SoC04 Mustakabali wa Teknolojia na suluhisho la ukosefu wa ajira na kukuza uchumi wa Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Wakusolve

JF-Expert Member
Jul 30, 2020
212
154
Teknolojia nini?

Teknolojia ni hatua ya mabadiliko kutoka katika matumizi magumu ya kazi kuja katika njia rahisi ya utendaji kazi kwa urahisi na haraka.

Au Teknolojia ni sayansi ya hali ya juu ya ubunifu wa vitu na kubadilisha vitu vilivyokuwa na mifumo wa njia nyingi za uchakataji wa jambo fulani na kuwa mmoja na haraka katika kuleta maendeleo na matokeo chanya ya haraka zaidi.

Au Teknolojia ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi, ujenzi, vifaa, mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii.

HISTORIA YA TEKNOLOJIA
Teknolojia imeanza miaka mingi iliyopita toka binadamu kuwepo duniani.Teknolojia ya zamani kabisa ni hile ya matumizi ya zana za mawe ambayo iligundulika Olduvai Gorge nchini Tanzania.

UGUNDUZI WA INTANETI NA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA

Baada ya kompyuta kugundulika na kutumika kama kifaa cha mawasiliano, teknolojia iliendelea kukua ambapo mwaka 1965 Email iliweza kugundulika pia na watu walitumia kama sehemu ya mawasiliano kupitia kompyuta.

Mnamo mwaka 1969 Wizara ya ulinzi ya nchini Marekani ilitengeneza mfumo unaoitwa "Advanced Research Project Agency Network" (ARRANET) mfumo huu ulikuwa unaziunganisha kompyuta za wizara hiyo kwa ajili ya kuwasiliana ndani ya wizara hiyo. Tarehe 29 october mwaka 1969 barua pepe ya kwanza ilitumika katika mfumo wa ARRANET.

Website ya kwanza duniani info.cern.ch ilitengezwa mwaka 1991 na Tim Berners Lee hii iliendeleza kusaidia teknolojia duniani kuendelea kusambaa zaidi na lengo la project hii ilikuwa ni kuhusu "World Wide Web" na lilichapishwa kwa kompguta ya Next. Pia ugunduzi wa google, microsoft, facebook, Amazoni, twitter, instagram, youtube, telegram na nyenginezo umechangia kwa ukubwa sana teknolojia kusambaa duniani kote na kufanya dunia kama kijiji ambapo watu wa nchi moja wanawasiliana na nchi nyengine kwa urahisi zaidi.

UKUAJI NA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA NCHINI TANZANIA

Tanzania inakadiliwa kuwa na watu millioni 69, 149, 893, ukubwa wa ardhi 885, 800km2.
Source worldometer(www.worldometer.info).

Data hizi zinaonesha jinsi Tanzania idadi ya watu inazidi kuongezeka kwa kasi zaidi.

Tanzania hatuko nyuma sana kwenye maswala ya teknolojia kwani kuna vyuo vikuu zaidi ya vitatu vinatao kozi za Teknolojia na vyuo vingine zaidi ya vitano mfano wa vyuo ni kama UDSM, UDOM, MUST, IFM, DIT, NIT na vingine hii inachangia kukua kwa teknolojia nchini Tanzania kupitia ujuzi wanafunzi wanaopata kupitia vyuo hivi.

Ongezeko la wahitimu wa vyuo na Sababu za ukosefu wa ajira Tanzania

Kutokana na nchi yetu idadi ya watu kuongezeka ambapo mpaka sasa inakadiliwa kuwa Tanzanaia ina idadi ya watu milioni 69, 149, 893.

Idadi hii ya watu inapelekea ukosefu wa ajira kutokana na mahitaji ya watu kuongezeka, kuna idadi kubwa ya wahitimu wanaombaliza vyuo vikuu na kati kwa mwaka hivyo soka la ajira kuwa dogo.

Hapa chini ni utafiti ulioyofanywa na gazeti la mwananchi jinsi tatizo la ukosefu wa ajira lilivyo Tanzania

Mwanachi

Kutokana na wahitimu wengi Tanzania kuongezeka mfano mwaka 2018 kulikuwa na wahitimu 49, 154 , mwaka 2019 walikuwa wahitimu 51, 228, mwaka 2020 walikuwa wahitimu 48, 621 na Mwaka 2021 walikuwa wahitimu 54, 810 ripoti ya vitalstats ya TCU.

Ripoti ya Tanzania figure 2021 inayotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)inaonesha idadi ya ajira inaongezeka kidogo huku idadi ya wahitimu ikiongezeka kwa kasi kubwa, idadi ya wenye ajira nchini mwaka 2019 ni millioni 22.4, mwaka 2020 ni millioni 23 na mwaka 2021 ni millioni 23.5.

Idadi ya wasio na ajira mwaka 2017 ni asilimia 9.9, mwaka 2018 ni asilimia 9.7 , mwaka 2020 ni asilimia 9.6.

kusoma zaidi link hii
Source ni gazeti la Mwananchi

Sababu za ukosefu wa ajira Tanzania
1. Mabadiliko katika sera za serikali Katika nchi yetu ya Tanzania.

Tanzania kuna sera zilizobadilika zinapelekea idadi kubwa ya wahitimu kukosa ajira nchini mfano kitendo cha utumishi kuachia taasisi na mashirika kuajili wenyewe badala ya utumishi kutumia utaratibu wa awali ambapo wao kama wao ndio wanafanya mchakato wa kuajiri, mchakato wa mashirika na taasisi kuajiri wenyewe unawezakuwa na kosoro kama kujuana na kupelekea baadhi ya watu wenye sifa sitahiki kukosa ajira na watu wasio na sifa kupata kazi kutokana na kujuana.

2. Sheria kali za kazi

Sheria kali za kazi inaweza pelekea baadhi ya wahitimu kukosa ajira mfano kutumia vigezo vya uzoefu , hichi ni kigezo ambacho kina wafanya wahitimu wengi kukosa sifa za kuajiriwa kwani wengi wao unakuta katoka kumaliza chuo na ajapata uzoefu wowote akiwa chuoni.

3. Mabadiliko ya kiteknolojia

Tanzania pia ni miongoni mwa nchi duniani inayo athirika na teknolojia mfano matumizi ya zana za kisasa yanachangia pakuwa baadhi ya vibarua kukosa kazi ambazo hapo awali zilikuwa zinafanywa na binadamu lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia inapelekea kazi kufanywa na machine mfano ujio wa matrekta unapelekea vibarua wa kulima kukosa ajira.

4. Mitala ya elimu kutoendana na soko la ajira Tanzania

Elimu inachangia kwa nafasi kubwa mtu kupata ajira, wakati huu baadhi ya programu aziendani na ushindani wa soko au wanafunzi awafundishwi vizuri kukabiliana ukosefu wa ajira ambalo ni janga kote duniani.

5. Kupungua kwa Uzalishaji

Uzalishaji unachangia kwa kiasi kikubwa kwa vijana kupata ajira kupitia kampuni mbalimbali kutoka na uzalishaji wa kampuni kupungua upelekea baadhi ya vijana kukosa kazi za kufanya, mfano kipindi hichi kutokana na mvua kubwa kumepelekea baadhi ya vijana kupoteza mali zao kama nyumba walizokuwa wanaishi na kurudi nyuma , wengine walikuwa wamejiajiri kwenye kilimo lakini kutokana na mvua kubwa zimepelekea kuwa watu ambao awana kazi yoyote ya kufanya.

Note: Hizi ni baadhi ya sababu za ukosefu wa ajira nchini , zipo sababu nyingi zinazopeleka ukosefu wa ajira nchini Tanzania.

Mabadiliko ya Teknolojia na suluhisho la ukosefu wa ajira Tanzania

Tanzania ni nchi inayokuwa zaidi barani Afrika ili tuweze kupata maendeleo yajao ni vizuri serikali ikawekeza nguvu kwenye sekta ya teknolojia.

Duniani ya sasa hivi inategemea teknolojia kwenye sekta mbalimbali kutatua matatizo.

Serikali ikiwekeza kwenye sekta ya teknolojia inaweza kuwa mkombozi kwenye maswala ya ukosefu wa ajira pia kukuza uchumi wa nchi kupitia fedha za kigeni kwa njia ya wananchi kufanya kazi kwenye makampuni ya nje kwenye sekta ya teknolojia kama vile software developer, graphic designer na nyengine.

Mambo ya msingi ambayo serikali ikiwekeza inaweza tatua tatizo la ukosefu wa ajira wakati huu na ujao

1. Matumizi ya lugha ya kiswahili

Kiswahili ni lugha inayokuwa kwa kasi sana Afrika na nje ya Africa mfano nchini kongo, Afrika kusini, Rwanda , Burundi, Gabon, Marekani, ujerumani, bara la ulaya , uchina kiswahili kinatumika.

Kiswahili kinatambulika miongoni mwa lugha za kimataifa kama vile kifaransa, kiarabu, kihispaniola na hata kireno. Marekani, wamerekani wenye asili ya kiafrika na wazungu wamekuwa wakijifunza kiswahili kama mojawapo ya masomo katika vyuo vikuu.
Kiswahili kimetuliwa kama lugha rasmi ya umoja wa Afrika.

Nini kifanyike katika nchi ili kuongeza ajira kupitia kiswahili
A. Serikali ianzishe tahasusi zenye masomo ya kiswahili na lugha za kigeni kama kichina, kifaransa, kijerumani kutokana na mwiingiliano wa jamii hizi na Tanzania katika biashara.

Kupitia mwiIngiliano huu ni vizuri watanzania kujua lugha za watu wanao fanya nao biashara.
Pia kutawasaidia walimu wa lugha ya kiswahili na wanaojua lugha za mataifa hayo kupata ajira katika mataifa hayo kama uchina, ufaransa na ujerumani. Sababu kuu watu watakuwa wanataka kujifunza kiswahili na wengine kutaka kujua lugha za kigeni ili kuweza kutumia katika biashara hivyo wakalimani watapata ajira pamoja na walimu wanaofundisha lugha za kigeni.

B. ubadilishanaji wa wanafunzi
Serikali ili kuweza kukuza zaidi kiswahili inaweza kutumia njia ya kubadilishana na wanafunzi wa mataifa hayo ya kigeni ilikuweza wao kujifunza lugha yetu na sisi kujifunza lugha zao hii itapelekea vijana wengi kupata uzoefu wa maisha ya nchi mbalimbali na kuja kuwekeza Tanzania na kuongeza ajira pia inasaidia vijana kutafuta masoko nje ya nchi na kufanya uchumi kuwa mkubwa zaidi kwa kuuza bidhaa nje ya nchi.

2. Matumizi ya Akili bandia(Artificial intelligence)

Akili bandia ni uwezo wa programu za kompyuta kufanya kazi kama uwezo wa mwadamu. Matumizi aya yanaweza kutumika katika kutatua matatizo katika fani ya afya, elimu, kilimo na nyengine.

Teknolojia ya akili bandia inaendelea kukua zaidi na kutumika katika sehemu mbalimbali mfano kwenye simu kama iphone, samsung akili mandia imewekwa kwenye baadhi ya programu kwenye simu hizo. Kusoma zaidi hapa

Nini kifanyike katika matumizi akili bandia
Katika kutatua tatizo la ajira nchini serikali inabidi iweke mitala ya matumizi ya akili bandia.

Teknolojia hii ikifundishwa sasa basi inaweza kutatua tatizo la ajira wakati ujao kwani ni teknolojia inayotabiliwa kufanya mapinduzi wakati ujao mfano kama wanafunzi watafundishwa kuusu akili bandia basi watakuwa na uwezo wa kufanya kazi sehemu yoyote duniani(remote jobs)na hii inaweza kuwa suluhisho la ukosefu wa ajira.

Dunia ya wakati huu kazi unaweza kufanya sehemu yoyote kutokana na ujuzi ulinao moja ya ujuzi wa wakati ujao ambao serikali inatakiwa kutilia maanani ni matumizi ya akili bandia.

3. Matumizi ya Virtual Reality(VR)

Virtual Reality ni teknolojia inayounda mazingira ya kweli ya kufikirika ambayo ni ya kina mara nyengine zaidi kuliko ulimwengu wa kweli pia inaweza kutumika katika kufundishia

Nini kifanyike katika kutatua tatizo la ajira nchini
Serikali na mashirika mengine ya umma inatakiwa kuwekeza nguvu kazi kwenye teknolojia hii kwani ni fursa ya ajira inayoweza kusaidia kupata kipato mfano teknolojia hii watu wanaweza kutumia kama sehemu ya kufundishia, kufanya burudani na kupata pesa kupitia kujiajiri katika teknolojia hii.

Pia tunaweza kupata pesa za kigeni kwa watu kufundisha kupitia Virtual reality, mfano waalimu wa kiswahili wanaweza kutumia fursa ya teknolojia hii kufundisha lugha ya kiswahili kwa watu wa afrika na nje ya Afrika.

Na mwisho serikali inatakiwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana walio jiajiri katika teknolojia hii ili kuweza kusaidia kupata kipato bila shida mfano serikali inatakiwa kufanya malipo ya PayPal kufanyika nchini itasaidia watu walio jiajiri kupata pesa zao kwa urahisi na haraka zaidi.

4. Kutoa msaada wa kifedha kwa startup project(Wazo bunifu) ilizoanzishwa Tanzania

Serikali inatakiwa kuwapa msaada wa kifedha kwa waanzilishi wa hizi project kwani zinaweza saidia watu wengi kupata ajira pindi zikishakuwa kubwa mfano saizi kuna start up kama Niajiri, Waga, Nilipe, TUNZAA, NaLa App na nyengine hizi project kama serikali itaweka nguvu nyingi pesa zinaweza kuwa msaada mkubwa wa kupunguza tatizo la ajira nchini wakati huu na ujao.

Serikali kupitia TCRA, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia itoa sheria wezeshi kwa vijana wale wanaotaka vibari kwa ajiri ya kuanzisha au kuendesha kampuni za teknolojia nchini itasaidia mwamko wa vijana kufungua kampuni nchini.

5. Matumizi ya Cyptocurrency

Cyptocurrency ni biashara ya manunuzi mtandaoni kupitia bitcoin au sarafu za dhahabu na shaba.
Matumizi aya ya cyptocurrency au Teknolojia hii inaenea kwa kasi duniani kote ambapo nchi mbalimbali zimeshaanza kufanya biashara hii mfano nchi kama south Afrika, Ghana, Nigeria, Kenya , Ethiopia, Senegal kuna ecfa hizi nchi zote matumizi ya bitcoin yanaendelea kukua siku hadi siku.

Source :businessworld
Kusoma zaidi

download (1).jpeg

Nini kifanyike?
Serikali inatakiwa kuangalia kwa umakini Teknolojia hii na kufanya utafiti wa kina nakujua itasaidiaje mazingira wezeshi kwa vijana wanaofanya biashara ya bitcoin maana hii ni biashara ya wakati ujao ambayo italeta mapinduzi.

Serikali inatakiwa kuitilia mahanani maana inaweza kuwa msaada kwa tatizo la ukosefu wa ajira wakati huu na ujao.

6. Matumizi ya Ujuzi wa mtandao (Digital skills)

Ujuzi huu unamuwezasha mtu kufanya kazi sehemu yoyote hile duniani mfano graphic designer, software developer, Human resource, na zengine, ujuzi huu unaweza patikana chuoni au kupitia mitandao ya kijamii kama youtube.

Nini kifanyike
Serikali inatakiwa kuweka nguvu kwenye ujuzi huu wa kimtandao kwani itapunguza sana vijana wasio na ajira kuweza kujiajiri mtandaoni kupitia ujuzi huo walio nao.

Serikali pia iboreshe mitahala yao ya chuo katika kozi zinazo husu mambo ya teknolojia kuwa wa vitendo zaidi kuliko nadharia mfano vyuo au wanafunzi kupata huduma ya intaneti bure wakiwa chuoni itaongeza wanafunzi kujifunza zaidi.

Serikali kuendelea na kuongeza nguvu mashindano yanayohusu digital skill kupitia TCRA ili kuendelea kukuza tasnia ya teknolojia ambayo inaweza kuwa mkombozi wa kuondoa tatizo la ajira wakati huu na ujao.

Sekta ya teknolojia ili iweze kufika mbali nini kifanyike nchini na kuongeza ajira zaidi

A. Huduma ya intaneti iwe rafiki

Serikali inatakiwa kutengeneza sheria ambayo watoa huduma pamoja na watumiaji wa mitandao hii kuwa na manufaa pande zote mbili, mfano mabando yanatakiwa yawe rafiki ilikuweza vijana walio jiajiri kufanya kazi mtandaoni kufanya kazi katika mazingira rafiki zaidi.

B. Matumizi ya Paypal

Serikali inatakiwa kufanya matumizi ya malipo kwa njia ya paypal yanafanyika nchini ilikufanya vijana wanaofanya kazi mtandaoni kupata pesa zao kwa njia rahisi zaidi.

C. Matumizi ya Solar panel vijijini

Katika maeneo ambayo ajafikiwa huduma ya umeme ni vizuri wananchi kupewa huduma ya umeme wa jua ili watu waweze kupata huduma ya watu kujifunza ujuzi wa mtandao katika mazingira wezeshi kwani nishati ya umeme inasaidia kuendesha vifaa vya kelectroniki.

HITIMISHO
Mawazo katika chapisho hili ni matumizi ya teknolojia wakati huu na ujao kama serikali itayafanyia kazi inaweza kusaidia kuondoa au kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini wakati huu na ujao kwa sababu hizo ni teknolojia za wakati ujao pia inaweza saidia uchumi kukua zaidi kwa sababu vijana watajiajiri ndani na nje ya nchi na kuongeza pesa za kigeni zaidi.
 
Attachments

  • IMG_20240514_170131.JPG
    IMG_20240514_170131.JPG
    160.1 KB · Views: 2
  • download (1).jpeg
    download (1).jpeg
    21.4 KB · Views: 2
Teknolojia ni sayansi ya hali ya juu ya ubunifu wa vitu na kubadilisha vitu vilivyokuwa na mifumo wa njia nyingi za uchakataji wa jambo fulani na kuwa mmoja na haraka katika kuleta maendeleo na matokeo chanya ya haraka zai
Nimeipenda hii, matumizi ya teknolojia ni kipimo mojawapo cha akili. Kusahilisha michakato

Kutokana na nchi yetu idadi ya watu kuongezeka ambapo mpaka sasa inakadiliwa kuwa Tanzanaia ina idadi ya watu milioni 69, 149, 893
Mmmh hapa bro hujakadiria: hadi watatuu🤫🤯, ungesema tu karibu milioni sabini au 69,150,000

5. Kupungua kwa Uzalishaji

Uzalishaji unachangia kwa kiasi kikubwa kwa vijana kupata ajira kupitia kampuni mbalimbali kutoka na uzalishaji wa kampuni kupungua upelekea baadhi ya vijana kukosa kazi za kufanya, mfano kipindi hichi kutokana na mvua kubwa kumepelekea baadhi ya vijana kupoteza mali zao kama nyumba walizokuwa wanaishi na kurudi nyuma , wengine walikuwa wamejiajiri kwenye kilimo lakini kutokana na mvua kubwa zimepelekea kuwa watu ambao awana kazi yoyote ya kufanya.
Hali ni ngumu hivi, na bado tunazipeleka ajira nchi za nje. Yaani Mmarekani ambaye waganyakazi kwake ni gharama apeleke ajira zake Asia na Uchina..... na sie ambao wafanyakazi si gharama bado tunazipeleka ajira huko huko China Asia na hadi Mmarekani mwenyewe tunalazimisha kumuajiri??🤯

Serikali kupitia TCRA, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia itoa sheria wezeshi kwa vijana wale wanaotaka vibari kwa ajiri ya kuanzisha au kuendesha kampuni za teknolojia nchini itasaidia mwamko wa vijana kufungua kampuni nchini.
Hakika, Kazi kuu iwe ni kulea na kujenga kuliko kutoza na 'kudhibiti' zaidi. Hata wanapodhibiti iwe ni katika lengo la kulea zaidi ya vyote.

Serikali inatakiwa kuangalia kwa umakini Teknolojia hii na kufanya utafiti wa kina nakujua itasaidiaje mazingira wezeshi kwa vijana wanaofanya biashara ya bitcoin maana hii ni biashara ya wakati ujao ambayo italeta mapinduzi.

Serikali inatakiwa kuitilia mahanani maana inaweza kuwa msaada kwa tatizo la ukosefu wa ajira wakati huu na ujao.
Hapa sijajua kama serikali itasapoti fedha isiyoendeshwa na yenyeweyenyewe🤒🤔. Nchi kama nchi itahusika zaidi na mambo inayoyaongoza.
Na hasa tunatamani watu wa bitcoin na forex muwekeze pia kwenye vitu vinavyoshikika zaidi. Vitu hewahewa hivi sio vya kuendekeza sana. Soko la mtaji libaki kuwa soko la mtaji kwerikweri.

Huduma ya intaneti iwe rafiki

Serikali inatakiwa kutengeneza sheria ambayo watoa huduma pamoja na watumiaji wa mitandao hii kuwa na manufaa pande zote mbili, mfano mabando yanatakiwa yawe rafiki ilikuweza vijana walio jiajiri kufanya kazi mtandaoni kufanya kazi katika mazingira rafiki zaidi.
Nakubali.

Matumizi ya Paypal

Serikali inatakiwa kufanya matumizi ya malipo kwa njia ya paypal yanafanyika nchini ilikufanya vijana wanaofanya kazi mtandaon
Yas, kwa ajili ya kuboresha soko la ujuzi wa vijana wetu. Waweze kufanya kazi za nje (tuimpprt kazi) na kupokea malipo kiulainii. Hii nzuri.

Mawazo katika chapisho hili ni matumizi ya teknolojia wakati huu na ujao kama serikali itayafanyia kazi inaweza kusaidia kuondoa au kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini wakati huu na ujao kwa sababu hizo ni teknolojia za wakati ujao pia inaweza saidia uchumi kukua zaidi kwa sababu vijana watajiajiri ndani na nje ya nchi na kuongeza pesa za kigeni zaidi.
Ahsante sana, umetisha 👏
 
Nimeipenda hii, matumizi ya teknolojia ni kipimo mojawapo cha akili. Kusahilisha michakato

Mmmh hapa bro hujakadiria: hadi watatuu🤫🤯, ungesema tu karibu milioni sabini au 69,150,000

Hali ni ngumu hivi, na bado tunazipeleka ajira nchi za nje. Yaani Mmarekani ambaye waganyakazi kwake ni gharama apeleke ajira zake Asia na Uchina..... na sie ambao wafanyakazi si gharama bado tunazipeleka ajira huko huko China Asia na hadi Mmarekani mwenyewe tunalazimisha kumuajiri??🤯

Hakika, Kazi kuu iwe ni kulea na kujenga kuliko kutoza na 'kudhibiti' zaidi. Hata wanapodhibiti iwe ni katika lengo la kulea zaidi ya vyote.

Hapa sijajua kama serikali itasapoti fedha isiyoendeshwa na yenyeweyenyewe🤒🤔. Nchi kama nchi itahusika zaidi na mambo inayoyaongoza.
Na hasa tunatamani watu wa bitcoin na forex muwekeze pia kwenye vitu vinavyoshikika zaidi. Vitu hewahewa hivi sio vya kuendekeza sana. Soko la mtaji libaki kuwa soko la mtaji kwerikweri.

Nakubali.

Yas, kwa ajili ya kuboresha soko la ujuzi wa vijana wetu. Waweze kufanya kazi za nje (tuimpprt kazi) na kupokea malipo kiulainii. Hii nzuri.

Ahsante sana, umetisha 👏
Thanks mkuu
 
Ndio mkuu tutaongeza pesa na kukuza uchumi wa ndani na pia itasaidi kupata pesa za nje na hii inaweza kuwa suruhisho la upungufu wa dollar nchini
 
Hakika, Kazi kuu iwe ni kulea na kujenga kuliko kutoza na 'kudhibiti' zaidi. Hata wanapodhibiti iwe ni katika lengo la kulea zaidi ya vyote.
Ndio inatakiwa watoe msaada zaidi wa kifedha kuliko kuzuia au kufungia kabisa
 
Hali ni ngumu hivi, na bado tunazipeleka ajira nchi za nje. Yaani Mmarekani ambaye waganyakazi kwake ni gharama apeleke ajira zake Asia na Uchina..... na sie ambao wafanyakazi si gharama bado tunazipeleka ajira huko huko China Asia na hadi Mmarekani mwenyewe tunalazimisha kumuajiri??🤯
Ndio mkuu kuondoa changamoto hizi ni sisi kama taifa kuinvest kwenye teknolojia maana dunia wakati huu ipo kwenye teknolojia tupate expert wengi ambao wata invest kwenye teknolojia namini tatizo la ajira litapungua
 
Ndio mkuu tutaongeza pesa na kukuza uchumi wa ndani na pia itasaidi kupata pesa za nje na hii inaweza kuwa suruhisho la upungufu wa dollar nchini
Yas, na dola zinakuja kwa kile tunachouza bidhaa na UJUZI vikiwamo. Sasa mazingira yanapokuwa magumu kupokea madolari tunakuwa hatujengi.

Mifumo tu ya kiintelijensia inakuwepo kudhibiti uhalifu na utakatishaji fedha. Lakini sio kuzuia kabisa. Ahsante
 
Back
Top Bottom