Msaada Rice cooker ipi nzuri yenye uwezo wa kupika mchele kilo moja na nusu?

Wadau kwema? Aisee hii wiki ya pili sasa kila nikijaribu kupika wali nachemka. Mara siku nyingine napatia mara siku nyingine kinatoka kiini.

Leo kimetoka kiini nimekumbuka nilipokuwa chuo pale udsm niliwahi kuwa natumia rice cooker kwenye umeme wa bure wa mabibo hostel.

Nahitaji rice cooker yenye uwezo wa kupika wali kilo moja na nusu.

Brand ipi ni nzuri na bei yake?

Vipi kuhusu bajeti ya umeme. Rice cooker inakula sana umeme ? Nijiandae kwa bajeti ya umeme kiasi gani kwa mwezi maana almost kwa wiki nitakuwa napika wali kwa rice cooker.

Kingine vipi rice cooker inatoa wali ambao unakuwa umekwiva vizuri ? Au na yenyewe kuilia timing kama unapikia kwenye gesi au mkaa? With much thanks in advance
Nunua nikai naona ni nzuri
 
  • Usinunue Rice cooker.
  • Bali nunua Pressure cooker
Kwanini ununue pressure cooker?
  • Utaweza kupika wali kama kawaida
  • Utaweza kupigia Nyama
  • Utaweza kupikia Maharage
  • Kwa ujumla chochote kile waweza kupikia.
Utapika Kwa muda kidogo zadi hivyo kubana matumizi ya umeme.

Bei : Haizidi 120,000
Brand: Ailyons ( na ndugu zake), Wapi: Karikoo ziko kwa wingi
Asante sana kaka nitanunua zote rice cooker na pressure cooker
 
Kwa aboder hapo utapata performance, applicability na technology lakin huwezi kupata durability ,quality,na efficiency.
Mkuu nina mifano ya watu waliotumia hizo brands (ikiwemo mimi mwenyewe) na wanazisifia sasa sijui labda matoleo ni tofauti, kuna mahali nimeona umetaja Nikai sasa kuna watu nawafahamu hiyo brand hawataki hata kuisikia ongezea na Bosch, so mimi naona hizi brands ni suala la experience ya mtu binafsi ni kama tu kwenye vitu vingine kama simu au magari kila mtu huwa na machaguzi yake
 
Mimi natumia West Point niliinunua 2020 kwa 120,000/= Game iliyokuwa Mlimani City mpaka leo iko poa inapiga kazi.

Yani kwa jinsi nilivyoizoea ni bora nikose vifaa vyote vya umeme jikoni sio rice cooker. Ni mara chache kupika wali nje ya rice cooker na ni ikiwa ni wali nazi pekee.
Haya mama

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Good mimi kutokana na experience yangu ya kutumia hizo brand mbili ulizoziponda, nimepata hivyo vyote je ni vibaya kuzisifia, au nilitakiwa nisemee kutokana na experiences za watu wengine mkuu
Mtu aliyeendesha PASSO siku zote akiambiwa Harrier ni bora huwa hakubali.
 
Mkuu nina mifano ya watu waliotumia hizo brands (ikiwemo mimi mwenyewe) na wanazisifia sasa sijui labda matoleo ni tofauti, kuna mahali nimeona umetaja Nikai sasa kuna watu nawafahamu hiyo brand hawataki hata kuisikia ongezea na Bosch, so mimi naona hizi brands ni suala la experience ya mtu binafsi ni kama tu kwenye vitu vingine kama simu au magari kila mtu huwa na machaguzi yake
Huwezi fananisha product za NIKAI na hizo takataka za akina aborder and co. mkuu labda kama una ubia na hiyo michina low class
 
Ninayo ila sijawahi hata kupikia mara Moja kwa Sasa naitumia kama kibubu nadondosha hela siku ya valentine nimezila zote sikupenda siku nikianza nadhani sitaacha bahati mbaya hapa jirani Kuna mgahawa nikiwa na ham ya wali naenda kununua ila mi ni team ugali bamia all the way
 
Back
Top Bottom