Mind Bending| Blowing Movies| Series| Special Thread.

Requiem For a Dream(2000).
[Spoiler alert]

Hii movie ilianza tu kuleta mkanganyiko katika jina la movie, sio sababu hawajui maana ya neno "Requiem" ila kujumuishwa kwa "For a" na sio "Of a" imeleta tafsiri tofauti tofauti.

Nimeona wengi wanasema, imewaacha na trauma, ila tatizo wanaiangalia hii movie kama ni documentary na sio horror movie.

Inawezekana sababu ya uwepo wa drugs addict or pills wengi, ndio maana wanaichukulia kama imeonesha maisha halisi.

Yote ya yote, hii ni movie iliyojaribu kuonesha kwa namna gani, katika njia ya kupambana kufanikiwa (kutimiza malengo fulani) unaweza ukapita njia isiyo sahihi.

Mama anataka kupunguza mwili wake ili akaonekane vizuri kwenye TV show, anatumia pills mwisho zinaharibu akili na mwili wake.

Vijana wanataka kufanikiwa kimaisha, wanaingia kuuza drugs mwisho wanakua drug addicts.

Pia, mwanamke nae anataka kutimiza ndoto zake anaishia kuwa malaya/kahaba.

Kupitia maelezo hayo, ndoto zao wote zinakufa. Na hii ndiyo maana angalau inaendana na title "Requiem for a Dream".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom