Mlio huko Vyuo Vikuu mnasoma sijui Masters na Doctorates zenu zina maana gani wakati hata tusio na Elimu Kubwa EAC tunatunukiwa tu Vyeti ya Heshima?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,029
109,985
Ndiyo maana GENTAMYCINE nikaamua tu kubakia na hii hii Degree yangu Moja tu kutoka Chuo Kikuu cha Werevu tupu Tanzania cha Mtakatifu Augustino Mwanza ( SAUT Mwanza ) na wala sikutaka tena sijui Kuhangaika kufanya Masters au Doctorates kama wafanyavyo Washamba wengi ninaokutana nao.

Sasa kama tu hii Degree yangu Moja ya Chuo Kikuu cha Werevu tupu Tanzania ( SAUT Mwanza ) imeweza kunifanya niwe Mwerevu, Mjenga Hoja mzuri huku hata wenye hizo sijui Masters na Doctorates zao Wananiogopa huku hadi wengine sasa wakiniita Daktari na Pofesa yanini nihangaike kwenda kufanya Masters na hizo PhD's zenu?

Kwa mfano kuna haja gani ya Mtu kujitapa kuwa ana Masters au PhD huku akiwa hata tu Kutumia Computer hajui, kufanya Presentation kwa kutumia Pojector hajui, Programs za Computer kama Power Point na Excel hajui, Kuzungumza katika Public hawezi na Kiingereza ndiyo kabisa hakijui ila katika Vyeti vyake ana A na B za Kumwaga tu?

Hivi mmeshajiuliza au tumeshajiuliza kuwa ni kwanini Wazungu wengi ( ambao Kutwa tunawapelekea Mibakuli yetu Kuwaomba Misaada ya Fedha ) wao Kipaumbele chao hasa ni kuwa tu na angalau Degree Moja na hata wakiwa na Masters au Phd huwa hawapendi Kuzitambia au hata kuwa addressed kama mwana Utopolo maaufu hapa JamiiForums Dr Matola PhD?

Kuna Mtaalam Mmoja nchini Tanzania na pia ni Mtafiti Mwandamizi wa Masuala ya Elimu aliniambia kuwa 98% ya Watanzania wanaosoma Masters wamesoma kwa kutafuta tu Sifa Mitaani ila Vichwani mwao ukikutana nao hutokutana na hizo Masters zao bali ni Upuuzi na Utoto mtupu. Alisema dhamira Kuu ya Mtu kwenda kufanya Masters ni kuja kuleta Kitu Kipya Kazini Kwako sasa unawezaje kuleta Tija Kazini Kwako wakati Masters unayoenda au uliyoenda Kuifanya Chuo Kikuu hapo Ofisini Kwako kila Mtu anayo hiyo hiyo namaanisha ya Field yako hiyo hiyo?

Akaenda mbali na hapa sasa ndiyo aliniumiza kweli kweli ambapo alisema kuwa kama Kweli hizi Doctorates ( PhD's ) zingekuwa zina Tija sehemu kama Benki Kuu, huko Bandarini na katika Madini na Nishati ambako zipo nyingi Tanzania ingekuwa inaibiwa tu kila Siku na kuendelea kuwa Masikini na Tegemezi kwa nchi za Ulaya na Marekani ambao Wao Watu Wao wala hawana muda wa Kukimbilia kufanya Masters na PhD's?

Mwisho GENTAMYCINE namalizia hivi kuna haja gani ya Mimi kuharakisha kufanya sijui Masters au PhD's wakati najua kabisa kuwa nikija kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2040 nitazipata nyingi tu kutoka Finland, South Afrika, UDOM, UDSM, Uarabuni, SUZA na Uturuki japo najua sitozitumia ila najua Ukutani Kwangu Sebuleni nitazitundika zote ili mliofanya Masters na PhD's zenu mkiziona tu muumie na mjione Mizozola ( Mijinga ) na Mipopoma ( Mipumbavu )

Haya naomba sasa nami GENTAMYCINE baada ya Kuandika huu Uzi wa Kimkakati wenye Mitego mingi mahala fulani na Ujumbe wa Kificho na Chokonozi Chokozi mkae chini na mjddiliane mtanipa Zawai gani nami ya Heshima ya Kitaaluma kwani nadhani kwa niliyoyaandika hapa nastahili Mastes au PhD ya Heshima.

Kama kawaida yangu namalizia na ANGALIZO langu Tukuka hapa chini kwa wale 'Visokolokwinyo' na 'Wawashwaji Kunako' wa mara kwa mara hapa Jamvini.

ANGALIZO

Kama unajua HUMPENDI GENTAMYCINE na Mada ( Threads ) zake hapa JamiiForums HUZIPENDI tafadhali nakushauri KIUSTAARABU tu acha KUZIFUNGUA, KUZISOMA na hata KUZICHANGIA badala yake nenda Kawasome tu wale MEMBERS wako UNAOWAKUBALI zaidi hapa na Mimi niachie wale MEMBERS wangu WANAONIELEWA KUTWA na hawana USWAHILI, UPUUZI, USHAMBA na UPUMBAVU wa KUTUKUKA kama ulionao.

Ukikaidi hili ANGALIZO langu usije KUNILAUMU kwa MAJIBU YANGU UMIZA ambayo NITAKUPOROMOSHEA pale tu UTAKAPOSHOBOKA nami kwa KUWASHWAWASHWA Kwako nami kama MNYAMA JIKE anayetaka KUPANDWA ( KUINGILIWA ) na MNYAMA DUME a.k.a GENTAMYCINE.

Nimemaliza.
 
Kwanza nimshukuru mama Dr Samia Suluhu Hassan Kwa kuamka salama.

Nikirudi kwenye hoja yako kama udaktari wetu unakuumiza roho Yule Muhindi wa Marekani anauza Honorary Causa Kwa $5000 tu, muone Babu Take au Msukuma wakupe mchongo Yule Muhindi siyo mpaka uende Marekani mkifika vichwa 10 tu anakuja mwenyewe kuwatunuku Honorary Causa.
 
Kwanza nimshukuru mama Dr Samia Suluhu Hassan Kwa kuamkia salama.

Nikirudi kwenye hoja yako kama udaktari wetu unakuumiza roho Yule Muhindi wa Marekani anauza Honorary Causa Kwa $5000 tu, muone Babu Take au Msukuma wakupe mchongo Yule Muhindi siyo mpaka uende Marekani mkifika vichwa 10 tu anakuja mwenyewe kuwatuku Honorary Causa.
Nina uhakika Watakaokuelewa kwa hii Post yako hapa ni Sisi Majiniasi wachache ila adriz na Bujibuji Simba Nyamaume hawajakuelewa na kamwe hawatakuelewa labda ungekuwa umeandika Mambo ya Ngono Ngono na Mademu zao wa Ushuani Kwao huko Mbezi Beach.
 
Sasa bwana GENTAMYCINE wewe na serikali ya mama mna tofauti gani.
Wote mnakataa kupingwa bila ya kujali mnachokipinga ni nini?

Wewe ni nani mpaka usipingwe katika unayoyasema.
 
Sasa bwana GENTAMYCINE wewe na serikali ya mama mna tofauti gani.
Wote mnakataa kupingwa bila ya kujali mnachokipinga ni nini?

Wewe ni nani mpaka usipingwe katika unayoyasema.
Mimi ni The King, Mimi ni Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer na pia Mimi ni Mshindi wa Jumla wa Tuzo ya Mwanachama Bora Jukwaa la Michezo ( Sports ) hapa JamiiForums kwa Msimu wa Shindano wa mwaka 2022/2023 lakini pia Mimi ni Member ninayesomwa na Watu wengi sana Jamvini hapa ( akiwemo Rais wako Samia, Rais Mstaafu Kikwete, Wakuu wa Majeshi, Viongozi wa Serikali na wa Siasa, Wakuu wa Usalama wa Taifa, Wanahabari, Wachezaji Mpira na wana Michezo, Wasomi, Mabalozi kama alivyokuwa Dkt. Wilbroad Slaa ) hadi na wale Wapumbavu, Wandawazimu na wenye Wivu na Chuki nami ambao pamoja na Kuhubiri kuwa HAWANIPENDI lakini hawawezi Ku Log In JamiiForums na wasiangalie MBARIKIWA WA MWENYEZI MUNGU GENTAMYCINE nimendika nini.

Kudadadeki.....!!!!!
 
Wewe ni muhaya??
 
Kwanza nimshukuru mama Dr Samia Suluhu Hassan Kwa kuamka salama.

Nikirudi kwenye hoja yako kama udaktari wetu unakuumiza roho Yule Muhindi wa Marekani anauza Honorary Causa Kwa $5000 tu, muone Babu Take au Msukuma wakupe mchongo Yule Muhindi siyo mpaka uende Marekani mkifika vichwa 10 tu anakuja mwenyewe kuwatunuku Honorary Causa.
umesahau na # ya Kigwa,

Safari yetu ya maendeleo sioni tukitoboa.
 
Wako uliowahi kuutoa wenye Akili hapa JamiiForums uko wapi? Pumbavu.
Hujawahi kuuona? You can't be serious. Ila kusema ukweli nyuzi zako hapa ni za kijinga, kiprimitive na zimejaa unsubstantiated myths. Na ningekuwa moderator ungenikoma, na ulivyo mwepesi wa matusi sasa.
 
inafikirisha sana yaani hata kina Mwijaku eti na wao intelectuals , aisee inafika sehemu mpaka unapata hasira kwanini nchi hii imeendelea kuwa ya hovyo namna hii, ila haya yote aliyaanzisha Jiwe kwa kuona hayo mataito ya MA. na ma PhD ndio kila kitu kumbe alisahau kwamba elimu ni upeo wala sio makaratasi, na ukitaka kujua sasa hakuna ishu ya maana angalia Nyerere alikuwa na Honorary Doctorates zaidi ya 24 lakini hakuwahi hara siku moja kujiita dokta sijui profesa sijui nani lakini hawa vilaza wa sasaHIVI WANAKOMAA DOKTA DOKTA. SHAME ZAO
Uzi wangu ungechangiwa zaidi na Watu Intelligent kama Wewe na Walionielewa nilichokuwa nakilenga ningefurahi mno.
 
Back
Top Bottom