SoC03 Mnaifahamu postportum depression?

Stories of Change - 2023 Competition

Aunt Rasta

New Member
Jul 20, 2023
1
0
Wahenga wanasema utamu wa ngoma uingie ucheze, ukweli wa jambo kama halijakukuta wewe wakati mwingine ni ngumu kumuelewa Yule anaelipitia, katika maisha yangu sikuwahi kuwaza kama kuna siku uzazi utanifanya nijione mwendawazimu, hasa vile vipindi nikilia kama mtoto mdogo asiyejua mama yake yuko wapi, hayo ni machache tu ya yale nilipitia baada ya kujifungua mtoto wangu wa kwanza.

Je, nini kilikua kinanisumbua kama mama ambae nilikua tayari kuwa na mtoto na nilifurahi sana kumuona mwanangu kwanini nilie kama mwendawazimu pekeangu, bila kupigwa wala kuumia mahali. Khali yakawaida unaweza ukadhani nilikua nadeka la hasha, nilikua nahitaji msaada lakini hata mimi mwenyewe sikuwa najua kama naumwa. Hilo lilikua tatizo la kwanza.

Kwakuwa nilikua nakaa mwenyewe muda mrefu nilikuwa natumia sana simu kujifariji na kusoma mambo mengine mengi kuhusu uzazi mitandaoni kipindi chote cha ujauzito, kitu ambacho sikuwahi kukutana nacho ni “POSTPARTUM DEPRESSION.Baada ya kupitia vipindi vichache vya kushangaza nilirudi kwenye mitandao na kutafuta kile ninachokipitia, nikatafuta ni kwanini nahisi vile nilivyokuwa nahisi au kujisikia.

Postpartum depression ni hali ya unyogovu baada ya kujifungua, baada ya kupata mtoto mambo mengi hubadilika hii husababisha mwanamke ambae anapata mtoto kwa mara ya kwanza kupitia hali hii ya unyogovu. Msasa sijaju ni wanawake wangaki kwa Tanzania hupitia hali hii, nakumbuka nilipitia maandiko ya matatibu na wanawake wengine waliotoa ushuhuda juu ya hali kama yangu katika mitandao ya kijamii.

Je, nilikua napitia hali gani baada ya kujifungua? Haya ni machache niliyapitia;

- Kulia mara kwa mara bila sababu yoyote.

- Kujiona kama unakosea jambo, hasa ulezi.

- Kuwa na hofu iliyopitiliza.

- Kulia hata pale mtoto anapolia na kushindwa kunyamaza.

- Kuhisi kuchanganyikiwa.

- Kuna na huzuni isiyo na sababu maalum.

- Kuhisi uchofu sana na kushindwa kupata usingizi.

- kuhisi unaweza ukamdhuru mtoto wako wenyewe.

Kipindi chote hiki nayapitia haya nilikua pekeangu, nisijue namueleza nani na Napata wapi msaada, lakini pia sikujua kama haya yote ni matatizo ya akili, lakini je, nilikua kichaa au kupoteza uwezo wa kuwa mama, Hapana. Hiki kilikuwa ni kipindi kifupi cha miezi miwili ya mwanzo toka nimejifungua nilikua siongelei swala hili nikiwa na watu lakini naumia kila nikipanda kitandani na mtoto wangu tukiwa wawili usiku nilikua nakosa kabisa usingizi na kishinda katika mitandao ya kijamii usiku mnene au nitamuangalia mtoto na kuanza kulia bila sababu.

Ilinichukua muda kuelewa kwanini nakuwa vile, lakini pia nilishangaa hakuna mtu yoyote ambae alishawahi nielezea juu ya swala lile hata kwa kunigusia tu. Je jambo hili ni geni kwa wataalamu wa afya mbona basi hawakutuambia nini tunaweza kutananacho huku nje baada ya kupata mtoto hasa kama mwanamke amekuwa mama kwa mara ya kwanza kama mimi kipindi kile.

Lakini pia swali langu nilijijibu mwenyewe baada ya kuangalia mazingira ambayo nilikua naishi na mtoto wangu, tunahitaji watu wa karibu sana kipindi cha kujifungua ndio maana kuna uwezekano mkubwa watu wa zamani yaani mama zenu walishawahi kukutana na hili swala ila ilikua rahisi kwa wao kupona kwa sababu ya ushirikiano wa familia na kupindi cha kumlea mama na mtoto mchanga. Kwa mfano Mtoto anapolia bibi au mtu mwingine humsaidia mama kumbembeleza na mama anapata muda wa kupumzika na kula vizuri ili aweze kuzalisha maziwa kwa wingi.jamii zetu bado zinafanya hivi lakini kwa sisi wa mjini nini kimebadilika?

Kwa kesi yangu sikuwa na watu wakunisaidia hasa wamama wakubwa au mabibi zetu kama jamii zetu za kiafrika zinavyofanya mwanamke akijifungua, hali ya maisha na msongo wa mawazo kukubali mabadiliko, kukaa mwenyewe kwa muda mrefu, mabadiliko ya homoni na mudi ilichangia kwa kiasi kikubwa sana, kukosa usingizi na mwili kuchoka.

Hayo ni yale ambayo mimi kama mama niliyapitia nimeeleza yale tu yalitokea ila kuna wanawake wengine hata leo wanaweza kutana na jambo hii na wasielewe au wenza wao wakawaona kama wanakua wendawazimu, nitaanza na wababa wale ambao wanafikiri jukumu la kumlea mtoto linaanza pale anapozaliwa, Hapana malezi ya mtoto yanaanzia tumboni mwa mama yake kama baba mpe mama ushirikiano katika hili, na kutambua kua afya ya akili ya mama inaweza kulindwa kuanzia kwenye ujauzito kwani mama hupitia madalikio mengi katika wakati huu wa ujauzito.

Ujumbe wangu kwa SERIKALI hasa sekta ya afya, pale tunapoongelea “AFYA YA MAMA NA MTOTO” Kwa wanawake na wanaume wapewe somo juu ya hali hii kama wanayosema kwa kimombo “it takes a village to raise a child” afya ya akili ya mama inaweza athiri jinsi mama anavyolea mtoto wake, kuna matatizo mengi ya akili ambayo wengi wetu wamekua wakiyajadili mara kwa mama na jambo hili kwa udogo au ukubwa wake nadhani ni jambo halijatambulika kwa watu wengi hata kwa kujua kama jambo hili ni tatizo la akili.

Tuangazie pia changamoto za maisha, hizi zinaweza pia kuchangia akili ya mama kuwa katika hali mbaya au kukosa msaada wa kutosha kutoka kwa mwenza wake, wanawake wapewe ushirikiano kwa kupatiwa wataalamu wa afya ya akili pale ambapo mama amepata dalili za kuwa na postpartum depression watu wa karibu na mama huyu wampe ushirikiano wa kutosha kama itatokea mmoja wa familia amegundua mama kapatwa na shida hii.
 
Back
Top Bottom