata pesa Nenda kauzee kwenye Minanda/Magulio huko ndio Kuna pesa hasa Kwa nguo za Mitumba
 
Safi na hongera sana kwa uthubutu. Hujachelewa kabisa, fanya tathimini angalau ya siku tatu wahi mapema kabisa mida ya saa kumi pale mlango mmoja. Katika hizo siku tatu angalia vile wanafanya na utafute mwenyeji katika hizo mishe. Naimani katika hizo siku tatu utakuwa umepata kitu, hizo siku tatu usichukue mzigo we nenda kwa ajili ya kusoma namna wanavyo fanya na kupata uenyeji vizuri pia wadau kadhaa.

Baada ya hapo ingia mzigoni sasa, chukua bidhaa ambayo unaona inatoka kwa urahisi huko kitaa. Pita kitaa ukiuza viwalo vyako, usiogope unapo enda kwa mteja akagoma kununua ni sehemu ya mchezo husika. Muhimu we kaza tu, fanya kwa miezi mitano ndani ya mwaka huu naimani hiyo 100k itakuwa imezaa sana.

Sote kwa pamoja tukifika mwezi wa kumi panapo majaliwa nitafute nikupe heka tatu huko Mpanda-Katavi upige kilimo cha mahindi, utakuja kunishukuru. Maishani ni ukutane na watu sahihi tu, wengi tunafeli kwa kuwa na watu wasio sahihi.
Haha mkuu nawe saiv una heka
 
Kazi moja ngumu saanaa hii.
Usiwekeze pesa nyingi sana
Asante, eleza kidogo boss
Utatembea sana na jua ni lako,vumbi,mvua na kadhalika.
Wanakopa sana haswa wamama wa kitaa.
Kuhenya na mzigo mtaa kwa mtaa
Tarajia kuumwa miguu,mikono,shingo,mgongo na kichwa.
Uswahilini wamejaa wazee wa wewe chuma uleta so jiandae kugawana mapato.
Kama una mtaji unaofikia 2 mil anzisha biashara ya maji ya kunywa,juice na soda
 
Back
Top Bottom