Dig the EA
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 287
- 274
Kama unafanya kazi chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI ngazi za chini hususani Ualimu harafu ukapata Elimu kubwa ya juu hususani ngazi ya Masters au doctorate degree, unanielewa vizuri.
Ngazi ya Halmashauri idara ya Elimu hawazingatii mwalimu mwenye degrees mbili au tatu. Sababu ya maana haieleweki lkn husikika ikisemwa ngazi hiyo ya Elimu ni faida ya mwalimu.
Sasa nini hutokea ukiwa na Elimu hiyo; kwanza hutegemea hutakaa uendelee kufundisha, wanahisi na kuamini utaondoka. Katika mtazamo huo linaloibuka ni kuwa unaweza usifikiriwe kwa lolote kwa maana ya post ya nafasi ya uongozi hata ngazi ndogo tu kama U- headmaster na kujikuta vijana wadogo wanateuliwa na kuanza kuwaongoza wale wazoefu kazini na wenye elimu kubwa. Hali hii inafikirisha sana kwa nini maamuzi ya teuzi hizo kuwa hivyo. Lingine Kuna ishara za mtazamo hasi kutoka wa watumishi (kundi la waajiriwa) kwa watu /walimu wenye Elimu kubwa.
Mara nyingi wenye Elimu kubwa hutazamwa na kusemwa vibaya na watumishi wengine kwa vile wanafanya kazi Kama wanazofanya wenyewe. Katika hilo huwasema wasomi hao kuwa Elimu zao hazijawasaidia. Mitazamo yao wanataka ukiwa na Masters degree au doctorate degree ukakae TAMISEMI au Elimu au Wizara yoyote au kazi nyingine tofauti na kufundisha darasani.
Kiuhalisia kusoma degree ya pili au ya tatu harafu ukarudi kituoni kwako kufundisha ni changamoto sana. Kuna watu wanatamani uwezo wako wa Elimu usijulikana, Kuna watu wanataka usionekane wala kutoka. Na usiposhtuka waweza kuzeeka na kustaafu bila kuteuliwa na kupuuzwa tu.
Maana yake ni nini Elimu hiyo kwa mashuleni Kama vituo vya kazi na Halmashauri siyo sehemu sahihi ya kwenda au kupeleka masters na PhD huko. Kingine nilichokiona, Elimu ya juu nchini bado haipokelewi vzr ngazi za chini. Kuna mwamko na exposure ndogo huko. Ukisoma sana bado unaonekana threat kwa wengi. Hapo ndo utapingwa, kutengwa na kubaguliwa kwa mengi mazuri.
Hivyo kama ni mtumishi (mwalimu) na unatamani kupata Elimu hizo kubwa jiandae kwa stress, au ujiandae kabla hujaipata uwe umetafuta sehemu nyingine ya kwenda kufanya kazi lakini si kule chini kufundisha. Kuna changamoto sana.