Mwanandoa hapaswi kuishi mbali na mwenza wake

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,587
22,155
Hii inawahusu wale ambao mume anaishi mkoa tofauti na mkewe kwa sababu za kikazi.

Sio vyema kuishi namna hiyo. Ikiwa hamuishi pamoja kama wanandoa, mtakuwa na uaminifu kwa ndoa yenu kwa muda mfupi tu, baada ya hapo mambo yataanza kubadilika. Mwili utakusukuma kwenye ukuta, utaanza kutaniana na wafanyakazi wenzio kuhusu mwili kuwaka tamaa, utashawishika hata kupiga nyeto kwa kuwa mwenza wako yupo mbali nawe, baada ya muda utaona utasema kwenye nyeto na kutafuta mtu wa kupeana naye raha.

Kwa wasomaji wa Biblia mnajua wazi kile Biblia inafundisha kwamba sex ni HITAJI muhimu la mwili. Tunahitaji oksijeni.

Mume na amtimizie mkewe mahitaji ya sex, naye mke amtimizie mumewe mahitaji yake -1 kor 7:3.

Ni Mungu ndiye aliyeumba mahitaji yetu ya sex, hivyo huwezi kuomba ama kufanya maombezi eti usiwe na hamu ya kunyanduana.

Mtume Paulo hakuwahi kufanya maombezi ya ukombozi dhidi ya wenye kuwaka tamaa ya sex bali alishauri kwa wote wasioweza kujizuia waoe ili kutimiziana mahitaji ya sex ili kuepuka uasherati 1kor7:1-5.

Sababu kuu ya wanandoa kukaa mbali ni (majukumu ya kazi) pesa.

Isipokuwa kazi yako haiwezi kuruhusu kuwa pamoja kwa kipindi kama vile shughuli za kijeshi, wanandoa wanapaswa kuishi pamoja - na ikiwa wanahitaji malisho ya kijani kibichi, wanapaswa kuhama pamoja.

Ubarikiwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom