Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 11,014
- 22,780
Kwenye dini zote vijana wa kiume tuko nyuma sana.Onana na kiongozi wako wa msikiti, umpe hicho kisa akikwambia ndoa ipo kisheria basi ruhuaa kuendelea nae(utamuacha tu kwa maamuzi yako) ila watoto wape elimu nzuri ya dini uhakikishe wameijua na usiwalazimishe upande wa kuwepo, kikubwa wape elimu.
Ima sheikh akisema ndoa hamna hapo, basi huna budi kuachia goma.
Je ulivyombadili dini ulimpa elimu ya dini, ulikuwa kiongozi mzuri kwake, ama ndio ile muislam jina, ukiwa muislam lazima uoneshe athari za uislam wako, marafiki, majirani n.k wote wapate athari kwamba huyu kweli ni muislam
Pole kwa yote mkuu.
Ni wachache sana wanaozingatia ibada.
Afadhari waislam mwezi huu wacRamadhani utawakuta vijana wameshika dini zao baada ya hapo wanapotea, wala huwezi mtambua kwa dini yake.