Naomba ushauri wa kimasomo

Yohimbe bark

JF-Expert Member
Sep 1, 2019
1,131
2,701
Hello great thinkers,

Mwaka 2021 nilikua nafanya mtihani wangu wa mwisho wa diploma ya pharmacy lakini sikuweza kumalizia mitihani yangu ya mwisho miwili iliyokua inafanyika kesho yake kwasababu nilipata ajali iliyonipelekea kukaa kwa mwaka nikitibiwa.

Mistake niliyofanya sikuandika barua ya kupostpone mwaka huo, mwaka huu nikataka nikamalizie mitihani yangu hiyo miwili lakini nipo mkoani chuo kipo dar ikanibidi nianze kufanya communication na chuoni but sioni ushirikiano mzuri wananiambia wanafatilia, ikanibidi niende nacte ya huku mkoani kufatilia wakaniangalia kwenye system wakakuta nimeandikiwa "postponed" wakaniambia niende chuoni ili chuo kiandike barua iende nacte ili niweze kuruhusiwa nifanye mitihani yangu iliyobaki mwezi wa nane.

Dhumuni la kuanzisha uzi huu majibu ya NACTE huku kanda ya ziwa sijaridhika nayo niliwaza niende NACTE Dodoma mwenyewe labda issue inaweza kuishia dodoma mimi nikaenda chuo kufanya mtihani tuu. Kwa wenye uelewa na utaratibu wa NACTE na vyuo vya afya naombeni ushauri, wale wakutukana ka kukebehi ruksa pia am ready, by the way mwandiko wangu m'baya mtanisamehe.
 
Nacte wameshakwambia nenda chuoni, sasa sijui wewe unataka nini tena huko Dodoma, labda una nauli za kuchezea
 
Son, ushapewa ushauri ufuate na utekeleze, usiwe mjuaji sana itazidi kukugharimu. Muda unavyozidi kwenda usipotuliza halmashauri ya kichwa chako utaishia kulia lia.
 
Zile pilikapilika za maisha umepitia baada ya hiyo inshu (ajali) utaweza kweli kujibu hiyo mitihani ilibaki? Kwamba mwanangu maisha ya kitaa yamekuwa magumu mpaka umetamani kurudi darasani, sio poa aisee!

Yote kwa yote kila la kheri.
 
Zile pilikapilika za maisha umepitia baada ya hiyo inshu (ajali) utaweza kweli kujibu hiyo mitihani ilibaki? Kwamba mwanangu maisha ya kitaa yamekuwa magumu mpaka umetamani kurudi darasani, sio poa aisee!

Yote kwa yote kila la kheri.
Ni mitihani miwili mzee namalizia, siendi kukaa darasani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom