Mwanza ni sehemu gani wanachoma kitimoto Murua?

Achana na kitimoto ukiwa Mwanza....

Furahia namdhari ya nyumba ndani ya mawe na milima ya mawe, wakazi wataalam wa kunyonga baskeli nakadhalika.

Kama ni mdau a kupenda msosi basi kula Samaki wanaopatikana huko kama chakula kwa muda uko huko hadi utapoondoka.

Sato au Sangara wa supu/mchemsho
Sato au Sangara wa kuchoma
Sato au Sangara wa kukaanga
Sato au Sangara aliyechovywa mchuzi
Ukitaka kubadili ladha agiza wale waliokaushwa /vibambala.
Ukiweza kulumangia dona na dagaa la Mwanza basi utakuwa ume vyeza sana.

Kila la kheri.
 
Uache kuwaza sato aliyekaangwa vizuri unawaza vitu vya ajabu?
 
Kuna sehemu hapo mbele kidogo ya daraja la Rock City Mall, upande wa kulia. Wana kitimoto tamu
 
Sasa Mwanza kuna maajabu gani? Samaki wa maji baridi (Victoria) wanauzwa Mwanza ghali zaidi ya Dar es salaam? Haya nayo ni maajabu.
Seriously? 😳
Iweje Dar wawe low priced kuliko wanapovuliwa?
 
Back
Top Bottom