Filamu Zilizotabiri ‘Future of Humanity’ kwa Usahihi

Best Daddy

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
774
1,294
"Hakuna mwenye uwezo wa kutabiri mambo yatakayotokea wakati ujao kwa usahihi isipokuwa Mungu pekee". Hivyo ndivyo wanasema, maana yeye pekee anatambua mwanzo na mwisho wetu. Wataalamu wengi wamejaribu kufanya hivyo, wengi wameaibika na wengine kuapa kabisa kamwe hawawezi kuja kutabiri, baada ya kuona kila vitu walivyodhani vitatokea, havikutokea. Hii haimanishi hatuwezi kabisa kutabiri, HAPANA.

Tumeona tabiri za hali za hewa n.k angalau tunafanya vizuri kwa sasa, (Ukuaji wa teknolojia unatufanya tuwe bora kwenye mambo mengi).Ila kinachozungumzwa hapa kuwa ni ngumu kutabiri kwa usahihi(Predict the future accurately).

Pamoja na ugumu huo, kuna baadhi ya waandishi angalau wamejaribu kutabiri yatakayotokea kwa usahihi. Sasa katika Makala hii tunaenda kuona filamu zilizojaribu kuonesha kile kitakachotokea kwa usahihi.

N.B: Katika Makala hii, haitajalisha filamu imekuwa adapted kwenye kitabu, imetabiri kwa bahati mbaya au makusudi. Kitu pekee kitazungumzwa ni usahihi wa kile kilichooneshwa tu katika filamu,na uwezakano wa kutokea katika dunia halisi.

2001: A SPACE ODYSSES (1968)
Hii ni filamu kuhusu ‘Human Evolution”. Nitasamehewa, kama uliona au utaona tofafuti na hatua za “human evolution’. Uko huru kutoa tafsiri yako, maana hata Director hadi leo amekataa kutoa tafsiri sahihi ya kipi alimaanisha katika filamu hii. Wengine watajaribu kutoa tafsiri kiroho (spiritually), lakini mahali ambapo mawazo yetu yatakapo kutana ni kuwa movie imeeleza dhana ya ‘ Human evolution na Artificial Intelligence.

Hii filamu imeanza kuonesha the The Dawn of Man: picha ya Maisha ya kale, , hadi sasa tumeendelea kutengeza akili. Imeendelea kuonesha uwezo wetu wa kutengeneza Akili bandia zenye uwezo kama au kuzidi akili ya bianadamu. Imeonesha uwezo wetu wa kusafiri kutoka sayari moja hadi nyingine, hadi kufikia uwezo kutoka galaxy moja kwenda nyingine. Hii filamu imebainisha , uwezekano wa akili bandia kwenda nje ya matakwa ya kibinadamu, baadae kuwa na uwezo mkubwa zaidi kuliko binadamu, na uwezekano wa kutokea kwa aina nyingine ya ‘Human Evolution”.

Kwa ufupi imetoa picha kamili tangu enzi za our cousins (Apes- Homo Sapiens), wameanza Maisha, wamegundua vifaa, wakati huu tuliopo hadi pale atakapozaliwa mtoto katika Space/Anga(A space Child).Japo ilitoka 1968, lakini hii ni movie iliyotabiri kwa usahihi zaidi, na itaendelea kuwa na uhalisia hata zaidi ya miaka 100 ijayo. Hii ni Timeless Movie. Maana ni kama tumepita na tunaendelea kupita katika kile kilichotabiriwa katika movie.

Mfano kuhusu science ya akili badia kwa sasa imekua kwa kasi sana. Kuna baadhi ya task AI imekua bora au sawa na akili ya bninadamu. Inasemekana kuna makubwa yanaendelea huko Silicon Valley, ujio wa “Super Intelliegent—AI) hautachukua miaka mingi kama tunavyotarajia. Filamu imeonesha tumeweza kuzunguka katika space (tayari tumeona tumeweza na jitahada zinafanyika kwenda mbali zaidi), pia katika movie inaonesha A Star Child amezaliwa, japo inatafsiriwa tofauti ila , katika Makala hii, kwa kuwa naamini hadi kufikia hapa sisi ni product of evolution, basi A star Child ni aina ya human evolution nyingine ‘great stage of human evolution.

WALL-E (2008)
Katika miaka ya 2105, filamu inaonesha binadamu tumeondoka duniani, baada ya dunia kuwa si sehemu salama tena kutokana na uhatari wa mazingira. Nilitamani sana, kuelezea hii part, katika movie ya Interstellar, ambayo inatuaminisha kuwa japo tumezaliwa duniani, lakini haimaanishi maisha yetu lazima yaishie hapa. Ila kutokana na huu uzi kuwa mrefu sana, basi nitaelezea hapa hapa.

Japo kwa wengi, athari za kamazingira imekuwa sio sehemu ya fikra zetu za kila siku, lakini kwa mataifa yaliyoendelea hili jambo ni kubwa sana. Ni janga la kidunia. Ndio maana wanawekeza pesa nyingi kutafuta sayari nyingine, mfano hizi safari za kwenda Mars (US na Elon Musk). Wakati wengi, tunaamini hizo pesa wanazotumia katika safari zao , ni bora tungezitumia kuiboresha dunia yetu, ila wao wanaamini itafika wakati dunia itakua sio mahali salama kabisa, hatutaweza iokoa tena, bali tutapaswa kuondoka. .

Ukitoa zile tafiti zilizo zoeleka basi kuna baadhi ya taarifa zinasema hii hali ya joto iliyokuwa inatokea kila baada ya karne, basi sasa inatokea kila baada ya Miaka mitatu, pia hali ya Ujangwa imeongezeka mara mbili zaidi ya ile ya miaka kadhaa iliyopita. Hii kuonesha labda miaka kadhaa ijayo, sayari hii haitakuwa salama tena.

Japo movie imeonesha Maisha ya Miaka ya 2085, lakini kuna baadhi ya mambo hayo sio utabiri tena, bali ni uhalisia wa Maisha yetu ya kila siku. Filamu imejaribu kuonesha (addiction)urahibu wa watu katika technolojia hasa smart phone. Hii sio utabiri ila ni uhalisia kwa sasa. Angalia endapo upo dining, sitting room, public transport au barabarani watembea kwa miguu kila mtu yupo busy na simu yake. Hata ukiwa sehemu za starehe, kila mtu hayupo pale— busy na simu yake. " Umoja utakufa wakati tumeshikwa na simu zetu" Haya ni maneno ya Dizasta Vina.

Takwimu zinaonesha kwa wastani watu wazima(18+) wanatumia zaidi ya masaa 11 katika screen. Tayari tumeanza kupoteza uhusiano wa sisi kwa sisi, watu wako busy kwenye mitandao ya kijamii. Tumekua wavivu kufikiri huku tukiamini kile tunachokiona kwenye screen hata kama ushahidi wa dunia halisi unathibisha tofauti.

Hitimisho, kumbuka hii ni filamu ya Mwaka 2008 ambapo athari za utegemezi wa technolojia hasa smartphone haukuwepo, hivyo tutaendelea kuona athari zake zake katika miaka ijayo. Pia, jinsi teknolojia inavyoendelea kufanya kazi zile ambazo binadamu tulikua tunazifanya kila siku, labda tunaweza fika wakati wa kile kilichooneshwa katika WALL.E.

The Minority Report (2002)
Hii ni movie iliyoilenga dunia ya miaka 2054. Katika filamu hii inaonesha uwezo wa kutambua waharifu and kuzuia makosa kupitia utambuzi wa sura (Facial recognition). Hii movie imeonesha Driveless Cars, Facial recognition and predictive and personalized ads(mfumo wa utabiri na matangazo yanayokulenga muhusika).

Kuhusu utambuzi wa utendaji wa makosa, tayari tumeshuhudia mfano marekani, kupitia mfumo wao wa COMPAS, sijajua kwa sasa walipofikia, ila ni mfumo ambao walitaka uwe unatumika kutambua, kabla hawajatoa dhamana, au kumuachia huru mtuhumiwa, ana uwezo wa kufanya makosa tena baadae? Japo ulionesha kuwa ulikuwa na hali ya ubaguzi kwa “Blacks”lakini tayari ni vitu ambavyo tumeanza kuviona katika dunia halisi.

Katika interview aliyoifanya Director wa hii filamu, Spielbeg anasema kuwa wakati ujao, Television zitakuwa zinatutazama sisi na kutupa kile tunachohitaji. Hii sasa ni Kweli, tumeona DSTV tayari wame-tumia hii approach kupitia AI, sasa inaweza kurecommend vipindi maalumu unavopendelea.

Sio hivyo tu, Internet now is watching us, ndio maana hata ukisearch sasa movie, unakuta google inakuambia “you will love it”, maana tayari inajua kile unachokipenda. Angalia mfano wa reels katika Instagram yako inaendana na interest zako, vipi kuhusu recommendation za Netflix? Unakuta kabisa inakupa kile kitu ambacho kipo katika interest zao. Hivyo basi, , ni kweli TV/ Internet is watching us.

Kuhusu Magari yanayojiendesha yenyewe, tumeona tayari china wamefanikiwa kutengeneza, huku soko lake kubwa likiwa Marekani, ambapo tayari kuna barabara maalumu-kutokana na baadhi ya changamoto zilizopo kwa sasa, ila naamini kwa nguvu anayoitumia Elon Musk, kwenye Tesla siku si nyingi tutaona yakitembea mtaani, kutokana na ukuaji na ubora wa AI (Akili bandia).

IDIOCRACY (2007)
Hii ni movie inayotupa picha ya miaka ya 2505— inaonesha wakati teknolojia inaendelea kukua kiakili, basi uwezo wa binadamu kiakili unazidi kupungua. Hata wale ambao tulitegemea wawe smart nao wao uwezo wa akili umepungua. Kuanzia viongozi wa serikali hadi wanataaluma wa mambo mbalimbali. Japo ni comedy, lakini kuna uhalisia imetoa, tena kuna baadhi tunaweza kuuona katika miaka ya sasa. Japo katika dunia watu hawawezi kuwa wajinga wajinga kama ilivyooesha kwenye movie.

Lakini, ukweli lazima usemwe, wakati dunia inaendelea kuamka, mambo mengi makubwa yanaendelea kufanyika, lakini idadi ya watu werevu inapungua kila kukicha. Tunaishi katika dunia ambayo inaidadi kubwa ya watu wenye vyeti vya vyuo vikuu, lakini bado hawajaelimika.

Moja ya sababu kubwa wanasema kuwa kwa Maisha ya sasa hauhitaji kuwa na akili sana ili kusurvive katika dunia hii. Japo sikubaliani nao kwa asilimia nyingi, lakini kuna sababu zenye mantiki kama mifumo ya elimu, hii hata kwetu imetokea, ukiachana na uwezo wa kutatua au kujenga hoja, ila unakuta mtu anamaliza form IV ila hata kusoma kwa ufasaha ni changamoto.

Sasa hali ni mbaya zaidi. Ukitoa ule mfumo wa zamani wanafunzi kuangalizia, unakuta mwanafunzi wa chuo amepewa task, kupimwa uelewa au uwezo wake yeye anaenda kumpa mtu amfanyie kwa malipo. Sasa wanatumia AI kufanya kazi zao, au mambo mengine hapo unategemea nini? Hizi sio tafiti zangu, ila inaonesha kutokana na utegemezi katika teknolojia, uvivu wa kufikiri , mfumo wa masiha ya sasa, binadamu wengi wamepoteza uwezo wa kumbukumbu hata kukariri namba na password baadhi ni changamoto. Uwezo wa kufikiri na kutafakri mambo, pamoja na uwezo wa kutatua changamoto umepungua. Hili tutaliona zaidi kutoka na kuendelea kutegemea technolojia kuvaa majukumu yetu ya kiakili huko mbeleni. Maana akili ni kama misuli tu, jinsi unavyoitumia basi ndivyo inakuwa bora. Hata watafiti wengi wa Akili bandia wanakili kusema kuwa, hofu yao sio ujio wa Super intelligent AI, bali ni kupungua kwa uwezo wa akili ya mwanadamu, hili ndio wanaogopa zaidi. Na hii ni mbaya zaidi ya baadhi ya bara fulani(siwezi kulitaja, halina kabisa uhusiano na mwandishi, au wasomaji), watu wengi katika IQ test wapo chini 80(To be fair), ambayo ukitoa point chini ya 20, basi huyo mtu anaonekana mwenye tatizo la “ Intellectual disability’ (To be fair). Japo, hii changamoto inaweza tatulika.


HER (2013)
Baada ya kukumbwa na kuteseka kwa upweke, pamoja na msongo wa Mawazo baada ya kutengana na mke wake, Maisha ya theo yanabadilika baada ya kununua Computer (OS)— Samantha. Ni mfumo uliyoundwa kama mwanamke ambaye anazungumza kama mwanamke halisi, wenye uwezo wa kutimiza mahitaji yako. Baada ya Samantha kumsaidia baadhi ya mambo ya hapa na pale, Theo anaanza kumpenda Samantha , sio kama mfumo wa computer lakini kama mpenzi, maana ndio kitu kinachompa furaha.

Ni movie ambayo kwa upande wa kwanza, imejaribu kuonesha ni ngumu sana kuwa na mahusiano halisi na AI, kutokana na vikwazo kadhaa vilivyopo. Pia kutegemea sana , vitu ambayo sio binadamu kunaweza kukapoteza mahusiano kamili kama binadamu.

Ila kwa tafsiri pana, hii movie inajaribu kuonesha jinsi gani watu wameanza kutafuta companion/partnership nje ya binadamu, baada ya changamoto za hapa na pale zinapotokea.Mfano, naona watu wengi wanashauri vijana wengi wasiingie kwenye ndoa, sababu ya changamoto wanazopitia huko. 'Sikubaliani nao lakini nawaelewa kwanini wanasema hivyo.'

Kuthibisha, hili tunaona sasa wameanza kutengeza Robots za kike “Robot Wives”. Mfano baada ya kutangazwa na Elon Musk, taarifa hii ilitawala sana kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakifurahishwa kwa kusema bora tunaenda kupata wenzi ambao sio pasua Kichwa. Na hili jambo sio nadharia tena, tayari kuna Mchina mmoja aitwae, Zheng JiaJia alijipatia umaarufu, baada ya kuamua kuoa Robot, kwa maneno yake anasema amefika uamuzi huo baada ya kukosa mwenzi sahihi(binadamu). Sex toys sasa imekua sio siri tena, au jambo la aibu bali watu imekua ni sehemu ya maisha yao, kuna namna connection katika ya binadamu inapotea, hata ukienda kule kwenye page ya mapenzi, basi unakuta watu wanapenda na kuhubiri ngono, ila mahusiano hawataki. Huku Watoto wakike nao waki-generalize kuwa wanaume wote ni mbwa tu. "Fear Men, Fear Ladies" umekua ni wimbo wa taifa, hasa kwa vijana wa kitanzania.

Wito wangu, kwa yale yaliotabiriwa na kutokea kwa uzuri, tuboreshe ila kwa yale ambayo ni mengi yana athari kwetu kama binadamu inabidi kila mtu kwa nafasi yake aendelee kupambania yasilete madhara zaidi, au kwa yale ambayo bado hayajatokea basi ni wakati wa kuhakikisha tunachukua tahadhari zote kufifisha athari zake au hata kuzuia kabisa yasitokea, na hiyo ndio faida pekee ya kuweza kutambua yale yanayotarajiwa kutokea.

Mwisho kabisa; Wengine wataanza kuogopa kila wanachokiona kwenye TV na kuhisi labda hii ndio kesho yetu, hapana kesho yetu sio yale tunayaona kwenye TV (The Future is not what you see in the movies) bali ni nadharia zenye lengo la kutuburudisha, hadi pale itakapothibishwa tofauti.

Warmest Regards,
Best Daddy.
 
Huu uzi wako ni shahidi tosha kuwa watu hawapendi vitu vya kufikirisha. Hawapendi kusoma makala ndefu. Ikiwa ndefu basi pawe na ngono ndani yake. Kati ya hizo nimetazama idiocracy (kama sijachanganya). Ila nikajiuliza ile migari, mashine, majengo, mitambo katengeneza nani wakati iq za watu zimeshuka sana?

Nyingine hujaweka hapo ni matrix
 
Siyo filamu tu mkuu,nakumbuka zamani kidogo wakati simu za rununu ndiyo zinatoka kuna game flani hivi lilikuwa maarufu kwenye hizo simu,kabla hata ya vitochi,sikumbuki jina la game ila ilikuwa inafanana na buble shooter,ilikuwa kwa juu angani kuna vijitu vinapita kama ndege,halafu vinadondosha bomu,sasa kazi ya mchezaji ilikuwa ni kuvi shoot hivyo vibomu na ikibidi hivyo vindege vinavyoshusha kombora, juzi nimeangalia jinsi israel walivyokuwa wanazishusha drones na yale makombora nikajiuliza sana, so wakati wanatuletea ile game kumbe nyuma ya pazia tayari watu walikuwa site wanatengeneza iron dome? Nimeanza kuamini kuwa kuna watu wanaijua kesho,ila hawataki sisi tujue kwa ukubwa kwa sababu maalum.
 
Huu uzi wako ni shahidi tosha kuwa watu hawapendi vitu vya kufikirisha. Hawapendi kusoma makala ndefu. Ikiwa ndefu basi pawe na ngono ndani yake. Kati ya hizo nimetazama idiocracy (kama sijachanganya). Ila nikajiuliza ile migari, mashine, majengo, mitambo katengeneza nani wakati iq za watu zimeshuka sana?

Nyingine hujaweka hapo ni matrix
Couldn't agree more, Mkuu.

Kuhusu kushuka kwa IQ na Uwepo wa Maendeleo: Najaribu kufikiri k labda kwa kuwa hii movie ililenga miaka ya 2505, hayo maendeleo ni zao la miaka iliyopita kabla ya mwaka huo waliolenga.
Kwanini nasema hivyo, kushuka kwa akili za watu haiwezi ikatokea overnight (Mara moja paap), ila ni matokeo ya muda mrefu, na pia haiwezi haiwezi kuwa sawa kwa watu wote duniani.

Hili tunawza litazama sasa, pamoja takwimu kuonesha kuwa IQ za watu zinashuka, ila kuna watu mfano wa Elon Musk, Sam Altman n.k ambao wanafanya mapinduzi makubwa ndani na nje ya sayari hii.

Umenikumbusha kuhusu, The Matrix hasa ile ya 1999. Pia, kuna The Truman Show(1998) ambayo imejaribu kueleza concept za matrix kwa mtoto atleast wa miaka 11. Naamini umeiona Mkuu.
 
Siyo filamu tu mkuu,nakumbuka zamani kidogo wakati simu za rununu ndiyo zinatoka kuna game flani hivi lilikuwa maarufu kwenye hizo simu,kabla hata ya vitochi,sikumbuki jina la game ila ilikuwa inafanana na buble shooter,ilikuwa kwa juu angani kuna vijitu vinapita kama ndege,halafu vinadondosha bomu,sasa kazi ya mchezaji ilikuwa ni kuvi shoot hivyo vibomu na ikibidi hivyo vindege vinavyoshusha kombora, juzi nimeangalia jinsi israel walivyokuwa wanazishusha drones na yale makombora nikajiuliza sana, so wakati wanatuletea ile game kumbe nyuma ya pazia tayari watu walikuwa site wanatengeneza iron dome? Nimeanza kuamini kuwa kuna watu wanaijua kesho,ila hawataki sisi tujue kwa ukubwa kwa sababu maalum.
Haha. Upo sahihi Mkuu.

Yote ya yote, umenikumbusha mbali sana.
 
ohoo! nina mengi yakuandika lkn ngoja niandike kiduchu!. na kiduchu yenyewe ni hii binadamu bado yupo kwenye evolution na tutaona mengi mpaka aje akae kwenye ustaarabu uliokamilika kiuchumi,kiutawala,kijamii na kibinafsi.
Ni kweli kabisa Mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom